Hoja binafsi za Arfi na Mnyika zazimwa kuwalinda Pinda na Lowassa

Paparazi Muwazi

JF-Expert Member
Dec 23, 2007
310
79
Hoja binafsi ya mbunge wa Mpanda Mjini Said Amour Arfi na ile ya mbunge wa Ubungo John Mnyika zimenyimwa fursa ya kuwasilishwa bungeni. Habari kutoka ofisi ya bunge hoja hizo zimezimwa kwa kuwa zingeibua mijadala mizito yenye kugusa vigogo ndani ya serikali na bunge. Chanzo hicho kimeeleza kuwa tayari bunge lilikuwa katika mivutano kutokana na hoja za posho, sheria ya mabadiliko ya katiba na mgomo wa madaktari hivyo isingewezekana kuingiza hoja nyingine.

Afisa huyo kutoka ofisi ya katibu wa bunge ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema kuwa hoja Arfi ingemgusa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuhusu uuzaji wa ardhi ya wananchi Rukwa wakati ile ya Mnyika ingemgusa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa kuhusu Richmond.


“Bado kuna kiporo cha utekelezaji wa maazimio ya bunge kuhusu suala la Jairo ambacho kinawagusa viongozi wazito akiwemo aliyekuwa katibu mkuu kiongozi na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali, hivyo hatuwezi kuingiza hoja nyingine kwa sasa”.


Chanzo hicho kimesema hoja mbili za wabunge Zitto Kabwe na January Makamba ziliingizwa ili kuchukua nafasi ambayo ingetumika kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa serikali kuhusu suala la Jairo na Taarifa ya Kamati ya Huduma za jamii kuhusu mgomo wa madaktari. Awali siku mbili za mwisho za bunge zilipangwa kwa ajili ya hoja binafsi za wabunge, lakini mvutano ndani ya CCM kuhusu muswada wa marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba na kuhusu mgomo wa madaktari zilifanya serikali isogeze mbele hoja zingine. Habari zaidi zinaeleza kuwa baada ya Spika wa Bunge kukabidhi ripoti ya Jairo na kuelezwa yaliyogunduliwa na kamati ya bunge kuhusu mgomo wa madaktari aliona kwamba itaivua nguo serikali hivyo akairudisha tena kwa serikali hali ambayo ililazimu hoja hizo mbili za wabunge kuingizwa katika ratiba ili kuziba pengo.

PM
 
Hakuna kitu hapo zaidi ya kutupotezea muda kusoma huu upupu!

Fisadi mkubwa wewe,tena uanche mara moja ku-comment ujinga humu JF hasa unapokuwa kwenye jukwaahili,hapa si mahali pa jokes,tena ukome kabisa tabia hii,ni afadhali ukae kimya na ufisadi wako.
Ungelikuwa unajua madhara ya ufisadi wala usingeliandika ujinga wako hapa.na ungelikuwa unajua jinsi Pinda alivyohusika na uuzwaji wa ardhi kwa muwekezaji wa kimarekani,huku wafugaji wakinyimwa maeneo makubwa kama hayo ili waendelee kuzalisha mifungo yao wakati serikali ikendelea kutoa elimu ya kuvuna mazao yatokanayo na mifugo wala usingekurupuka kuandika upupu hapa.Lakini pia ungelikuwa na moyo wa uzalendo wenye lengo la kupinga wizi wa rasilimali zetu na mambo yote yanayoletwa na ufisadi wala usingeshabikia upuuzi hapa.
Lakini tutaendelea kuwaomba waendelee kutafuta nafasi kwa bunge lijalo ili hayo mambo mpaka kieleweke,maana Richmond mpaka leo hakijaeleweka wal haijulikani nani hasa alihusika kwenye sakata hilo,na bunge la 9 Sitta aliufunga mjadala huo kwa ubabe.
Nawaomba Mnyika na Arfi wasichoke kuwaslisha hoja zao.
 
Hakuna jipya hapa sie hawa jamaa wanakamua wanavyotaka..coz hawana pingamizi raia wenyewe bongo lala hawahoji chochote
 
Jamani, sasa Sitta alitolewa uspika kwa sababu gani, sio kwa jinsi alivyo handle hoja ya Richmond Bungeni, kitu ambacho ndicho kikampa Makinda ulaji? Sasa na yeye aupoteze tena kama Sitta? Hilo lisingewezekana.
 
Anaesema huyu aliyeleta thrid anapoteza muda ni wale wale wazandiki na makuwadi wa mavisadi
 
Back
Top Bottom