Hoja fikirishi: Watanzania tufanyeje ili tuwe na vipato vikubwa?

spleen

JF-Expert Member
Apr 24, 2013
3,225
4,662
Habari za mchana wakuu,

Baada ya habari na hasa tambo serikali iliyopita kuhusu nchi kuingia uchumi wa kati,ikibidi nijiridhishe kwenye vyanzo mbali mbali.

Ndio nikaja kugundua uchumi wa kati unaozungumziwa na watawala wetu kama njia ya kujisifu/kuonekana wanafanya kazi,ikiwa ni kama lengo la muda mrefu ni ule wa kipato cha usd kuanzia 3956.

Lakini kiuhalisia sisi tupo bado kwenye usd 1080,na hii imetokana na benki ya dunia kuweka vigezo vipya au kugawanya kua kutakua na lower middle income na upper middle income, sasa sisi tumeingia lower middle income lakini viongozi wetu wa kisiasa walikuwa waituaminisha kua tupo level sawa ya hio middle income countries economies.

......

Sasa tuje kwenye mada ikiwa hio higher middle income ya kuanzia usd 3955 hadi 12475, ndio iliokua target ya muda mrefu(kabla hio figure kubadilishwa, hivi karibuni).

Nikajiuliza sana kua usd 3955 ni kama milioni tisa hivi. Je, ni Watanzania wangapi wanaipata hio kwa mwaka?

Nikaja kugundua hata zaidi ya nusu(50%) ukichukulia wafanyakazi wengi Tanzania ni walimu, polisi, askari Magereza na wanajeshi wa vyeo vya kawaida tu. Je, mishahara yao kwa mwaka inafika laki tisa. Tukumbuke kipato kikubwa cha mfanyakazi ni mshahara.

Ni ukweli usiopingika wanaofanya kazi serikali kwa maisha ya Kitanzania ndio wanaonekana wana maisha mazuri kuliko kundi jingine la wakulima, wafugaji na wafanyabiashara ndogo ndogo.

Sasa ukizingatia bidhaa nyingi ukiacha za vyakula Watanzania huzinunua kutoka nje,ina maa ana kwa vipato vyetu vidogo tunatumia asilimia kubwa ya vipato vyetu kuagiza bidhaa nje ya nchi sawa na raia wengine wa nchi zingine wenye uchumi mzuri.

Sisi kama nchi tufanyeje angalau hata kwa hao wafanyakazi walio nusu ya wafanyakazi wote wawe na kipato cha kuanzia milioni tisa kwa mwaka, yaani usd 3955?

Jaribu kuimagine mtu kama daktari mwenye degree msahahara wake kwa mwezi ni chini ya USD 700, huyu mtu anafamilia,ana mke ana ndugu ana mahitaji mengine etc, na huyu ndio angalau mtu mwenye kipato kikubwa miongoni mwa watumishi wa eneo husika

Huyo mtu inabidi anunue gari inayotegenezwa na inayouzwa kwa bei za nchi za uchumi wa juu,anunue nguo,anunue mahitaji mengine yote zaidi ya 60% ambayo hayazalishwi nchini kwake etc.

Kwa kipato hiko?,hapo kumbuka kuna watu vipato vyao ni chini ya USD 200 tena wapo serikalini na sekta binafsi nakufanya biashara, sasa kiukweli watu wa aina hii tutaweza kweli siku moja tuvunje mnyororo wa umasikini na siku moja watoto wetu wawe wakulima wa kisasa, wavumbuzi na watu mbali mbali wenye tija kwa jamii kwa kipato hiko?

Ipo siku mtu atanunua hata usafiri zero km, ama km chini ya elfu 10 tu,kujenga nyumba imara itakayodumu kwa angalau miaka 50 tu?

Matokeo yake mtu unafanya kazi ili watoto wale tu,tena unakuta kwa kipato hicho cha USD 200, kama laki nne na nusu,unahudumia wanafamilia kama nane hivi, ukigawanya kila mtu ni kama elfu 50 kwa mwezi

Kuna haja ya sisi kama raia tuone tunfanyaje tufike wenzetu walipofika.

Tusilizike na hii hali ya maisha tuliyonayo kama mtu mmoja mmoja, jamii na nchi.

Tufanyeje waungwana ili tujikwamue kutoka hapa tulipo, basi angalau hata wafanyakazi wawe na hiko kipato cha uchumi wa kati.

Wakiwekeza wao hata sisi wa mtaani tutafaidika tu na uwekezaji wao na matumizi mbali mbali wanayoyafanya.

Kwa maisha ya Kitanzania hata mtu awe analipwa pesa kama yupo U.S.A basi lazima kuna ndugu yake au jamaa tu au rafiki,anaishi kama digidigi huko kijijini..

Unakuta ni mkurugenzi wa shirika flani anakula mamilioni ya mapesa sema ndugu zake ukiwaona utawaonea huruma.

Na kiukweli hawezi wapa hela wote wakatoboa,hii inaashiria hata kama mtu mmoja atajikwamua basi kwa kua amezungukwa na jamii masikini "impact" ya kujikwamua kwake haionekani.

Wadau wa jamii forum tupeni mbinu za kuondokana na huu unyonge,maana huwezi amini kipato cha raia wa Zimbabwe ni kikubwa kuliko hata raia wa TZ,yaani sisi ni katika ile kumi bora ya nchi masikini na sisi tupo yaani.

Umasikini so kitu cha kujivunia kabisa, imagine unakutana na msomi wa Tanzania taulo la mtumba, chupi, boxer, sidira kwa kisingizio ni nguo imara ila uhalisia hio boxer ikiwa mpya tu ni nusu ya mshahara wake,kama unabisha nenda mwenge,karume etc. Tufanyeje kama nchi kujikwamua hapa tulipo?

Note.
Hapa sizungumzii Watanzania wote bali nazungumzia watanzania wengi kundi linalofikia hata asilimia 90% ya maudhui ya huu uzi.

Screenshot_20210604-132903.jpg
 
Mi bado sijafika huko mkuu napambana,uchumi wa juu inabidi kipato chako kiwe kuanzi milioni 28 kwa mwaka,sio baada ya kustaafu ama baada ya kuuza mali za urithi ...yaani hustle zako za daily kwa mwaka ukijumlisha ukunje huo mpunga
Mkuu hatar sana me nafikisha lakin sio permanent kutokana na hustle Zangu kama mwaka wapili Sasa na make 100k per day
 
Tubadili namna ya kufikiri..
Kubadili baadhi ya mifumo.
Kivipi mkuu,unaweza toa mifano hai.....mfano huwezi amini nchi kama Palestine ambayo ukubwa wake ni kama kutoka mwenge hadi mbagala kipato Chao ni mara tano ya wa TZ na wanapigana vita kila siku,hawana ziwa,hawana mto hawana mbuga,......yaani kitu naogopa duniani na nahisi ndio zambi kubwa ni kuwarithisha umasikini watoto nitakaowazaa.......tupeni mbinu wakuu,munaodhurura duniani wenzetu wanafanyeje/wanaishiji?
 
Mkuu hatar sana me nafikisha lakin sio permanent kutokana na hustle Zangu kama mwaka wapili Sasa na make 100k per day
Hongera sana mkuu,....tupe mbinu tufanyeje/serikali ufanyeje ili ilipe raia wake hata nusu ya hio tu kwa siku?
 
Kivipi mkuu,unaweza toa mifano hai.....mfano huwezi amini nchi kama Palestine ambayo ukubwa wake ni kama kutoka mwenge hadi mbagala kipato Chao ni mara tano ya wa TZ na wanapigana vita kila siku,hawana ziwa,hawana mto hawana mbuga,......yaani kitu naogopa duniani na nahisi ndio zambi kubwa ni kuwarithisha umasikini watoto nitakaowazaa.......tupeni mbinu wakuu,munaodhurura duniani wenzetu wnaafanyeje/wanaishi?
Ndo tunarudi huko huko tubadili namna ya kufikiri..watz wengi ( majority) tuko mambumbu had inatia uvv!
 
Mkuu hata mimi mwenyewe magumash tu mkuu huku polin kwenye dhahabu
Pambana aisee.,....maisha yetu wa TZ ni ya kuoena huruma tu,tulio wengi.....kuna jamaa yangu amenunua Rav 4 ya Mwaka 1998,km zaidi ya laki,gari ina miaka zaidi ya 23 toka iundwe anatamba sana mtaani,wafanyakazi wenzake wanampa hongera kwa hatua aliyofikia......sio jambo dogo kusema kweli......lakini gari ina miaka zaidi ya 20?,mtu anapongezwa baada ya kuhurumiwa?.....umasikini mbaya wandugu,unatufanya tupate "fake respect" kwenye jamii baada ya kuonewa huruma
 
Hapa matatizo ni sisi mwenyewe Watanzania elimu zetu ni duni,tuna elimu za darasani but uelewa wa mambo ni sifuri.
Matatizo yote yanaanzia kwenye siasa zetu na watu tunao wachagua ambao wanapata kibali cha kufanya maamuzi huu ya maisha yetu.asikudanganye MTU siasa ina play 98 ya namba anavyotaka Taifa liwe.

Kupitia Siasa ambapo itaundwa Serikali ambayo itatunga Sera na kufanya utelekezaji wa Sera jumuishi za kiuchumi na kijamii kwa makundi yote ya watanzania.
 
Back
Top Bottom