Hoja: Je! Mavazi ya Polisi wa Kike yanakidhi matakwa ya Waraka Na 3 wa Mavazi ya Watumishi wa Umma? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja: Je! Mavazi ya Polisi wa Kike yanakidhi matakwa ya Waraka Na 3 wa Mavazi ya Watumishi wa Umma?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Gumzo, Aug 18, 2012.

 1. G

  Gumzo JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CHANZO: GUMZO LA JIJI: Hoja: Je! Mavazi ya Polisi wa Kike yanakidhi matakwa ya Waraka Na 3 wa Mavazi ya Watumishi wa Umma?  Waraka wa Utumishi Na. 1 wa mwaka 1971 unaohusu mavazi ulitokana na mwongozo uliotolewa na Chama cha TANU kuhusu mavazi. Madhumuni ya waraka huo ilikuwa kuimarisha heshima ya Taifa kwa kuhakikisha kuwa watumishi wa Serikali wanavaa mavazi ya heshima wanapowahudumia wananchi. Waraka huo uliainisha baadhi ya mifano ya mavazi ambayo yalionekana hayafai na yale yanayofaa kwa wanawake na wanaume, utengenezaji wa nywele unaofaa na usiofaa na vipodozi visivyokubalika.


  Hali ilivyo sasa:


  2. Tangu waraka huo ulipotolewa kumekuwepo na mabadiliko makubwa ya mitindo ya mavazi, nywele na vipodozi. Mabadiliko ya mitindo ya mavazi ni jambo lisiloepukika. Hata hivyo baadhi ya mitindo hiyo ya mavazi inashusha heshima na hadhi ya utumishi wa umma kama itaendelea
  kuvaliwa na ni kinyume na kifungu cha 2 (e) cha kanuni za Maadili ya utendaji katika utumishi wa umma za mwaka 2005 Hata hivyo kumekuwepo na tatizo la kutokuwepo na tafsiri inayoeleweka juu ya mavazi gani ni ya heshima au yanayokubalika na yasiyokubalika mahali pa kazi.


  2
  Uamuzi wa Serikali:
  Tafsiri ya mavazi ya heshima hutegemea mila na desturi ya jamii husika. Katika utumishi wa umma mavazi ya heshima kwa mtumishi wa umma ni yale ambayo yanazingatia mila na desturi za taifa letu ambayo yanapovaliwa hayaonyeshi sehemu ya maungo ya mwili ambayo hayakuzoeleka kuachwa wazi, hayabani na ambayo hayana michoro au maandishi ya kudhalilisha wengine au yanayoonyesha ushabiki wa kitu fulani. Kwa hiyo waraka huu unatoa ufafanuzi kuhusu mavazi nadhifu yanayopaswa kuvaliwa kazini kwa kutoa mifano michache ya mavazi ambayo siyo ya heshima na ambayo hayakubaliki katika utumishi wa umma kwa jinsi zote mbili.


  Utekelezaji:
  3. Ufuatao ni ufafanuzi wa mavazi yasiyokubalika mahali pa kazi ambayo pia yameonyeshwa kwa picha kwenye kiambatisho A na B. Nguo kama “Jeans” na fulana zinaweza kuvaliwa na watumishi ambao wanalazimika kufanya kazi za nje ya ofisi.


  3.1 Kwa Wanawake
  (i) Baadhi ya mavazi yasiyofaa:
  • Nguo zinazobana,
  • Nguo fupi ambazo zinaacha magoti wazi.
  • Nguo ambazo zinaacha sehemu ya mwili wazi kama
  vile kitovu na kifua,
  • Nguo ambazo zina picha, michoro, na maandishi ambayo hayaendani na shughuli za serikali,
  • Kaptura aina yoyote ile kama vile pedo na pensi,
  • Nguo zinazoonyesha maungo ya mwili (transparent).
  • Suruali za “Jeans”,
  • Suruali yoyote iliyoachwa bila kupindwa,
  • Fulana – “T-Shirts” (Hizi zivaliwe tu wakati wa shughuli maalum inayotambulika),
  • Nguo ambazo ni za kazi maalum – michezo, kazi za nje au burudani. Hizi zivaliwe mahususi wakati wa utekelezaji wa shughuli hizo,
  • Nguo yenye maandishi ya chama chochote cha siasa au ushabiki wa kitu fulani,
  • Nguo yeyote inayopingana na maadili ya utumishi wa umma.
  (ii) Nywele zisizofaa:
  • Nywele chafu na ambazo hazikutengenezwa vizuri.
  (iv) Viatu visivyofaa
  • Kandambili,
  • Viatu vya michezo (isipokuwa wakati wa shughuli
  maalum za michezo),
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Aug 18, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,335
  Likes Received: 22,187
  Trophy Points: 280
  Ulitaka polisi wa kike wavae ma dera?
   
 3. Gwangambo

  Gwangambo JF-Expert Member

  #3
  Aug 18, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 3,655
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Lazima mtoa mada utakuwa mzinzi au muasherati.:shetani:
   
 4. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #4
  Aug 18, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Mkuu, ni kweli kabisa hawa askari wa kike wanatatanisha sana katika uvaaji wao. Maana sketi wanazovaa ni fupi na zinawabana, i mean zinakuwa juu ya magoti. Wakivaa suruali ndo kabisaaa, utata mtupu.
   
 5. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #5
  Aug 18, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,407
  Trophy Points: 280
  mtoa mada umechemka. Sioni tatizo la mavazi ya askari wa kike. Nahisi una yako.
   
 6. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #6
  Aug 18, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Wanavaa visketi vifupi juu ya magoti,Mapaja yote nje,Kwa kweli ni kero na inaleta picha mbaya sana kwa jamii hasa watoto.
   
 7. Biohazard

  Biohazard JF-Expert Member

  #7
  Aug 18, 2012
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 2,002
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  [​IMG]

  Hiyo kiboko
   
 8. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #8
  Aug 18, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,272
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo ulitaka wavaeni Max??mbona yapo sawa au wewe ni uhamusho??kaa kwenu huko zanzibar
   
 9. peri

  peri JF-Expert Member

  #9
  Aug 18, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  kuna haja ya polisi wa kike kukumbushwa juu ya hii sheria, wanavaa nusu uchi.
  Nb:
  kuna watu wa ajabu ambao wameathirika na mila za kigeni ndo wanaotetea haya mavazi.
  Wakumbuke hizo co mila za tanzania, ni kinyume na maadili yetu.
   
 10. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #10
  Aug 18, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  hivi ikitokea kurukushani barabarani na hivi vimini itakuwaje?
   
 11. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #11
  Aug 18, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,700
  Trophy Points: 280
  Pia ni extremist wa deen fulani
   
 12. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #12
  Aug 18, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,223
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Halafu siku hizi vibinti vidogo kweli ndiyo vimejaa mtaani vimetoka CCP,yaani na yale mavazi yao badala ya kuogopwa na jamii wamekuwa wanashawishi. Hebu Mwema aliangalie hili upya aisee .
   
 13. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #13
  Aug 18, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,110
  Trophy Points: 280
  mkuu, kwanza askari si mtumishi wa umma, ni mtumishi wa jeshi ndio maana ajira zao huwa ni za mikataba mitatu mitatu, akifikisha mikataba 4, sawa na miaka 12, ndo anaanza utumishi wa umma.
   
 14. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #14
  Aug 18, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  acha tamaa polisi hujui wake zetu wengine ni polisi ntakuua wewe!
   
 15. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #15
  Aug 18, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,109
  Likes Received: 1,499
  Trophy Points: 280
  Ni kweli tuna tatizo la mavazi kwa watumishi wa umma lakini pia kuna mtindo wa viongozi wetu au watumishi wetu kuvaa nguo zinazoashiria dini fulani kumbuka serikali haina dini lakini watu wake wana dini sasa haya mavazi yanawafanya watu wengine wenye dini tofauti kukosa amani na wakati mwingine kujenga hisia yanapotolewa maamuzi fulani yametolewa kwa hisia za dini hili litazamwe kwa undani
   
 16. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #16
  Aug 18, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  mbona mabosi wanawake wanakuja na mapaja nje? Ni afadhali polisi ile nguo analetewa achague inayomtosha kuliko wanawake wa siku hizi wanaoenda kupima nguo kwa mafundi na kutujia ofisini mapaja nje! Siku hizi wameacha kuonesha matiti wamehamia kwenye mapaja. Pumbaf wanawake except my my mom na wale wote wanaojiheshimu!
   
 17. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #17
  Aug 18, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Hii ni chakula ya Kova !!!!!!!!!!!!!!! Hawezi kukemea!!!!!!!!!!!!
  Polisi Wengi wa kike wameingizwa katika kazi hiyo baada ya kufanya ngono na vyeo vyao huwa vinapanda harakaharaka kwa misingi hiyohoyo ya ngono , wamepewa kazi za utafriki kwa ngono hiyohiyo sasa wao wenyewe juzi wamehiza matumizi ya kondomu badala ya kuhimiza mavazi bora
   
 18. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #18
  Aug 18, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  ngoja tusubiri kuvaliwa vimini
  553557_456892804327352_100000199094899_2005964_392781373_n.jpg
   
 19. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #19
  Aug 18, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Ha ha ha ha. Hayo yalikuwa mawazo yangu mkuu. Tunajitahidi kuzuia hizo tamaa ila wanatutamanisha. Dont kill me please
   
 20. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #20
  Aug 18, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Duu afadhali mkuu, nilishaanza kuingiwa na wivu bwana, kumwambia abadili nguo avae ndefu siwezi.
  Any way hayo mambo yapo kila sehemu bwana tujitahidi kuzuia tamaa zetu!
   
Loading...