Hoja maalum kuhusu ukatili/mauaji ya watoto, ni nani mtetezi wa hawa viumbe innocent?

Complicator

JF-Expert Member
Aug 23, 2013
2,198
3,566
Poleni na harakati za sherehe za mwisho wa mwaka, hongera kwa kufika hatua hii angalau uko hai pamoja na majanga yote yanayopita kuisumbua dunia.

Mada hii naileta nikiwa na rekodi mbalimbali ingawa siyo kwa uhakika wa tarehe na mahala,mimi ni mfuatiliaji mzuri wa vyombo vya habari ambako ndio machimbuko ya taarifa mbalimbali.

Kipindi cha mwaka huu unaiosha nilikua makini kufuatilia zaidi habari zinazouhusu matukio ya unyanyasaji wa watoto wadogo hasa yanayopelekea vifo, ulemavu wa kudumu au matatizo ya kudumu ya kisaikolojia.

Kwa uchunguzi wangu ilikua haiwezi kupita siku tati hakujaripotiwa habari ya mtoto kuuliwa aidha na wanyama, binadamu hasa ndugu au katika mazingira ya uzembe wa kimazingira mfano mtoto aliyejiua kwa kujipiga risasi baada ya baba yake kuisahau kitandani asubuhi akiwa bafuni.

Matukio ya watoto kubakwa na kulawitiwa hasa na ndugu ambao aidha ni akina babu,wajomba au hata wazazi wa kiume,kuna matukio ya watoto kuliwa na wanyamapori kama fisi n.k

Matukio ya watoto kupigwa vibaya kwenye taasisi wanazopata elimu kwa kigezo cha kuwafundisha yamekua ni mengi sana,pia unyanyasaji wanaofanyiwa nyumbani na walezi wao hapa wakiwemo wazazi na wadada au wakaka wa kazi.

Kwanini nimezungumzia watoto?

Sababu hili ni kundi kwenye jamii ambalo bado haliko kwenye nafasi ya kuweza kujilinda binafsi zaidi ya kutegemea ulinzi wa jamii inayowazunguka (wazazi, walezi, wanafamilia, serikali, mazingira n.k) ndio maana wanawekewa sheria mbalimbali za kutambua utoto wao,maana yake hawana uwezo wa kujilinda zaidi ya kulindwa na jamii inayowazunguka kwa kuwalea kwa umakini na kuwatengenezea mazingira salama wakiwa hatika harakati zao za utoto kuelekea utu uzima.

Pamoja na kwamba kuna sheria na taratibu mbalimbali za kudeal na issue za watoto lakini bado nahisi hazitoshi ndio maana kuna ongezeko kubwa la haya matukio dhidi ya watoto.

Ikiwa hayo ni matukio machache tu yanayotangazwa na vyombo vya habari,tujiulize maswali yafuatayo.

1. Ni matukio mangapi hayatangazwi? Ukitaka fanya hesabu ni zingatia idadi ya media na coverage yake hasa maeneo kunakofanyika zaidi ukatili guu,hasa vijijini huku? Nani anajali?

2. Ni kwanini matukio haya yanaongezea kila uchwao pamoja na kwamba tunaamini kiwango cha ustaarabu kinazidi kuongezeka kwa sisi watanzania? Shida ni nini, je sheria bado hazitoshi kuwabana wanaohusika na matukio haya?

3. Je, ni kufeli kwa wanaofanya hizi harakati za kutetea haki za watoto,au tumefeli kwa pamoja kama jamii na taifa kwa ujumla.

Hali inatisha sana kuhusu watoto,wazazi tumepoteza kabisa ile hali ya upendo kwa watoto,wakifika tu miaka mitatu tunawatenga kwa kuwapeleka shule za boarding ambazo huko hawajifunzi kuhusu upendo wa kifamilia,kukutana nao ni likizo na kuwadanganyishia kwenda kubembea siku za sherehe,then boarding tena..na kwa sababu ya utoto wao hata hawajui athari ya malezi wanayopiti huko mbeleni.

Kuna video ya ajali ya jana,ukiangalia kwa makini kuna miili imebaki ndani ya gari sababu watu wazima walikua wamefunga belt za gari, lakini nani anazingatia kuhusu watoto,wale watoto wote wamerushwa nje ya gari sababu hakuna ambaye huwa anawaza usalama wa mtoto wakati wa safari wengi tunawapakata tu ila sisi ndio tunajifunga mikanda, inapotokea ajali wao ndio wanakua wahanga wa ajali hizi tunalazimisha sana kusafiri na familia nzima wakati gari ina nafasi ndogo nawe una watoto watano na mke.

Inasikitisha sana,bahati mbaya kuwazungumzia hadi siku ya watoto mwezi wa sita..hapa katikati huwezi sikia raisi wala waziri yeyote akizungumzia kwa mkazo nasuala ya viumbe hawa dhaifu na tegemezi kwetu.

Tufanye nini kuwalinda watoto?
 
Hizi taasisi za utetezi wa haki za watoto siku hizi zimegeukia mambo mengine kabisa hawana habari tena kama zamani

Hata siku ya mtoto wa Afrika sio kama zamani
 
Hio ya watoto kutofunga mkanda ipo aisee SAA zngne unakua wamama wanaendesha Gari mtoto kasimama karibia na dashboard ile wala hawana habari me Naona elimu zaidi wapatiwe
 
Back
Top Bottom