Hoja dhidi ya Hoja: Maswali Sahihi Huleta Majibu Sahihi: Tatizo la Kudhania Kutoonekana kwa Magufuli

Mimi nimekuelewa;

Tumejibiwa tusivyotegemea na kwakua majibu tuliyonayo hayafanani na tuliyopewa tunalazimisha wenye majibu sahihi kutoa majibu yanayofanana na yale tunayotamani kusikia; huku siyo kutaka kujua bali ni kutega tena kwa hila
 
Ngoja niisome taratibu bwashee!

Ni jambo jema kwa kuwa umeridhika na majibu ya waziri mkuu kulingana na maswali yalivyoulizwa!
Komenti baada ya kusoma na kuelewa ,acha kukurupuka.Na km hujasoma usikoment na km pia hujaelewa kaa kimya.Acha kumlisha mwandishi yale yanayokufurahisha wewe.Haitakusaidia wala si afya kwa ubongo wako.
 
Cha kushangaza ni kwamba wanaoulizia Rais aliko ni walewale waliotuambia yuko nairobi hospital, ni walewale waliotuambia yuko kati ya sehemu mbili🙄 india au china 🤔🤔

Yohane johnthebaptist hawa watu tuwaiteje!?
Unapouliza swali au kumtag mtu tag angalao wale wenye utimamu wa akili.Pengine ndege wafananao huruka pamoja ndiyo maana ukamtag huyo.
 
Uaminivyo ww na unavyoomba sisi hatuna shaka nayo,ila kwa vile tunampenda Rais Wetu tutaendelea kumwombea tu...Popote atakapokuwa ili harudi aendelee na ziara zake za kupambania wanachi masikini...Nyie hamtufai kiukweli
Upo mjomba? Mungu hadhihakiwi ameona amalizane naye, alishajikuta naye ni Mungu sana
 
Answers;
1. Rais yupo Ikulu ya Tanzania kama alivyosema Mh. Makamu wa Raisi na Waziri Mkuu
2. Kwasababu anachapaka kazi zake ofisini/ikulu basi ni mzima wa afya hii na kwa mujibu wa Mh. Makamu wa Rais na waziri Mkuu
3. Kama rais yuko ikulu anafanya kazi kama kawaida yake, ni mzima wa afya; kama tulivyojuzwa na viongozi wetu, yeye Mh. Rais ndiye anayeendesha nchi ndiyo maana hakuna jambo lolote la nchi ambalo tumejulishwa limekwama

Unayo maswali mengine?🤔
Haya basi sawa.
 
Kichaa ni wewe na ukoo wako wote!

Na wewe pamoja na hao wahuni wako huko Twitter lazima mtaumbuka tu,

Kila siku mnalalama mnaonewa kwenyr chaguzi sababu tume siyo huru. Muda huu yule muhuni wa ubelgiji na wafuasi wake badala ya wautumie kudai hiyo tume huru nyie mnautumia kufanya uhuni!

Sisi tunamsubiri yeye pamoja na nyie wafuasi wake mlete pua zenu 2025 ili tuwagonge kisawa sawa.
Hahahahahahahahahaha..vipi hapo..
 
Wala hata mimi sijazania kuwa Rais wetu anaumwa.
Naomba usirudie tena kunilisha maneno, nina mke na watoto na pisi moja matata sana wote wananitegemea mimi.
Basi naomba ww na hiyo familia yako na pisi yako muanze kunitegemea mm,mana naona mtegemezi wao utawapotosha
 
MASWALI YASIYO SAHIHI HULETA MAJIBU YASIYOSAHIHI: TATIZO LA KUDHANIA

Na. M. M. Mwanakijiji

Katika hoja yangu ya wiki iliyopita nilijikuta nami nimechokosa udhanifu (assumptions) katika kujenga hoja hiyo na hivyo kuingia kwenye mtego wa maswali yasiyo sahihi. Mtu anapouliza kitu anafanya hivyo kwa sababu anataka kujua au kujulishwa jambo fulani. Hata hivyo, wakati mwingine watu wanauliza maswali ambayo yanaangukia makundi mbalimbali.

Maswali ya Jela: Maswali haya ni maarufu kuwa ni maswali ya jela kwa sababu yanauliza kitu ambacho kiko wazi. Yanaitwa ya “jela” kwa sababu ukiona mtu yuko jela kafungwa ni kwa sababu kafungwa. Sasa ukimuona mtu kaingia na magwanda ya wafungwa halafu unamuuliza “na wewe uko jela”? anaweza kujibu kuwa ameenda kutalii! Maswali ya “jela” ni maswali ya vitu vilivyo wazi. Unakutana na mtu halafu unamuambia “mbona huoenakani bwana”? ni kichekesho.

Lakini pia yapo maswali ya aina nyingine; maswali ya kuudhi. Maswali haya hayana lengo la kutaka kujua kitu bali yanataka katika jibu anayejibu akasirike. “We mbona mjinga sana!” hili si swali ni kero. Ni maswali yenye kuchokoza hasira.

Lakini pia yapo maswali ya aina nyingine; yenye lengo la kudadisi lakini yenye kutaka kuchokoza ufahamu wa kitu. Maswali ya mtu kutaka kujulishwa kitu. Hata hivyo, wakati mwingine maswali haya yanajikuta yanakosa majibu sahihi kwa sababu ndani ya swali lenyewe kuna jibu linalopendekezwa.

Mfano mzuri ni suala la “kutoonekana” kwa Rais Magufuli hadharani kwa wiki kadhaa sasa. Swali hili linaulizwa huku kukiwa na pendekezo – anaumwa. Kwamba, wanaotaka kujua aliko tayari wamedhania kuwa anaumwa na hivyo wanataka uthibitisho kuwa ‘haumwi’. Hapa ndipo na mimi nilipounga tela na kutaka serikali iseme kama Rais anaumwa basi waseme “anaumwa”. Ndani ya swali langu nami kulikuwa na kudhania; kuwa Rais anaumwa.

Ni kwa sababu hiyo jibu la Waziri Mkuu wiki iliyopita naamini lilijibu swali lisilo sahihi. Jibu lake lilisema kwa ujumla wake ni kuwa Rais yupo anaendelea na kazi zake ofisini na kuwa anaweza kuwasiliana na viongozi wenzake. Na kuwa si lazima Rais atoke toke nje kuonekana ili kuridhisha tu udadisi wa watu. Kwa maneno mengine, jibu la Waziri Mkuu ni kuwa linajibu swali lililokosewa la “Rais anaumwa ndio maana haonekani”? Lakini pia limejibu maswali ya kama aliondoka nchini kwenda Nairobi kutibiwa au kukimbizwa hadi India usiku wa manane (kama ilivyodaiwa miezi kadhaa nyuma kuwa alikimbizwa Afrika ya Kusini halafu Ujerumani)! Labda hili si swali sahihi.

Naamini swali lililotakiwa kuulizwa kwa usahihi wake ni “Kwanini Rais hajaonekana hadharani au hata kupiga simu radioni au kwenye TV kama ilivyo kawaida yake na badale yake tunaambiwa tu ameongea na watu”. Na kuwa kama Rais yuko ofisini kuna ugumu gani wa yeye kuonekana kwa TV (kukiwa na ushahidi wa muda wa sasa) kuwa rais yuko anaendelea na shughuli zake? Kwamba, kuna ugumu gani kwa yeye badala ya kutuma tu “salamu” angepiga simu kama ilivyokuwa kawaida yake. Si mara moja Rais amepiga simu kwenye mkutano wa hadhara au tamasha na kuzungumza na wapenzi na mashabiki wake. Kinachozuia yeye kufanya hivi ni nini?

Hapa ndipo tunaweza kuanza kupata majibu ya uhakika au yenye kutosheleza udadisi wa watu. Lakini pia maswali mengine ambayo hayajaulizwa na yanahusiana na hili ni:

Mbona hatujamuona Mama Janeth Magufuli kwa muda karibu na ule wa Rais? Naomba kupendekeza kuwa inawezekana kuwa swali hili ndilo kubwa zaidi kuliko lile la kutoonekana kwa Rais. Lakini pia, watu wangeuliza – baadaya baadhi ya watendaji wa karibu wa Rais akiwemo Katibu Mkuu kiongozi kufariki kwa kinachodaiwa ni COVID-19 serikali imechukua hatua gani kuhakikisha kuwa Rais Magufuli na kundi la wasaidizi wa karibu limepimwa na kuhakikisha kuwa hawamuexpose Rais kwenye kirusi hiki? Na japo tumesikia vifo vya baadhi ya watu wa karibu hasa wa ngazi za juu; je, kuna watendaji na watumishi wengine wa chini wa Ikulu ambao ama wameugua au wamefariki kwa changamoto ya kupumua inayoweza kuhusishwa na COVID-19?

Katika kujibu maswali haya ni vizuri kuangalia kwa uhakika bila kudhania; hata tunaposema “COVID-19” je tunajuaje ndio sababu ya vifo vya watu hao isipokuwa ni vifo vilivyotokea wakati kuna wimbi la maambukizi? Je, serikali inafanya utaratibu gani wa kupima watendaji wakuu wa serikali. Binafsi nikiangalia mikutano ya Waziri Mkuu na Makamu wa Rais najiuliza kama wao wenyewe wanaamini COVID haijagusa Ikulu na kama ni hivyo, basi ni vigumu kujua kama ugonjwa huu umegusa watu Ikulu. Nje ya hapo, yumkini kuna tatizo jingine kabisa – lisilohusiana na COVID-19 ambalo limegusa afya ya Rais.

Lakini, kama Waziri Mkuu amesema Rais ni mzima, imara na anaendelea na shughuli zake za ofisini; tunaweza vipi kupinga? Na hili linajibu swali la Zitto juzi kuwa nani anaongoza nchi. Kama Rais ni mzima wa afya na anaendelea na shughuli zake basi utawala wa nchi haujakaimishwa kwa yeyote isipokuwa Rais mwenyewe. Makamu wa Rais anafanya shughuli zake zote kama Makamu wa Rais na hajachukua jukumu lolote kwani Rais hajashindwa kutimiza majukumu yake kwa sababu zilizoanishwa kikatiba. Kinachoitwa “ulinzi” wa Makamu wa Rais mbona hakuna kipya, ulinzi wa Mama Samia Suluhu Hassan umekuwa hivyo wakati wote isipokuwa mara nyingi watu hawafuatilii sana. Lakini pia kama Rais yuko Ikulu, Makamu anapotoka anaweza kuongezewa ulinzi. Nina uhakika kama kuna tatizo lolote la ombwe la uongozi Katiba yetu wala haina shida.

Kwa sasa tujaribu kuuliza maswali sahihi; ili tupate majibu sahihi. Vinginevyo sote tutakuwa tunaangukia huu mtego wa kudhania na matokeo yake kupewa majibu yenye kuridhisha tu udhanifu wetu. Maswali sahihi, huleta majibu sahihi. Hata kama ni majibu tusiyoyapenda au yasiyoridhisha.
Ulizidi kujitoa ufahamu!
 
Back
Top Bottom