Hoja hii ya Mbunge wa Simanjiro imeishia wapi?

Azipa

JF-Expert Member
Mar 19, 2012
1,069
322
MMOJA AJITOLEA KUFUKUZWA,
WATAKA IUNDWE TUME
KUICHUNGUZA HAZINA
Neville Meena na Mussa Juma,
Dodoma
KAMATI ya wabunge wa CCM
jana ilikutana kwa zaidi ya saa
tano katika kikao ambacho
wabunge hao waliibua hoja ya
kutaka kuchunguzwa kwa Mfuko
Mkuu wa Serikali kwa maelezo
kwamba kuna dalili za kuwapo
kwa ufisadi.Habari kutoka ndani
ya mkutano huo ulioongozwa na
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
zilisema msingi wa hoja hiyo
iliyotolewa na Mbunge wa
Simanjiro, Christopher Ole
Sendeka ni kutokuwapo kwa
uwiano kati ya fedha
zilizokusanywa na Mamlaka ya
Mapato (TRA) pia kutoka kwa
wahisani, na zile zilizopelekwa
katika wizara na Idara za
Serikali.
Katika hoja hiyo ambayo
iliripotiwa kwamba iliungwa mkono
na wabunge wengine kadhaa, Ole
Sendeka alipendekeza iundwe
Kamati Teule ya Bunge
kuchunguza mfuko huo au
iteuliwe Kampuni ya Kimataifa
ya Ukaguzi wa Hesabu kufanya
ukaguzi.
“Tumeshindwa kuelewa inakuwaje
TRA inakusanya mapato asilimia
106, yaani zaidi ya asilimia 100,
wahisani tunaambiwa wametoa
fedha asilimia 80,halafu eti
fedha za maendeleo
zilizopelekekwa wizarani ni
asilimia 22 tu, haiwezekani na
hapa tunataka uchunguzi
ufanyike,”alisema mmoja wa
wabunge wa CCM.
Mbunge mwingijne alisema
wamebaini kwamba taarifa ya
Waziri wa Fedha kuhusu fedha
zilizotolewa kwa mujibu wa bajeti
ya 2011/2012 zinatofautina na
uhalisia katika wizara ya idara za
Serikali na kwamba hiyo ni dalili
kwamba hizo ni dalili ya kuwapo
kwa matundu kwenye hazina hiyo
ya nchi yanayopaswa kuzibwa.
“Tumesema haiwezekani,
tunahitaji kutekeleza Ilaani ya
CCM na ahadi ambazo sisi
wabunge, Rais na chama tulizitoa
kwa wananchi, sasa kama
tunapitisha bajeti, fedha
zinakusanywa, lakini hazifiki kwa
wananchi ndiyo tunafanya kazi
gani? Hili tunasema
haliwezekani,”alisema mbunge
mwingine baada ya kikao hicho
jana jioni.
Habari zaidi kutoka ndani ya
kikao hicho kilichoanza saa 5.30
asubuhi katika Ukumbi wa Pius
Msekwa na kumalizika saa 11.30
jioni ziliwataja baadhi ya
wabunge waliounga hoja mkono
hoja hiyo kuwa ni Alphaxard
Lugora (Mwibara), Godfrey
Zambi (Mbozi Magharibi) na
Livingstone Lusinde (Mtera).
Bajeti 2012/2013
Kuhusu Bajeti ya 2012/2013,
wabunge hao wa chama tawala
wanaelezwa kwamba waliigeukia
Serikali wakieleza kutoridhishwa
na bajeti iliyowasilishwa bungeni
juzi jioni na Waziri wa Fedha, Dk
William Mgimwa.
Miongoni mwa malalamiko
makubwa ya wabunge ni hao ni
kutozingatiwa kwa vipaumbele
vya Taifa pia Mpango wa wa
Maendeleo wa Miaka Mitano
2011 - 2016 ambao ulipitishwa
na Bunge mwaka jana.
“Wewe bwana wewe, sijui
nikwambie nini, lakini wabunge
tumesema tumechoka, maana
hakuna mabadiliko kwenye bajeti,
tunayaona mambo mengi kuwa ni
danganya toto tu, tumejadili,
lakini sijui kama kipo cha
kubadilika,”alisema mmoja wa
wabunge waliohudhuria kikao
hicho.
Habari zaidi zilidokeza kuwa
Waziri Mkuu Pinda alilazimika
kutoa nafasi kwa kila mbunge
aliyeomba nafasi ya kuzungumza
ili kupunguza hasira ambazo
zingeweza kujitokeza kwenye
mjadala wa jumla keshokutwa.
“Ndiyo maana tumechukua
masaa, Pinda ameamua kuwapa
watu wote nafasi ili wazungumze,
ila mimi nimetoka wala
sikuchangia kitu nasubiri huko
ndani Jumatatu au Jumanne
nikipata nafasi,”alisema Mbunge
mwingine.
Mbunge wa Viti Maalum, Sara
Msafiri aliripotiwa akipinga
ushuru kwenye muda wa
maongezi ya simu na kutaka
Serikali kuhakiki kwanza mapato
ya kampuni za simu.
Kadhalika mbunge huyo
alinukuliwa ndani ya kikao hicho
akisema bajeti hiyo imejaa
maslahi ya wakubwa tu, na
kwamba lazima yafanywe
marekebisho ambayo yataifanya
ishuke chini kwa wananchi.
Mwingine ni Naibu Waziri wa
Sayansi, Mawasiliano na
Teknolojia, January Makamba
ambaye alinukuliwa akiishauri
Serikali iwe wazi kuhusu msamaha
wa Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) kwenye vifaa vya gesi
kwani mwanya huo unaweza
kutumiwa vibaya kukwepa kodi.
Kadhalika Makamba alinukuliwa
akitaka kubadilishwa kwa
taratibu za kutoza kodi kampuni
za mafuta kwa kuweka utaratibu
wa kodi kulipwa baada ya biadhaa
hiyo kuingizwa nchini badala ya
siku 45 za sasa.
“Kwanini tuwape hawa
wafanyabiashara mitaji
kwasababu utaratibu wa sasa
wanaingiza mafuta hata kama
hawana senti tano, na sisi
tunakubali kuahirisha kuchukua
kodi hadi baada ya siku 15 na
baadaye siku 30. Hili ni tatizo na
tuangalie eneo hili vizuri,”chanzo
chetu kilimnukuu Makamba
akisema katika kikao hicho.
Kutokana na hoja za wabunge
hao, Kikao hicho kiliazimia
kuundwa kwa kamati ndogo ya
wabunge wa CCM kuangalia jinsi
ya kupanua wingo wa kukusanya
mapato pia kupendekeza
mgawanyo wa mapato hayo
tofauti na Bajeti ya Serikali.
Baada ya kikao hicho, Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Fedha na
Uchumi aliwaongoza wajumbe wa
kamati yake kwenda kukutana
tena na Waziri wa Fedha ili
kuangaliwa kama wanaweza
kufanya marekebisho ya bajeti
hiyo kwa kuzingatia maoni ya
wabunge wa CCM.
Mpina apinga hadharani
Wakati hayo yakiripotiwa kutokea
ndani ya kikao cha wabunge wa
CCM, Mbunge wa Kisesa, Luhaga
Mpina jana alijitokeza mbele ya
waandishi wa habari mjini
Dodoma na kusema kwamba
hataunga mkono bajeti hiyo na
kwa maana hiyo “yupo tayari
kufukuzwa” kutokana na uamuzi
wake huo.
Licha ya kutangaza kutoiunga
mkono bajeti hiyo, mbunge huyo
alisema keshokutwa Jumatatu
ataomba mwongozo kwa Spika
kutoa hoja ya kuomba bajeti hiyo
irejeshwe serikalini ili ifanyiwe
marekebisho na kama Serikali
ikiing’ang’ania ni bora Rais
Jakaya Kikwete avunje Bunge na
kurejewa uchaguzi.
Hata hivyo, alisema anaamini
kwamba hatua ya kuvunja Bunge
haiwezi kufikiwa ikiwa busara
itatumika kumaliza mvutano
uliopo.
Mpina alisema Bajeti ya Serikali
inakiuka azimio la Bunge la
kutengwa fedha walau asilimia
35 kwa ajili ya miradi ya
maendeleo.
Mbunge huyo ambaye ni Mjumbe
wa Kamati ya Bunge ya Fedha na
Uchumi alisema yapo makubaliano
ya wabunge kwamba kila mwaka
wa fedha, zitatengwa Sh2.7
trilioni kutoka fedha za ndani
kugharamia miradi ya maendeleo
ili kuwezesha fedha hizo kufikia
walau asilimia 35 ya bajeti.
Alisema kwa mshangao bajeti
iliyowasilishwa juzi iliweka kando
mapendekezo na maazimio ya
wabunge.
“Bajeti hii, tuliikataa katika
kamati yetu, kwa kuwa inakiuka
Azimio la Bunge na pia mpango
wa serikali wa miaka mitano, na
juzi iliposomwa niliomba Mwongozo
wa Spika ili niitake Serikali
irudishe bajeti hii na
kurekebisha, lakini bila kufuata
kanuni spika alinizuia kwa madai
kuwa siku ya kusomwa bajeti
hakuna mwongozo” alisema Mpina.
Mpina alisema, kanuni ya bunge
ya 68 kifungu cha 7, inaeleza
wazi kuwa mbunge, anaweza
kusimamia wakati wowote
anapoona hakuna mtu
anayeongea.
“Naamini Spika hakunitendea haki
na Jumatatu pia nitaomba
mwongozo tusiendelee na mjadala
wa bajeti hii na kama itaonekana
kutetea fedha kupelekwa kwenye
maendeleo ni kosa hasa wakati ni
utekelezaji wa ilani ya CCM, nipo
tayari kwa lolote,”alisisitiza.
Alisema kitendo cha Serikali
kutenga Sh 2.2 trilioni badala ya
Sh2.7 trilioni ambao ni upungufu
wa Sh500 bilioni, kumesababisha
miradi mingi kutengewa fedha
kidogo na mingine kukosa fedha
kabisa.
Alisema kibaya zaidi mapato ya
ndani yameongezeka kwa kiasi
cha Sh1.5 trilioni, lakini fedha
hizo zimeliwa na matumizi ya
kawaida ambayo yameongezeka
kwa Sh1.9 trilioni, huku fedha za
maendeleo zikipungua kwa
Sh397.8 bilioni ikilinganishwa na
mwaka 2011/12.
Mpina alisema kwa muda mrefu
Serikali imekuwa ikiahidi
kupunguza matumizi ya kawaida
ili kuongeza kasi ya utoaji
huduma na uwekezaji katika
sekta zinazokuza uchumi na
kupunguza umasikini, lakini
hakuna kinachotekelezwa.
“Matumizi kama haya ya safari,
posho,mafuta,ununuzi wa magari ,
samani, mawasiliano,
sherehe,warsha ,makongamano,mafunzo,nje
ya nchi yanaweza
kuepukika,kupounguza au
kuahirishwa”alisema Mpina.
Mbunge huyo alihoji inakuwaje
serikali ilipata fedha za kufidia
mabenki na wafanyabiashara
walioathirika na mtikisiko wa
uchumi Sh1.7 trilioni halafu
ishindwe kupata Sh500 bilioni
kugharamia miradi iliyoainishwa
katika mpango wa maendeleo.
Saturday at 2:43pm
 
Back
Top Bottom