Hoja Inapokuwa Vioja

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,201
219
Kwa kawaida mimi napenda kutembelea baadhi ya marafiki ambao ninashirikiana nao kwa njia mbali mbali katika suala zima la kuandaa habari , kuhabarisha , kutafiti na kufanya shuguli zingine ambazo zinahusiana na uhabarishaji na upashaji wa habari .

Jana ilikuwa ni tofauti sana kuliko siku nyingi ambazo nimewahi kuwa katika fani hii kidogo , nilienda kumsalimia mmoja wa rafiki zangu hawa kwanza nikaambiwa hayupo amesafiri baada ya muda nikaambiwa nimsubiri .

Alikuja huko amenuna sana , mimi nikawa nacheka tu nikaanza kumtania jinsi anavyonuna kumbe alikuwa hana matani bwana amekasirika sana , akanikumbushia utani mmoja ambao niliwahi kumtania katika jukwaa moja la mtandao kwamba umemuudhi sana – lakini nikamwambia kule katika majukwaa tunatumia majina bandia usikasirike hakuelewa

Tukaachana na hayo , suala muhimu nililomfuatia rafiki yangu huyu ni kumuuliza mambo kadhaa ambayo nimeulizwa labda kwa njia ya barua pepe kwa njia ya simu na njia zingine za mazungumzo ya kawaida anieleweshe yeye anajua nini .

Akaanza kunipa simulizi moja iliyonivunja mbavu ni ile ya watu kusema kwamba mimi ni usalama wa taifa , ninashirikiana na usalama wa taifa kwa karibu sana pia nina husika katika kukamatwa kwa wale vijana 2 wa Jukwaa la Jambo – nikamuuliza sasa nani huyo aliyesema

Kwa maelezo yake anasema ni kijana mmoja wa huko huko jambo amesema nimepewa Milioni 5 na Usalama wa Taifa ili nionyeshe yule kijana yuko wapi kutokana na ujuzi wangu katika masuala ya mtandao na mawasiliano usalama wa taifa wananitumia sana hata kwa shuguli zingine .

Nikamsimamisha nikamwambia hivi hao vijana wanaosema hivyo wanajua kwamba mimi ndio nilikuwa mtu wa kwanza kufika wizara ya mambo ya ndani kuulizia kadhia hiyo ? nilifika pale na kutoa taarifa hiyo kwa njia ya sms kwenda kwa jamaa wengine ndio wao wakaanza kuja na kutoa taarifa kwingine ?

Je wana ushahidi wowote wa malipo hayo ya milioni 5 niliyopewa na usalama wa taifa ? je wana ushahidi mwingine wowote wa kuonyesha mimi ni usalama wa taifa au nimewahi kushirikiana nao kwa njia nyingine yoyote ile ? hata kama ni usalama wa taifa je nani alinipa jukumu la kufanya shuguli hiyo ? wanaweza kumtaja ?

Nilisikitika sana nilipoambiwa habai hii , watu wanaosambaza taarifa hizi ni watu ambao nimewahi kufanya nao kazi kwa karibu na wengine tunaendelea kufanya kazi kwa karibu mpaka sasa hivi na sijapenda kuingia katika mzozo na watu hawa

Ni rafiki zangu naheshimu urafiki wetu na ushirikiano wetu mwingine tuliojijengea tokea wakati huo tunajuana kwa mara ya kwanza nimesikia hiyo na nimeelewa kwa mara nyingine tena nimewasamehe kwa kutoa taarifa za uwongone na uzushi kwa watu wengine .

Ninaheshimu sana uhuru wa watu au mtu kutoa maoni yake popote pale alipo lakini yule ambaye anatoa maoni yake au taarifa yake bila kuwa na nyaraka za kuyatetea yale ambayo ameandika au kusema basi ajue atakua amekosea sana na kujivunjia heshima yake .

Haya ma jukwaa ya mtandao yanajengwa na watu , watu wenyewe ndio sisi kwahiyo tujaribu kuheshimiana ili kujenga jamii iliyo bora na makini zaidi sasa na hata siku zijazo .

……………………………………………………………………………..

Niliposikia habari hizi kwa mara ya kwanza nilikuwa na mawazo ya kwenda pale pale wizara ya mambo ya ndani ambapo suala hili liliendelea , nilikuwa na uwezo wa kwenda kuomba nyaraka za maelezo ambayo vijana hawa waliyatoa wakati wanahojiwa .

Adhari zake ni kubwa sana kwa sababu hawa vijana pamoja na mzazi wa vijana hawa wamedanganya kwahiyo ingeweza kutokea watu kuombwa kutoa taarifa zingine za baadhi ya wanachama wa majukwaa haya viwekwe hadharani na hiyo itakuwa mwanzo wa kuvunja majukwaa haya sipendi mambo hayo yatokee .

……………………………………………………………………………….

Ndugu Max Mello , Mike Mushi na William Mushi popote mlipo mkipata ujumbe huu napenda kuwaambia kwamba nimewasamehe kwa yote ambayo mumesema na kusambaza , mimi siko tayari kuingia katika mabishano haya wakati ukweli unajulikana kuhusu suala lenu

Na kama mnataka hili suala liendelee au niendeleze mbali zaidi nina uwezo wa kufanya hivyo nina mashahidi ya watu ambao taarifa hizi mliwapelekea kwa njia moja au nyingine kuwaambia kwamba mimi ni usalama wa taifa , nimelipwa milioni 5 na usalama wa taifa ili kutoa taarifa za maeneo yenu .

Kwa bahati mbaya nyie sio ma expert wa mambo ya mtandao mngekuwa angalau na utaalamu wa mambo haya basi kumkamata mtu au kujua sehemu ya mtu kutokana na tabia zake za mtandao ni rahisi sana kuliko hata hivyo munavyofikiria ni kitu cha dakika kadhaa kama mtu unatumia majina zaidi ya 4 katika jukwaa moja na katika post zingine unaweka namba zako za simu na sehemu ulipo kwa nini usijulikane ulipo ?
Ina maana usalama wa taifa au watu wote wanaohusika na usalama wa raia ni wajinga kiasi kwamba hawawezi kutambua hivi vitu ? kwanini wamepewa idara zile kwanini serikali inatumia mamilioni kupeleka vijana shule wakasome zaidi mambo haya ?

Ndugu Mike , wewe ni kijana mdogo sasa hivi nakumbuka mara ya mwisho nilivyokuja arusha tulivyoongea na niliona changamoto ulizonazo maishani mwako nakusihi uendeleze juhudi katika masomo yako na mambo yako mengine yanayoweza kujenga maisha bora kwako na kwa wadogo zako , inawezekana wengi unaoshirikiana nao au kuwasikiliza au kutegemea wako wameshasoma wana taaluma na ujuzi wao wale popote wanaweza kufanya kazi katika dunia hii , lakini wewe huwezi kufanya kazi popote dunia hii umri wako bado kufika huna sifa hizo kwahiyo endeleza juhudi za kujitafutia elimu bora ili ujenge maisha bora mbeleni wachana na porojo mdogo wangu , ninakujua binafsi ndio maana nakuambia hivi usijifananishe na watu hata sikumoja .

Ndugu William Mushi ambaye ni baba Yake Mike , nashukuru kwa yale yote uliyoyasema bila kuwa na ushahidi wowote ule , kumbuka unavyodanganya ummah una muharibia sifa mtoto wako na hata wale wote ambao wanafanya nae kazi pamoja au wale ambao wanapenda siku moja kuja kushirikiana nae , kwanini usimwandalie mtoto wako elimu bora na maisha bora kuliko kumpeleka sehemu ambayo sio ? nina mdogo wangu mooja anaitwa David ana umri wa miaka 16 ni mmoja wa maprograma wazuri sana ambao sijapata kuona katika Tanzania na mwingine anaitwa ford ana miaka 17 yeye anaishi uingereza nae ni kijana shupavu sana katika masuala ya mawasiliano na habari hawa wote muda wao wa kujitokeza bado bado tunawapeleka shule na kuwapa changamoto zingine za maisha waje kuwa bora zaidi miaka michache ijao – ndugu William iga mfano huo mchache tu kujenga maisha ya watoto wako waje kuleta neema kwa taifa .

Ndugu Max sina chochote cha kusema lakini nakusihi uendelee vizuri na masomo yako hapo DIT uje kuleta changamoto katika suala zima la ujenzi na miundo mbinu kwasababu hiyo ndio fani yako wacha kabisa hizi longo longo za mitaani najua wewe ni mtu mzima sasa kwahiyo take care of ur self .

Naomba kuishia hapa ninatangaza kuwasamehe kwa yote hayo mliyoyasema na kuyafanya , mimi sina adui dunia hii na sintokaa kuwa na adui na sifikirii kuwa na uadui na mtu wowote au kikundi chochote kile cha jamii .

Mimi ni mtu makini nimelelewa katika mazingira ya familia makini iliyokuwa inajua nini inataka kutoka kwa mtoto wao ,nitaendeleza umakini huo huo katika kuendeleza itikadi za umakini wetu toka katika ngazi ya familia , mitaani na popote pale ninapo kanyaga .

Ahsante

Yona F Maro
 
Kwa kawaida mimi napenda kutembelea baadhi ya marafiki ambao ninashirikiana nao kwa njia mbali mbali katika suala zima la kuandaa habari , kuhabarisha , kutafiti na kufanya shuguli zingine ambazo zinahusiana na uhabarishaji na upashaji wa habari

si Tuambie Ulimtembele nani,Mambo ya Story kama Habari za Magazeti ya Bongo Tumechoka!!

na hayo , suala muhimu nililomfuatia rafiki yangu huyu ni kumuuliza mambo kadhaa ambayo nimeulizwa labda kwa njia ya barua pepe kwa njia ya simu na njia zingine za mazungumzo ya kawaida anieleweshe yeye anajua nini

ina maana uliyemfuata anajua sana kuhusu hii habari ya wewe kuwa Uaslama,na haukwenda kumsalimia kama ulivyosema Mwanzo bali kwenda kumuuliza mambo ya uchochezi/udaku uliyosikia huku tulishayamaliza!1

Kwa maelezo yake anasema ni kijana mmoja wa huko huko jambo amesema nimepewa Milioni 5 na Usalama wa Taifa ili nionyeshe yule kijana yuko wapi kutokana na ujuzi wangu katika masuala ya mtandao na mawasiliano usalama wa taifa wananitumia sana hata kwa shuguli zingine .

Kila Mtu akiwa Jambo Forums anaambiwa Usalama,Hata mie nilishawahi kuambiwa hivyo kwamba ni mtu wa Usalam,ila kuwa usalama na kutokuwa usalama ni jambo la Mtu Binafsi na kuchagua kutumika wapi.Hivyo alina msingi na ungelipuuza tu kama kweli wewe sio mtu wa Pale.

Je wana ushahidi wowote wa malipo hayo ya milioni 5 niliyopewa na usalama wa taifa ? je wana ushahidi mwingine wowote wa kuonyesha mimi ni usalama wa taifa au nimewahi kushirikiana nao kwa njia nyingine yoyote ile ? hata kama ni usalama wa taifa je nani alinipa jukumu la kufanya shuguli hiyo ? wanaweza kumtaja ?
Hayo ni maswali magumu sana kujibiwa sababu mambo ya Usalama wa Taifa yanafanywa kwa usiri Mkubwa sana na inawezekan ukawa Mtu wa usalama na bila mtu kujua labda kw auhakika wa majibu yako basi Kamuulize Othman Rashid..na kwa ufafanuzi zaidi

kwa ibara ya Pili ya sheria ya TISS
(2) Subject to this Act, the Director-General may, on behalf of the
Government of. the United Republic or of the Revolutionary Government
of Zanzibar-
(a) employ under written agreements, such officers of intelligence
and security as he thinks necessary;
(b) engage such other employees as he thinks necessary,
for the purposes of this Act.
(3) Every person referred to in subsection (1) shall, upon the commencement
of this Act, continue to have employment benefits equivalent
to that he had immediately before the commencement of this Act, until
such time as those benefits are modified by the Service according to law.
Niliposikia habari hizi kwa mara ya kwanza nilikuwa na mawazo ya kwenda pale pale wizara ya mambo ya ndani ambapo suala hili liliendelea , nilikuwa na uwezo wa kwenda kuomba nyaraka za maelezo ambayo vijana hawa waliyatoa wakati wanahojiwa .

Adhari zake ni kubwa sana kwa sababu hawa vijana pamoja na mzazi wa vijana hawa wamedanganya kwahiyo ingeweza kutokea watu kuombwa kutoa taarifa zingine za baadhi ya wanachama wa majukwaa haya viwekwe hadharani na hiyo itakuwa mwanzo wa kuvunja majukwaa haya sipendi mambo hayo yatokee .

……………………………………………………………………………….

Kwa bahati mbaya nyie sio ma expert wa mambo ya mtandao mngekuwa angalau na utaalamu wa mambo haya basi kumkamata mtu au kujua sehemu ya mtu kutokana na tabia zake za mtandao ni rahisi sana kuliko hata hivyo munavyofikiria ni kitu cha dakika kadhaa kama mtu unatumia majina zaidi ya 4 katika jukwaa moja na katika post zingine unaweka namba zako za simu na sehemu ulipo kwa nini usijulikane ulipo ?
Ina maana usalama wa taifa au watu wote wanaohusika na usalama wa raia ni wajinga kiasi kwamba hawawezi kutambua hivi vitu ? kwanini wamepewa idara zile kwanini serikali inatumia mamilioni kupeleka vijana shule wakasome zaidi mambo haya ?
Suala la kuwa Expert sio hoja ni kioja katika jambo hili,Kila mtu anaweza kuwa specialist katika Area yake,na nina amaini hawa vijana ni wakli katika baaadhi ya mambo ila sio kote,il shy heshimu hata hicho kidogo wanachokifahamu..hii ni Tanzania na wala sio Uk au ughaibuni ambapo mtu akizaliwa na kukua anajua kila kitu na mfumo wa Elimu yetu hamjengi mtu kwa hivyo.!

Ndugu Mike , wewe ni kijana mdogo sasa hivi nakumbuka mara ya mwisho nilivyokuja arusha tulivyoongea na niliona changamoto ulizonazo maishani mwako nakusihi uendeleze juhudi katika masomo yako na mambo yako mengine yanayoweza kujenga maisha bora kwako na kwa wadogo zako , inawezekana wengi unaoshirikiana nao au kuwasikiliza au kutegemea wako wameshasoma wana taaluma na ujuzi wao wale popote wanaweza kufanya kazi katika dunia hii , lakini wewe huwezi kufanya kazi popote dunia hii umri wako bado kufika huna sifa hizo kwahiyo endeleza juhudi za kujitafutia elimu bora ili ujenge maisha bora mbeleni wachana na porojo mdogo wangu , ninakujua binafsi ndio maana nakuambia hivi usijifananishe na watu hata sikumoja .
Shy,Acha tabia ya Kibri sababu ni tabia ya Mwenyezi Mungu na usidhani udogo wa mtu ndio udogowa busara aliyonayo.!

Naomba kuishia hapa ninatangaza kuwasamehe kwa yote hayo mliyoyasema na kuyafanya , mimi sina adui dunia hii na sintokaa kuwa na adui na sifikirii kuwa na uadui na mtu wowote au kikundi chochote kile cha jamii .
Hii ni jambo amblo lilitakiwa kubeba ujumbe wote uliouandika na sio story uliyoileta,yalishaisha na tuendeleze libeneke.
 
Back
Top Bottom