Hoja: Halmashauri zote nchini zifutwe

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
17,871
33,236
Kama kuna ufujaji wa fedha ambao wananchi wa Tanzani wanabebeshwa basi ni kuwepo kwa Halmashauri za miji Tanzania. Hivi umuhimu wa kuwepo kwa Halmashauri hizi ni upi kama hazikusanyi kodi, zikifanya baadhi ya maamuzi yake yanaweza kutenguliwa na Waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa? Hazimiliki Ardhi, zinaweza kugawanywa wakati wowote bila ya kushauriana nao na Halamshauri hizi zinaendeshwa na wakurugenzi ambao wenye Halmashauri zao hawana sauti ya kuwaajiri ama kuwafukuza kazi.

Ni kitu gani kitapungua kama hizi Halmashauri hazitokuwepo kuliko hivi sasa hata ushuru kidogo wanaokusanya unaishia kuwalipa madiwani ambao ni kama simba wa karatasi kwani kila waliamualo likiwaudhi wenye nchi yao linabatilishwa? Kwa nini tusiache nchi ziongozwe na Wakuu wa wilaya na mikoa?
 
Kwa sasa Halmashauri karibu zote ziko taabani. Hakuna fedha inayoshushwa kwa ajili ya miradi,other charges. Inafikia wakati hata hela ya kununua rimu moja ya karatasi wanakosa. Kwa kweli Serikali Kuu iwashushie fedha zao kama zilivyopangwa na kuidhinishwa kwenye bajeti.
 
Mfano halmashauri ya kakonko ni kati ya halmashauri lofa ya mwisho kabisa wakijikuna wanatoka unga sasa na usawa huu wa kupayuka number sijui inakuaje kwa kweli.
 
Yohana Kilimba hizi Halmashauri ukichunguza kwa kina ni kama picha tu. Kila kitu kinaamuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania. Ndiyo maana wakati madiwani wanataka kukaa kikao chao kule Arusha Mkuu wa mkoa akawaita Mkurugenzi na wakuu wote wa Idara na wakaenda kwake badala ya kuhudhuria kikao cha "Full council" ya Arusha Manispaa.
 
Naunga mkono hoja .hakuna sababu za kuwa na halmashauri kama hazina Uhuru wa kujiamulia mambo yao. Siku zote halmashauri zimekuwa ni mihanga wa maamuzi kutoka serikali kuu.
Zifutwe tu hakuna namna
 
Ili mupate sifa ukawa au? Halmashauri zikiachwa huru zile za ukawa zitaendelea Sana, 2020 "mutatuangusha urais maana nchi nzima itawaamini nyie,
 
Mnyirani hoja hapa siyo UKAWA kupewa sifa, bali sheria haizipi hizo Halmashauri uhuru. Kuna sheria inampa Waziri nguvu ya kuteua madiwani kuingia kwenye Halmashauri yoyote nchini. Uhuru wa Halmashauri za miji haupo na hakuna sababu ya zenyewe kuwepo!!
 
Mbona vitu Vinci hufanyiwa majaribio tufanyie hilo nalo
Hapa hakuna majaribio bali ni kitu halisi. Wewe kati ya wakuu wa wilaya na mikoa na Mameya na wenyeweviti wa halmashauri nani anamiliki serikali. Yaani Wakuu wa wilaya na mikoa ndiyo wanamiliki ardhi na dola hivo kama hawakubaliani na Halmashauri hutumia Polisi kufanikisha mambo yao.
 
Janga la Taifa ili kuzikomoa Halmashauri ambazo ziko chini ya CHADEMA akaamua kukwapua vyanzo vyote vya mapato vya halmshauri nchini na kuviingiza Serikali kuu, sasa zinakufa taratibu.

Kama kuna ufujaji wa fedha ambao wananchi wa Tanzani wanabebeshwa basi ni kuwepo kwa Halmashauri za miji Tanzania. Hivi umuhimu wa kuwepo kwa Halmashauri hizi ni upi kama hazikusanyi kodi, zikifanya baadhi ya maamuzi yake yanaweza kutenguliwa na Waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa? Hazimiliki Ardhi, zinaweza kugawanywa wakati wowote bila ya kushauriana nao na Halamshauri hizi zinaendeshwa na wakurugenzi ambao wenye Halmashauri zao hawana sauti ya kuwaajiri ama kuwafukuza kazi.

Ni kitu gani kitapungua kama hizi Halmashauri hazitokuwepo kuliko hivi sasa hata ushuru kidogo wanaokusanya unaishia kuwalipa madiwani ambao ni kama simba wa karatasi kwani kila waliamualo likiwaudhi wenye nchi yao linabatilishwa? Kwa nini tusiache nchi ziongozwe na Wakuu wa wilaya na mikoa?
 
Kama kuna ufujaji wa fedha ambao wananchi wa Tanzani wanabebeshwa basi ni kuwepo kwa Halmashauri za miji Tanzania. Hivi umuhimu wa kuwepo kwa Halmashauri hizi ni upi kama hazikusanyi kodi, zikifanya baadhi ya maamuzi yake yanaweza kutenguliwa na Waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa? Hazimiliki Ardhi, zinaweza kugawanywa wakati wowote bila ya kushauriana nao na Halamshauri hizi zinaendeshwa na wakurugenzi ambao wenye Halmashauri zao hawana sauti ya kuwaajiri ama kuwafukuza kazi.

Ni kitu gani kitapungua kama hizi Halmashauri hazitokuwepo kuliko hivi sasa hata ushuru kidogo wanaokusanya unaishia kuwalipa madiwani ambao ni kama simba wa karatasi kwani kila waliamualo likiwaudhi wenye nchi yao linabatilishwa? Kwa nini tusiache nchi ziongozwe na Wakuu wa wilaya na mikoa?

Jana Mlileta mada hapa kuwa Halmshauri zote zenye Madiwan wengi wa Chadema zitaongozwa kwa Ilani ya Chadema tukawakosoa kuwa hizo ni ndoto za alinacha mkabisha kwa Maneno ya Kejeli lakin baada ya kutuliza akili mmekiri kwa njia tofauti kidogo
 
Janga la Taifa ili kuzikomoa Halmashauri ambazo ziko chini ya CHADEMA akaamua kukwapua vyanzo vyote vya mapato vya halmshauri nchini na kuviingiza Serikali kuu, sasa zinakufa taratibu.
Ni kama mtu anayekuja kwako kukusaidia kuu nyoka kwenye kabati lako, anavunja vyombo vyote pamoja na vioo vyote vya kabati, lakini mwisho wa siku anakwambia kuwa "lakini nyoka si nimemuua?" hasara aliyokusababishia inalingana na kuua nyoka na jee kulikuwa hakuna njia nzuri zaidi ya kuua huyo nyoka bila ya kukutia hasara?

Wazifute tu hizo halmashauri hazina faida wala tija!!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Pohamba tafuta bandiko la mimi kuchangia mada hiyo. Nimeiunga mkono CHADEMA tangu mwaka 2005 kwa kuwa walikuja na sera ya Majimbo. Iwe ni UKAWA ama CCM kama mfumo wa kuziendesha hizo Halmashauri ni huu wa sasa hakuna namna, wazifute tu!!
 
Kama kuna ufujaji wa fedha ambao wananchi wa Tanzani wanabebeshwa basi ni kuwepo kwa Halmashauri za miji Tanzania. Hivi umuhimu wa kuwepo kwa Halmashauri hizi ni upi kama hazikusanyi kodi, zikifanya baadhi ya maamuzi yake yanaweza kutenguliwa na Waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa? Hazimiliki Ardhi, zinaweza kugawanywa wakati wowote bila ya kushauriana nao na Halamshauri hizi zinaendeshwa na wakurugenzi ambao wenye Halmashauri zao hawana sauti ya kuwaajiri ama kuwafukuza kazi.

Ni kitu gani kitapungua kama hizi Halmashauri hazitokuwepo kuliko hivi sasa hata ushuru kidogo wanaokusanya unaishia kuwalipa madiwani ambao ni kama simba wa karatasi kwani kila waliamualo likiwaudhi wenye nchi yao linabatilishwa? Kwa nini tusiache nchi ziongozwe na Wakuu wa wilaya na mikoa?
Halmashauri ya rombo chini ya chadema tokea 1995 ndio inaongoza kwa rushwa nchini!!!
 
Majizi chadema mwambieni Mbowe alipe Deni la Nhc na pia alipe wafanyakazi wa gazeti la Tanzania daima.

Mwambieni aache maigizo ya kukata, funua na kushika ukuta
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom