Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,195
- 25,513
Tangu Rais Magufuli atangaze kumteua Prof. Florens D.A.M.Luoga kuwa Gavana mpya wa Benki Kuu ya Tanzania almaarufu kama BOT, kumejitokeza watu wanaokosoa katika namna ya kubeza uteuzi huo wa Rais Magufuli. Hoja yao, ambayo kwangu naiona hoja nyepesi na isiyo na utafiti wowote, ni kuwa Prof. Luoga si mchumi na hivyo hakustahili kuteuliwa kuwa Gavana wa BOT.
Huwa nashauri kuwa kabla ya kuzungumza jambo kubwa na la kutiliwa maanani,ni vyema mzungumzaji akafanya utafiti kabla ya kuzungumza. Ndiyo maana Waingereza husema: no research, no right to speak (kama hakuna tafiti, hakuna haki ya kusema). Msemo huo unalenga kuzuia uropokaji na upotoshaji.
Katika wakosoaji hao, wapo wananasiasa na wasomi. Hakuna ubishi kuwa Prof. Luoga ni mbobezi katika sheria na hasa sheria za kodi. Hatupaswi kubishana kuwa Prof. Luoga si mchumi. Lakini, wakosoaji wangefanya tafiti angalau kidogo, wangesema kwa uangalifu waliyoyasema. Na, wasingeropoka na kupotosha kama walivyofanya.
Gavana wa kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania, mwaka 1966, alikuwa Mzee Edwin Mtei ambaye baadaye alianzisha CHADEMA. Mzee Mtei hakuwa mchumi. Alisomea na kuhitimu Chuo Kikuu cha Makerere Uganda Shahada ya Sayansi ya Siasa katika Historia na Jiografia mwaka 1957 akiwa na miaka 25. Aliteuliwa Gavana akiwa kijana asiyekuwa mchumi mwaka 1966.
Kama hiyo haitoshi, Naibu Gavana wa Mzee Mtei ambaye pia aliaminiwa na kuteuliwa na Hayati Mwalimu Nyerere alikuwa Hayati Bob Makani ambaye naye ni mwanzilishi wa CHADEMA. Hayati Makani alikuwa Mwanasheria. Hadi hapo, wakosoaji wanakosa na kuishiwa hoja. Prof. Luoga si Gavana wa kwanza ambaye si mchumi.
Pia, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Kwanza wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) mwaka 1967 na aliyepata mafanikio makubwa katika uchumi, Hayati Dr. Amon Nsekela hakuwa mchumi. Alisomea Shahada zake za Awali na Uzamili za Sanaa katika Historia. Tena, mmoja wa Mawaziri wa Fedha, Mipango na Uchumi wa Tanzania aliyepata mafanikio makubwa, Mzee Cleopa David Msuya hakuwa mchumi.
Mzee Msuya alisomea Shahada ya Sanaa katika Sosholojia. Hata huko ughaibuni, aliyekuwa Waziri wa Fedha wa Uingereza na baadaye Waziri Mkuu baada ya Blair, Gordon Brown hakuwa mchumi. Alisomea shahada ya Sanaa katika Historia katika Chuo Kikuu cha Edinburgh huko Uskochi. Hadi hapo, wakosoaji wa uteuzi wa Rais Magufuli wameishiwa na kupotea.
Nawahakikishieni kuwa uteuzi wa Gavana mpya wa BOT, Prof. Florens Domonick Andrew Makinyika Luoga upo sahihi kisheria na kiuhalisia. Sheria inampa sifa za kuteuliwa kuwa Gavana kwakuwa sheria ni moja ya taaluma anazopaswa kuwanazo Gavana. Tena, Rais Magufuli alidokeza, kuwa BOT wapo wachumi watakaofanya kazi na Prof. Luoga.
Wakosoaji mjifunze kutafiti kabla ya kuropoka na kupotosha. Kinachotakiwa ni utendaji!