Hoja: Jeshi la polisi livunjwe na liundwe upya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja: Jeshi la polisi livunjwe na liundwe upya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by 255Texter, Sep 6, 2012.

 1. 255Texter

  255Texter Senior Member

  #1
  Sep 6, 2012
  Joined: Aug 31, 2007
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ndugu zangu Watanzania wenye mapenzi ya kweli kwa Taifa letu, naandika maneno haya huku moyo wangu ukuwa mzito sana kutokana na mauaji ya kila siku yanayoendeshwa na chombo tulichokikabidhi ridhaa ya kulinda usalama wetu.

  Jeshi la Polisi ni chombo muhimu katika jamii ambacho katika jamii huru na zenye kufuata utawala wa sheria, ni chombo kinachoaminiwa na kupendwa na raia.

  Kwetu Tanzania, ni dhahiri kwamba jeshi la Polisi limepoteza uhalali wa kuwa chombo cha kulinda amani na usalama wa raia na mali zao.

  Sababu ya kwanza ya jeshi hili kupoteza uhalali wake, ni mfumo mzima wa uongozi wake ambao kama ilivyo kwa vyombo vingine vya dola (TAKUKURU nk), unatokana na uteuzi wa Raisi na unatumikia matakwa ya Raisi na chama chake. Hivyo, uongozi wa chombo cha kuhakikisha usalama wa raia wote(wana-CCM na wasio wana-CCM) unafanya kazi yake si kwa misingi ya uadilifu wa "Profession" ya upolisi, bali kwa kufuata maagizo na matakwa ya wanasiasa.

  Sababu ya Pili ambayo inahusiana na hiyo ya kwanza, ni ukiukwaji wa maadali na utaratibu mbovu katika kusaili, kuchagua na kuajiri waTanzania wenye sifa za kujiunga na Jeshi hilo. Si ajabu siku hizi kuona watu wenye rekodi za uhalifu na kuwahi kushitakiwa na/au kutiwa hatiani kwa uhalifu, ndio wanaajiriwa kuwa mapolisi. Pia, kupotea kwa maadili hayo katika mfumo wa ajira ya Polisi inapelekea watu wenye vyeti vya kughushi kuwa na ujasiri wa kuwasilisha vyeti hivyo katika maombi ya ajira ndani ya Polisi. Hiki ni kipimo cha jinsi gani Jeshi la Polisi limeshindwa wajibu wake wa msingi, kwani ni moja ya majukumu ya Jeshi hilo kutafiti, kugundua na kufichua cyeti au kielelezo chochote ambacho ni cha kughushi.

  Ingawa matatizo ni mengi yanayowakabili askari Polisi, ikiwemo ujira mdogo, ukosekanaji wa vitendea kazi nk, lakini sababu hizo mbili nilizoanisha hapo juu ndio msingi wa kuporomoka kwa utendaji ndani ya jeshi hilo na kulifanya lipoteze uhalali wake wa kuendelea kuwepo kama chombo cha ulinzi wa usalama wa raia na mali zao. Ni kutokana na sababu hizo za msingi, ndio maana tunasikia askari Polisi wakihusishwa na ujambazi na vitendo vingine vingi vya uhalifu. Uongozi mbovu uliotokana na ajira zisizofuata taratibu madhubuti, ndio kiini cha kuwa na viongozi wa Polisi ambao wanaagiza askari wao kuleta "mshiko" pale askari hao wanapopangiwa kufanya doria. Si ajabu basi, kwa uongozi wa aina hiyo kuwaagiza askari wao kufanya mauaji ama kwa nia ya kuficha ushahidi (Ref. URT vs Zombe) au kutekeleza maagizo ya mabosi wao wa kisiasa. Kwa kifupi hakuna maadili ya Kipolisi kwa kuwa mfumo mzima umekufa.

  Kwa sababu hiyo basi, hatuna budi sisi kama wananchi, kuweka shinikizo la kutaka Jeshi hilo livunjwe na kuundwa upya. Uvunjwaji wa Jeshi hilo ufuate mpangilio maalum, kama ifuatanyo:

  1) Iundwe Tume/Kamati Huru chini ya moja ya Majaji waliostaafu (e.g. Jaji Augustino Ramadhani)
  2) Uongozi wote wa Juu wa Jeshi (IGP pamoja na Makamishna wote) katika makao makuu waondolewe/wastaafishwe na nafasi zao kukasimiwa na Tume. MaRPC wote pia waondolewe.
  3) Tume ifanye mpango wa kuajiri kwa mkataba maalum, maafisa wa Polisi kutoka nchi za jumuiya ya madola (Ghana, Nigeria, Uganda) ili kuchukua madaraka ya uongozi katika Makao Makuu. Pia kupata ushauri wa kitaalam kutoka nchi marafiki (e.g. Schotland Yark-UK)
  4) Tume ifanye usaili na uhakiki wa maafisa wa Polisi kuanzia cheo cha Inspector kwa msaada wa wataalamu hao kutoka nchi za nje, ili kuweza kupata wachache wenye uadilifu wa hali ya Juu na rekodi safi, ili wakaimishwe madaraka ya u-RPC.
  5) Tume kwa kushirikiana na uongozi mpya wa juu katika Jeshi, lianze usaili na uhakiki wa askari wote, ili kuthibitisha vyeti vyao, historia zao kimaisha na rekodi zao za kazi. Wale watakaothibitika kuwa sio safi, waondolewe mara moja na ikibidi kushtakiwa kama watagunduliwa kughushi vyeti au historia zao za maisha.


  Tume ipewe muda wa miaka mitano wa kulisafisha Jeshi la Polisi na baada ya kipindi hicho cha mpito, iundwe Tume ya Kudumu ya Usimamizi wa Jeshi la Polisi, ambayo itaundwa na Bunge na kutoa ripoti yake kwa Kamati ya Bunge inayosimamia Wizara ya Mambo ya Ndani. Hii itakuwa ni mwisho wa ukiritimba wa viongozi wa CCM wa kulitumia Jeshi la Polisi kwa manufaa yao kisiasa.

  Nawakilisha!
   
 2. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2012
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Una hoja nzuri lakini si kwa serikali hii kiziwi!
   
 3. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono hoja ..... hata kwenye katiba mpya napendekeza neno jeshi lifutwe na badala yake iwe service ..... muundo mpya utapelekea kuitwa Tanzania Police Service (TAPS) ..... South Africa wana South African Police Service (SAPS)

  More over ... policing is not force but enforcing
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  Sep 6, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu ipeleke hoja kwenye maoni ya katiba mpya. Wenzetu Kenya walitumia mwanya wa katiba mpya kuunda upya vyombo vya dola ikiwemo magakama, KACA na hata polisi inatakiwa iundwe upya. Tukitumia vizuri mchakato wa katiba tutapata vitu vingi vyenye manufaa na tukiikosa hii fursa tutakuja kuijutia. Vipo vingi vya kuvunjwa na kuundwa upya kuanzia mahakama, Polisi, PCCB, nk. Vinatakiwa viundwe upya na kufanya kazi kwa manufaa ya wananchi wa nchi na si kwa manufaa y wanasiasa.
   
 5. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #5
  Sep 6, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Livunjwe una kihere here wewe njoo hapa Simba kapakatwa tukukune
   
 6. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #6
  Sep 6, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,787
  Likes Received: 36,795
  Trophy Points: 280
  Kwa upande wangu natofautiana kidogo na mtoa mada.
  Nashauri tuanze kubadili mfumo uliopo ktk chuo cha mafunzo ya jeshi hili,
  Tubadili mfumo wa kuonea na kunyanyasa polisi wakiwa ktk mafunzo yao hapo ccp kwani mfumo uliopo wa sasa ni wa kunyanyasa askari waliopo mafunzoni na kusababisha askari hao kuwa wakatili na waonevu dhidi wa raiya kutokana na uonevu na unyanyasaji wanaopata wakati wa mafunzo hapo ccp.
  Tubadili mfumo wa mafunzo kutoka yale ya ukatili na kuwafunza polisi hawa kuwa rafiki wa raiya na kuwaelekeza kuwa karibu na raiya na kuwatumikia badala ya kuwafundisha roho mbaya dhidi ya raiya.
  Nina imani asilimia 100 kuwa mafunzo wanayopata huko ccp yanawandisha ukatili dhidi ya raiya badala ya kuwafunza kuwa karibu na raiya kwa madhumuni ya kuwatumikia na kuwasaidia.
  Pia swala la malipo na makazi ya askari ya boreshwe, kwa sasa unakuta polisi anaipwa kiduchu na wapo wanaopewa posho elfu 10 kwa kulinda benki usiku kucha hili hali wanalinda mabilioni ya pesa yaliyopo ndani ya benki iyo.
  Mateso wanayopata askari hawa kuanzia kwenye mafunzo, kwenye malipo mpaka kwenye makazi duni yanawafanya askari wetu kuwa na roho ya kukata tamaa na kuamua kunyanyasa raiya kwa nia ya kupunguza maisha duni waliyonayo pamoja na kupunguza hasira walizonazo dhidi ya mfumo wa jeshi hili.
  Ni hayo tu.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 7. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #7
  Sep 6, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mbunge Stephen Kazi aliwahi kuongea bungeni kuhusu kulivunja Jeshi la Polisi enzi ya Mahita.
   
 8. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #8
  Sep 7, 2012
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Kwa upande wangu, ni idara za magereza na zimamoto ndio sijawahi shuhudia mauchafu yao. Idara zingine zote za wizara ya nchimbi- polisi wa aina zote pamoja na idara ya uhamiaji, zinatakiwa kufanyiwa mabadiliko makubwa.
   
 9. Vijisenti

  Vijisenti JF-Expert Member

  #9
  Sep 7, 2012
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 475
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Hizi hoja zinaweza kuwa nzuri lakini zinanitia mashaka,
  wakati wa Mh. Fulani tulishuhudia mauaji mengi zaidi
  kuanzia Mwembe Chai, zanzibar n.k tena kwa mara ya
  kwanza toka uhuru nchi yetu ilikuwa na wakimbizi Kenya na Somalia
  Hivi haya hamkuyaona?
   
Loading...