Hoja korofishi: Tujitokeze kwa wingi tukiwa kifua mbele Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere kuipokea timu yetu ya Taifa Stars. Imeweza!

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,196
25,516
Natoa wito kwa watanzania wenzangu wazalendo kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam kuipokea Taifa Stars itakayorejea kutokea Misri kwenye mashindano ya Mataifa ya Afrika. Ilikuwa mara yetu ya pili kushiriki. Tumejifunza mengi.

Tukiwa kifua mbele, tujazane uwanjani na pembezoni mwa barabara kuilaki timu yetu ya Taifa iliyofungwa mabao manane tu na kufunga mawili kwenye mechi tatu dhidi ya Senegal, Kenya na Algeria. Ushiriki wetu kule Misri uwe funzo kubwa kwetu. Mosi, kutochanganya siasa na michezo. Pili, kutofanya matumizi yasiyo ya lazima kwenye soka letu.

Timu zote za Taifa zenye mafanikio zina maandalizi makubwa. Kuanzia kuwaandaa wachezaji tangu wakiwa makinda; kupata kocha na benchi la ufundi bora; kuwa na mashabiki wenye mshikamano na maelewano na hata hamasa kutoka kwa wadau. Kwetu sisi hatujachelewa. Maandalizi ya timu zetu za taifa yafanywe mapema kwa kila linalopaswa kufanywa badala ya kuendeshwa kwa hisia.

Inapofikia watanzania wenzetu, tena wakiwa hapa hapa Tanzania, wakiiombea Taifa Stars ishindwe, si jambo jema. Ni dalili ya hatari kwenye Umoja na mshikamano wetu kama nchi. Kwangu mimi, naiona sababu ya kuchanganya siasa na soka ikichangia. Soka lilikuwa hatarini kutumika kisiasa kwa maslahi ya vyama vya kisiasa au ya wanasiasa. Hili si jambo la mbolea.

Tutembee vifua mbele, one day YES. We are on the right track!😀
 
Wataenda hawa
IMG-20190624-WA0010.jpeg
IMG_20190624_003243.jpeg
 
Natoa wito kwa watanzania wenzangu wazalendo kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam kuipokea Taifa Stars itakayorejea kutokea Misri kwenye mashindano ya Mataifa ya Afrika. Ilikuwa mara yetu ya pili kushiriki. Tumejifunza mengi.

Tukiwa kifua mbele, tujazane uwanjani na pembezoni mwa barabara kuilaki timu yetu ya Taifa iliyofungwa mabao manane tu na kufunga mawili kwenye mechi tatu dhidi ya Senegal, Kenya na Algeria. Ushiriki wetu kule Misri uwe funzo kubwa kwetu. Mosi, kutochanganya siasa na michezo. Pili, kutofanya matumizi yasiyo ya lazima kwenye soka letu.

Timu zote za Taifa zenye mafanikio zina mandalizi makubwa. Kuanzia kuwaandaa wachezaji tangu wakiwa makinda; kupata kocha na benchi la ufundi bora; kuwa na mashabiki wenye mshikamano na maelewano na hata hamasa kutoka kwa wadau. Kwetu sisi hatujachelewa. Maandalizi ya timu zetu za taifa yafanywe mapema kwa kila linalopaswa kufanywa badala ya kuendeshwa kwa hisia.

Inapofikia watanzania wenzetu, tena wakiwa hapa hapa Tanzania, wakiiombea Taifa Stars ishindwe, si jambo jema. Ni dalili ya hatari kwenye Umoja na mshikamano wetu kama nchi. Kwangu mimi, naiona sababu ya kuchanganya siasa na soka ikichangia. Soka lilikuwa hatarini kutumika kisiasa kwa maslahi ya vyama vya kisiasa au ya wanasiasa. Hili si jambo la mbolea.

Tutembee vifua mbele, one day YES. We are on the right track!😀
Si mbaya kama tutakuwa tumejifunza lolote kwa wenzetu.
 
Tutembee vifua mbele, one day YES. We are on the right track!
wazo la kijinga.
 
Pierre alipewa tiketi ya kwenda Misri kushangilia.
RC wa Dar aliruhusiwa na Mh.Rais kwenda kuhamasisha timu yetu.Bahati mbaya tumeshindwa,basi tujitoe hiyo kesho Inshaallah kuwapokea.
 
Back
Top Bottom