Hoja fikirishi: 'Siri' za Baraza la Mawaziri zinawafikiaje Manaibu Mawaziri hadi nao waape kutozitoa?

Kuna vikao vingine Naibu Waziri huingia kama Waziri muhusika hayupo wakati mjadala muhimu kwenye kikao ni Wizara yake.

Jiulize, Unadhani kwa muda wote ambao Wizara ya Nishati na Madini haikuwa na Waziri ilikuwa haiwakilishwi kwenye vikao vya mawaziri?

Angalia hii picha ya aliyekuwa Naibu Waziri, Kigwangalla katika kikao cha baraza la Mawaziri

ikulu-jpg.577452
Hicho kikao ni cha juzi siku chache kabla mkaskazini hajaondolewa kwenye baraza. Namuona Angellah Kairuki kanenepa sana!
 
Eti nayo yanamuomba Mungu nakusali ayajaalie wakat maongo na ma nafiki hapo mengine yanaratibu kuwaumiza binadamu wenzao.
Unaandika kama vile wewe ni maraika asiye na dhambi!

Kwa fikra zako duni unadhani wale wote wanaosali/swali hawana dhambi.

Wakristo husema usihukumu ili usije kuhukumiwa.

Hata Yesu alikuja kwa wenye dhambi na sio kwa wasio na dhambi.
 
MsemajiUkweli labda nikuulize swali la mwisho.

Ni kwanini shughuli,mikutano na nyaraka za Baraza la Mawaziri zifanywa siri?

Kwanini haziko wazi kama Hansard,na Mikutano ya Bunge?

I will be thankful if you do answer my questions!
 
Nimekuwa nikifuatilia kuapishwa kwa Mawaziri na Manaibu Mawaziri mara kwa mara. Kati ya mambo wanayoapa kuyatekeleza ni kuihifadhi,kuilinda na kuitetea Katiba ya JMT. Pia,wanaapa kutotoa siri za Baraza la Mawaziri.

Kiapo hicho husemwa na Mawaziri na Manaibu Mawaziri. Kikatiba na kisheria,Manaibu Mawaziri hawahudhurii kikao cha Baraza la Mawaziri kwakuwa si Wajumbe wa Baraza hilo. Kinachozungumzwa katika kikao husika ndicho huwa siri za Baraza.

Kwakuwa siri hujulikana na Wajumbe tu wakiwemo Mawaziri (ambao wanaapa kutozitoa),nani huwapa siri za Baraza la Mawaziri Manaibu hadi nao waape kutozitoa? Katika maneno mengine,kuna haja Manaibu Mawaziri nao kuapa kutotoa siri ya Baraza la Mawaziri ambalo si Wajumbe wala hawahudhurii?
Mihitasari ya vikao huisoma
 
Kwakuwa siri hujulikana na Wajumbe tu wakiwemo Mawaziri (ambao wanaapa kutozitoa),nani huwapa siri za Baraza la Mawaziri Manaibu hadi nao waape kutozitoa? Katika maneno mengine,kuna haja Manaibu Mawaziri nao kuapa kutotoa siri ya Baraza la Mawaziri ambalo si Wajumbe wala hawahudhurii?
Mkuu kama wewe ni waziri,ukimpa naibu wako dokezo lenye maelekezo ya baraza la mawaziri alifanyie kazi maana yake umempa siri ya baraza la mawaziri,nae anapaswa kuitunza
 
Kiapo kimekosewa! Na waliokiandaa pengine hawajaliona hilo!! naibu waziri hayumo kwenye baraza la mawaziri!!!
pia alitakiwa kuapa kumshauri na kumsaidia waziri na siyo raisi!!! maana hata akipeleka taarifa za wizara kwa rais anapeleka kwa niaaba ya waziri. in short kiapo cha manaibu waziri kinatakiwa kurekebishwa kina kasoro kadhaa. Naibu anatakiwa awe chini ya waziri siyo chini ya rais.
 
Ofisi ya Waziri na Naibu wake ni moja kwa maana ya Wizara,hivyo kuapa kwao ni pamoja na kutokutoa siri za Ofisi yao.
Hasa ukizingatia kuwa Waziri kuna majukumu anamuagiza Naibu wake ambayo mengine ni siri kutoka baraza za mawaziri pengine pasipo Naibu wake kujua kuwa ni siri.
 
MsemajiUkweli labda nikuulize swali la mwisho.

Ni kwanini shughuli,mikutano na nyaraka za Baraza la Mawaziri zifanywa siri?

Kwanini haziko wazi kama Hansard,na Mikutano ya Bunge?

I will be thankful if you do answer my questions!
Mkuu,

Shabaha kuu ya serikali ni kutunza amani na usalama wa raia katika jamii.

Usalama wa nchi jinsi unavyotunzwa lazima iwe ni siri ili mbinu zake zisitambuliwe na maadui.

Huwezi kutunza amani kama uchumi wako ni mbovu na huwezi kukuza uchumi kama mipango yako inakuwa inatambuliwa na washindani wako.

Vikao vya Baraza la Mawaziri na baadhi ya maazimio yake lazima yawe siri kwa sababu kuu kama nilivyokueleza.

Kumbuka kuna siri zingine ambazo Rais anazifahamu lakini Mawaziri hawazifahamu.

Jaribu hata kuangalia katika ngazi za familia.

Hata wazazi hawawezi kuwambia watoto wao kila wanalotaka kulifanya au kuwafanyia. Wazazi wanaweza kukubaliana kuhusu mgawanyo wa mali za urithi kwa watoto wao lakini hawawezi kuwaambia na kama watawaambia watasema machache tu kuhusu mpangilio.
 
Kiapo ni kimoja kwa kuwa kuna wakati naibu waziri anaingia kwenye baadhi ya vikao pale ambapo Waziri mwenye dhamana anapokuwa hayupo. Pia, kuna mambo ambayo Waziri humbrief naibu wake for his/her information and/or actions na ndio "siri" zenyewe hizo. Nashangaa wengine wanakuja na majibu ya kipuuzi kama "kwani flani anasemaje". Uchizi huwa unaanza polepole.
 
Kuna wakati naibu waziri anaingia kwenye kikao kama mjumbe mwalikwa ingawa ni nadra kutokea hususan kama kuna jambo fulani linahitaji uwepo wake kwahiyo kuna sababu nyingi za kuapa hivyo hiyo ikiwa mojawapo
 
Back
Top Bottom