Hoja kuu mbili kuhusu taarifa iliyosambazwa na ubalozi wa Marekani, Tanzania

Asante huu ndio uzalendo
Aaah nimecheka mpaka basi,hivi nikuulize Paschal kwa bahati mbaya limetokea ilo shambulizi na watu wakafa ,je tunaweza kuwalaumu polisi wetu au na washirika wetu wa kimataifa ?
Pili,hivi sera na taratibu za ulinzi na usalama wa Marekani asa katika Sera za mambo ya nje kabla ya kushambuliwa na baada ya kushambuliwa bado ni zile zile . Wahenga wanasema bora kinga kuliko tiba. NOTE: Mzungu mmoja wa Marekani kwa nchi yao ni muhimu sana tena sana..sisi huku kiongozi anapigwa risasi hadhari,Azory na Ben wamepotea,viongozi wa CHADEMA wamekatwa mapanga ila serikali yetu ya kizalendo ipo kimya ..
Katika ili tuwashukuru wamarekani kwa upendo na utu wao kutupa taadhari.
 
Mdharau mwiba mguu huota tende. Hiyo ni tahadhari unaweza kuifanyia kaz au kuipuuza. Lkn ukipuuza na ikija kutokea utajilaumu mwenyew kwa upu.uzi uliyoufanya, na isipotokea basi maisha yataendelea. Usikimbilie kupingana na hawa wa2 b4 ya kufanya tafiti au uchunguz wa kina kwa hicho walichotahadharisha. Waliulize Kenya na Ethiopia ambao walipuuza kilichokuwa kinatahadharishwa na hawa jamaa nini kiliwatokea baada ya kupuuza tahadhari!
1132098

1132099
 
Aaah nimecheka mpaka basi,hivi nikuulize Paschal kwa bahati mbaya limetokea ilo shambulizi na watu wakafa ,je tunaweza kuwalaumu polisi wetu au na washirika wetu wa kimataifa ?
Pili,hivi sera na taratibu za ulinzi na usalama wa Marekani asa katika Sera za mambo ya nje kabla ya kushambuliwa na baada ya kushambuliwa bado ni zile zile . Wahenga wanasema bora kinga kuliko tiba. NOTE: Mzungu mmoja wa Marekani kwa nchi yao ni muhimu sana tena sana..sisi huku kiongozi anapigwa risasi hadhari,Azory na Ben wamepotea,viongozi wa CHADEMA wamekatwa mapanga ila serikali yetu ya kizalendo ipo kimya ..
Katika ili tuwashukuru wamarekani kwa upendo na utu wao kutupa taadhari.

Vyombo vya ulinzi na usalama vipo macho
1132102
 
Na, Ibrahim Haroub Geveva

Nikiwa katika shughuli za kikazi za Umoja wa Mataifa hapa Geneva, nimefadhaishwa na namna Ubalozi wa Marekani Tanzania ulivyotoa taarifa ya UZUSHI huko Tanzania.

Mwaka 1998, hao ndugu walipigwa na hawakutoa tahadhari yoyote Dar es Salaam wala Nairobi. Nakumbuka nilikuwa Sudan wakati huo katika shughuli za Kanda ya Mashariki ya UN.

Hakukuwa na taarifa zozote za tahadhari kama huu uzushi. Jiulize kwa nini leo wametoa, tena siku ya Bajeti ya Nchi inapojadiliwa, Siku ambazo Watalii wengi wanakwenda kwa makundi
makubwa Tanzania, Kuna nini hapo kimefichika?

Nimemuuliza Mtoto wa Shemeji yangu anayefanya kazi Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam, amethibitisha hata Ubalozi wenyewe umeshangazwa na aliyechapisha taarifa hiyo katika mitandao ya kijamii bila kujiridhisha.

Wanahojiana, hivi walishindwa hata kuwapatia Polisi Oysterbay wachunguze? Au hata wale walinzi wa pale FFU au G4S ambao wanalinda Ubalozi wao?

Walishindwa kuwapa JWTZ? walishindwa kuwapa Usalama wa Taifa waseme wanayojua? Je huu sio ujasusi uliopindukia katika nchi za wenzao?

Hayo maswali lazima yawasukume Wamarekani kuwaomba radhi washirika wao katika masuala ya Kiusalama. Kuna Mikataba ya Kimataifa inayowataka kushirikiana na vyombo vya ndani ya nchi husika wanapofuatilia mambo yanayohusu masuala ya ndani ya nchi.

Wamarekani hadi wanatoa kauli, walituma wachunguzi wao Masaki?Je, waliomba kibali Wizara ya Mambo ya Nje Tanzania au hata Umoja wa Mataifa? Wanatumia njia gani kuchunguza mambo nchini Tanzania hadi kutoa kauli ya namna hiyo?

Nani amewathibitishia huko mitaani hizo taarifa hadi kuchapisha katika tovuti yao? Tujiulize sote haya maswali.

Hivi Balozi wa Tanzania nchini Marekani hata akiwa na taarifa yoyote ya nchi hiyo ndio atoke kwa umma pale Washington DC kutangaza anachojua kuhusu Marekani?Sisi watu wa Diplomasia tunahoji, hiyo ni diplomasia ya wapi?

Basi ukiona hivi kuna jambo wanatengeneza kwa makusudi, si vinginevyo. Watanzania tuwe AMKENI.

Marekani, waombeni RADHI Watanzania na lazima mjenge tabia ya kufanya kazi na vyombo vya dola vya Tanzania katika kazi zenu. Umoja wa Mataifa unafuatilia jambo hili kwa karibu
Njoo Tanzania uendelee kutembelea maeeneo yaliyotolewa tahadhari ni siyo wewe uko nchi salama halafu unatuamisha utumbo wako hapa, polisi wenyewe wamekiri taarifa hizi zipo na wanazo sasa wewe unawashwa nini hadi uanze mitizamo isiyo chanya wakati ikitokea kweli tulioko huku ndo tutaathirika
 
Ikiwa Mambo sasa amekubali kulifanyia kazi swala hili basi taarifa hii hauwezi kuiita ya uzushi kama mleta mada anavyodai mpaka pale polisi wenyewe watapothibitisha kwamba hii taarifa ni ya uzushi. Mleta mada anaweza kuwa ni mmoja wa wanaopanga hiyo mipango ya kufanya shambulizi. So anawahi huku kukanusha taarifa ili kuvipoteza maboya vyombo vya usalama vidharau tahadhari ili yeye na wenzake wafanye walichokikusudia
 
*WATANZANIA TUWE MACHO NA WAMAREKANI NA WASHIRIKA WAO.*

Juni 19, 2019.
Kwa uzoefu wangu wa ufuatiliaji wa masuala ya kidiplomasia na siasa za kimataifa, kilichofanywa na Ubalozi wa Marekani katika Tahadhari yao iliyotolewa saa 1:19 Jioni tarehe 19 Juni, 2019 kuwa kuna minong’ono ya kutokea mashambulizi katika maeneo ya Masaki hususani katika hoteli na migahawa inayotumiwa mara nyingi na watalii na pia maeneo ya Slipway Msasani ni Mikakati ya makusudi isiyoitakia heri Tanzania.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa kupitia akaunti rasmi ya Twitter ya Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Marekani imekiri kuwa haina ushahidi wa kuwepo kwa tishio hilo na muda ambao mashambulizi yatafanyika na inawataka wananchi kuchukua tahadhari.

Kwa tabia za Marekani hasa pale wanapokuwa hawakubaliana na baadhi ya mambo kwa Taifa fulani hii ni mbinu ambayo huitumia ili kudhohofisha Serikali kwa kuwatisha Watalii, wawekezaji, Wafanyabiashara na hata wananchi wenyewe. Yapo maeneo ambayo hufikia hata hatua ya kutekeleza mashambulizi yenyewe ili mradi ionekane nchi hiyo sio salama na Serikali inashindwa kusimamia usalama wa nchi yake.

Huu ni ukoloni wa kupigiwa mfano na haukubaliki hata kidogo.

Zipo hoja kadhaa za kujiuliza kwenye tahadhari hii ya Marekani

1. Mkataba wa Vienna unaosimamia masuala ya Ubalozi na mashirika ya kimataifa katika nchi nyingine unaelekeza pamoja na mambo mengine, ni makosa kuingilia mambo ya ndani ya nchi ambayo Ubalozi upo. Mkataba huu unaelekeza kuwa kama kuna jambo lolote basi Ubalozi ama Shirika husika liwasiliane na Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje. Kwenye jambo hili Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umekiuka kwa makusudi kwa sababu ni mpango mahususi wa kuichafua nchi.

2. Ubalozi wa Marekani unatoa taarifa nyeti kama hiyo kwenye jamii bila kuwa na uhakika na jambo lenyewe. Tena unakiri kuwa hauna ushahidi. Hili ni jambo la ajabu na hatari sana hasa linapotolewa na Ubalozi wa nchi yenye hadhi kama Marekani. Maana ya hili ni moja tu kufanikisha mpango wake wa kuichafua nchi baada ya kuona njia zote zingine haziwezekani. Kulikuwa kuna ulazima gani kwa Ubalozi wa Marekai kutangaza kupitia Twitter kwa jambo ambalo hawana uhakika nalo tena bila hata kuvijulisha vyombo vya ulinzi na usalama na Wizara ya Mambo ya nje ya nchi?

3. Kilichofanywa na Ubalozi wa Marekani ni kama kujivika usemaji wa masuala ya usalama kwa Tanzania, nchi ambayo ni Huru na ina uhuru wa kufanya mambo yake yenyewe. Ni vizuri Watanzania wakajiuliza hivi leo Balozi wa Tanzania nchi Marekani Mhe. Wilson Masilingi atoe taarifa kwa vyombo vya habari kuwa kuna minong’ono imeenea kuwa maeneo fulani ya Jiji la New York ama Washington DC yatashambuliwa na anatoa tahadhari kwa wananchi huku akikiri kuwa hana uhakika na minong’ono hiyo, PATAKALIKA?

4. Kama kweli kuna hiyo hatari isingekuwa busara kwa Marekani kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kupanga namna ya kukabiliana na mashambulizi hayo badala ya kukimbili kutangaza kwenye mitandao ya kijamii. Ama kuvijulisha vyombo vya ulinzi na usalama ili vyenyewe ndivyo vichukue hatua ya kutangaza na kuweka tahadhari?

Lakini pia ni vizuri Watanzania tujiulize kwa nini mambo yafanyike leo siku ambayo Jarida la Forbes limeitangaza Tanzania kuwa nchi inayoongoza kwa Amani katika Afrika Mashariki?

Kwa nini yatangazwe leo wakati ambapo Tanzania inaendelea kung’ara kila mahali kwa msimamo wa Rais wake Dk. John Magufuli ambaye ameamua kupigania maslahi ya Watanzania dhidi ya unyonyaji uliofanywa na watu na makampuni mbalimbali yakiwemo ya Kimarekani kama vile Symbion, kampuni iliyoleta vichwa vya Treni bila kuzingatia utaratibu na mengine mengi yaliyojiandaa kutupiga katika gesi, madini na mikataba ya kinyonyaji?

Mchezo kama huu umeshafanywa na Marekani katika maeneo mengi baadhi yake ni Korea Kaskazini ambako sote tunajua mzozo uliopo kati ya nchi hiyo na Marekani, Canada na Uganda kwa kutaja machache.

Najua wapo wanasiasa wa upinzani nchini Tanzania ambao kwa umbumbu na ubinafsi wao watashangilia na kuunga mkono kinachofanywa na Marekani lakini Watanzania ni lazima tuwe macho na jambo hili.

Wamarekani ni wazuri sana kwenye kuharibu amani na uchumi wa nchi ambazo wanalazimisha maslahi yao. Na hutumia mbinu hii hii ya kuwatumia watu wa ndani na hapa kwetu wanatumiwa wanasiasa wa vyama vya upinzani. Walifanya hivyo Libya yanayowakuta Libya leo kila mtu anayaona, wamefanya Tunisia na kwingineko.

Watanzania tuvisikilize vyombo vyetu vya ulinzi na usalama, na bahati nzuri tayari vimeshazungumza kuhusu jambo hili. Tuwaambie wawekezaji, wafanyabiashara na watalii ambao wanakuja kwetu Tanzania kuwa nchi yetu ipo salama na vyombo vya ulinzi na usalama vipo na vinaendelea na majukumu yake ya kila siku ya kulinda usalama wa nchi na watu wake. Hata siku moja jukumu la ulinzi wa nchi yetu halijawahi kuwa mikononi mwa Wamarekani na nchi yetu ina historia ya kuwa kisiwa cha amani na utulivu.

Kwao Marekani kila uchao watu wanauawa kwa kupigwa risasi, tena ni nchi ambayo silaha za moto zinauzwa kama saa ya mkononi. Silaha zimezagaa kila mahali na mauaji ya kutumia silaha yametamalaki lakini hata siku moja Balozi wa Tanzania hajawahi kutangaza hali ya hatari katika Marekani.

Huu ni uhuni.

Wasituvuruge.
 
Umejitahidi kuandika sana ila nasikitika umeandika pumba, kumbuka lengo lao kubwa ni kuwanusuru wamarekani wenzao endapo kukitokea tatizo.

Ila ni kujiongeza tu kua wamesema hawana ushahidi ila hiyo ni akili tu kiukweli nchi yenye intelijensia kama marekani tayari ushahidi wanao ni kwamba wanaisaidia serikali kufatilia na kama vyombo vya usalama vikiomba msaada watatoa pia kwa maana ya leads.

Tatizo kila kitu tumeweka siasa mpaka majanga yatokee ndipo tuanze kufikiria. Tahadhari kabla ya hatari. Mmarekani hawezi kuja kukuzushia ujinga ka huo eti ndio anufaike, au aoneshe kutokuikubali serikali.

Cha muhimu ujumbe umefika watu wawe makini na vyombo vya usalama viwe macho zaidi.
 
Tukusaidie tuu mtoa thread, mwaka huu indonesia waliambiwa kunaweza kuwa na shambulio wakapuuzia! Kilichotokea wote tuliona! Kwani kuna ubaya gani ukipewa tahadhari! Au hiyo tahadhari ulitaka upewe na mambowakatihuu??? Kwa utawala huu unategemea watoe tahadhari my foot! Kama unaweza puuzia lkn pia unasema lazima kuwe na credible source? Aisee haya mambo huanza kama rumors ndo stage iliyopo then reality will hit us hard! Bora mimi ntachukua tahadhari.

Usiwe kama watu wa mtwara kuhusu kimbunga! Baada ya kuwakosa kimeelekea mozambique wanalalama kwa nini mlitupa tahadhari mbona hatujafa? Really like really???
 
Ikiwa Mambo sasa amekubali kulifanyia kazi swala hili basi taarifa hii hauwezi kuiita ya uzushi kama mleta mada anavyodai mpaka pale polisi wenyewe watapothibitisha kwamba hii taarifa ni ya uzushi. Mleta mada anaweza kuwa ni mmoja wa wanaopanga hiyo mipango ya kufanya shambulizi. So anawahi huku kukanusha taarifa ili kuvipoteza maboya vyombo vya usalama vidharau tahadhari ili yeye na wenzake wafanye walichokikusudia

Ninakubaliana na wewe mia kwa mia, huwezi kupewa tahadhari na super power ambalo kila wakati hutoa warnings kama hizo na mambo yanatokea kama kule Kenya, Ethiopia na kungineko! Dawa ni kuwa pro active as a nation! Mtu yupo Geneva, anakanusha, huo ni uwendawazimu wa Rais husema ni “wapumbavu”! Wala rushwa, mafisadi na wanaopenda penda vyeo(power hungry and greedy politicians) hawana raha kuona jinsi Rais Dr Magufuli anavyoongoza nchi ya Tanzania!!!wanaumia saaaaana!
 
Ubalozi wa Marekani wametoa tahadhari hii kwa raia wao, hii huwa ni kawaida yao kwa sehemu yeyote duniani pale wanapopata intelligence au tetesi za shambulio au tukio lolote lenye nia ya kudhuru ambapo raia wao wanaweza kuwa ni waathirika. Kwa sababu nchi yetu ya Tanzania haina utaratibu huu wala uzalendo wa kuthamini uhai wa raia wake basi mnataka kulazimisha kila nchi iwe magoigoi kama sisi. Watu wanatekwa na kuuawa Tanzania lakini serikali na vyombo vya usalama wala havina muda na havioni hata umuhimu wa kulinda uhai wa raia.
 
Na, Ibrahim Haroub _Geveva_

Nikiwa katika shughuli za kikazi za Umoja wa Mataifa hapa Geneva, nimefadhaishwa na namna Ubalozi wa Marekani Tanzania ulivyotoa taarifa ya UZUSHI huko Tanzania.

Mwaka 1998, hao ndugu walipigwa na hawakutoa tahadhari yoyote Dar es Salaam wala Nairobi. Nakumbuka nilikuwa Sudan wakati huo katika shughuli za Kanda ya Mashariki ya UN.

Hakukuwa na taarifa zozote za tahadhari kama huu uzushi. Jiulize kwa nini leo wametoa, tena siku ya Bajeti ya Nchi inapojadiliwa, Siku ambazo Watalii wengi wanakwenda kwa makundi
makubwa Tanzania, Kuna nini hapo kimefichika?

Nimemuuliza Mtoto wa Shemeji yangu anayefanya kazi Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam, amethibitisha hata Ubalozi wenyewe umeshangazwa na aliyechapisha taarifa hiyo katika mitandao ya kijamii bila kujiridhisha.

Wanahojiana, hivi walishindwa hata kuwapatia Polisi Oysterbay wachunguze? Au hata wale walinzi wa pale FFU au G4S ambao wanalinda Ubalozi wao?

Walishindwa kuwapa JWTZ? walishindwa kuwapa Usalama wa Taifa waseme wanayojua? Je huu sio ujasusi uliopindukia katika nchi za wenzao?

Hayo maswali lazima yawasukume Wamarekani kuwaomba radhi washirika wao katika masuala ya Kiusalama. Kuna Mikataba ya Kimataifa inayowataka kushirikiana na vyombo vya ndani ya nchi husika wanapofuatilia mambo yanayohusu masuala ya ndani ya nchi.

Wamarekani hadi wanatoa kauli, walituma wachunguzi wao Masaki?Je, waliomba kibali Wizara ya Mambo ya Nje Tanzania au hata Umoja wa Mataifa? Wanatumia njia gani kuchunguza mambo nchini Tanzania hadi kutoa kauli ya namna hiyo?

Nani amewathibitishia huko mitaani hizo taarifa hadi kuchapisha katika tovuti yao? Tujiulize sote haya maswali.

Hivi Balozi wa Tanzania nchini Marekani hata akiwa na taarifa yoyote ya nchi hiyo ndio atoke kwa umma pale Washington DC kutangaza anachojua kuhusu Marekani?Sisi watu wa Diplomasia tunahoji, hiyo ni diplomasia ya wapi?

Basi ukiona hivi kuna jambo wanatengeneza kwa makusudi, si vinginevyo. Watanzania AMKENI.

Marekani, waombeni RADHI Watanzania na lazima mjenge tabia ya kufanya kazi na vyombo vya dola vya Tanzania katika kazi zenu. Umoja wa Mataifa unafuatilia jambo hili kwa karibu
Sio siri..nlipofika hapa
"
Nimemuuliza Mtoto wa Shemeji yangu anayefanya kazi Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam, amethibitisha hata Ubalozi wenyewe umeshangazwa na aliyechapisha taarifa hiyo katika mitandao ya kijamii bila kujiridhisha. ""
Nahitimisha kwa kusema alieandika hii kitu awe serious.
 
Back
Top Bottom