Hoja binafsi ya Mnyika yatinga Bungeni KUHUSU KATIBA MPYA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja binafsi ya Mnyika yatinga Bungeni KUHUSU KATIBA MPYA

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Rutashubanyuma, Dec 27, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,787
  Trophy Points: 280
  Magazeti mengi ya leo yanatuhabarisha ya kuwa hoja binafsi ya Mbunge machachari wa Chadema kwa jimbo la Ubungo ya kuandaa mkakati wa kisheria wa kuandika katiba mpya imetinga Bungeni ..............................

  Gazeti la Tanzania Daima lina kichwa kisemacho................Chadema yawasilisha hoja binafsi bungeni..........................

  Mtanzania wao wameipa kichwa cha habari.........................Hoja binafsi ya Mnyika yatinga Ofisi ya Bunge..................................

  Huu utakuwa ni mtihani wa kwanza kwa Spika wa Bunge mama Anne Makinda kama kweli ana utashi na hekima za kuona watanzania wanatendewa haki au kama ataendelea kujikomba kwa chama chake ambacho tayari kupitia Waziri Mkuu Pinda kimekwisha kutoa mwongozo wa ya kuwa wao ni wa viraka tu...........hawaoni uhaja wa nchi hii kuwa na katiba mpya.......................

  Karibu Mama Makinda kwenye uwanja wa haki........tunasubiri kuona makali yako....................


  CHADEMA yawasilisha hoja binafsi bungeni
  • Wananchi wakumbushwa kutoa maoni

  na Tamali Vullu


  [​IMG] MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika, leo anawasilisha taarifa ya hoja binafsi kuhusu mchakato wa Katiba Mpya kwa Katibu wa Bunge. Mnyika alisema jana kuwa atawasilisha hoja hiyo kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge kifungu cha 55 (1) kwa ajili ya Bunge kupitisha maazimio ya kuweka utaratibu wa kiusimamizi na wa kisheria wa kuratibu mchakato mzima wa kuandikwa kwa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  "Nichukue fursa hii kufafanua kuhusu upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya watu kupitia baadhi ya vyombo vya habari mara baada ya kueleza kusudio langu la kuwasilisha hoja binafsi kuhusu Katiba mpya. Mimi kama mbunge ninapokwenda kuwasilisha hoja binafsi kuhusu Katiba mpya nafanya hivyo kama sehemu ya kutimiza wajibu wa kuwawakilisha wananchi na kulinda ukuu wa Katiba katika taifa letu.
  "Hoja binafsi ninayokwenda kuiwasilisha ni kwa ajili ya Bunge kwenda kutimiza wajibu huu wa Kikatiba ambao wabunge wote tumeapa kuulinda na kuutetea; kufanya hivyo hakuwezi kuwa tendo la 'unafiki' moja ya gazeti lilivyoeleza (sio Tanzania Daima)," alisema.
  Alieleza kuwa kumewakuwapo na upotoshoji unaoeleza kuwa anakusudia kwenda kuwasilisha rasimu ya Katiba mpya bungeni kupitia hoja binafsi na kueleza kuwa hilo si jukumu la mtu mmoja, chama, taasisi au dini bali ni jukumu la Watanzania wote.
  Mnyika alieleza kuwa anachowasilisha ni hoja binafsi kwa ajili ya Bunge kuazimia kuweka utaratibu utakaoanzisha, kusimamia na kuwezesha serikali kuratibu mchakato wa Katiba mpya utakaohakikisha wananchi wanashiriki kikamilifu kuandika Katiba kupitia tume inayohusisha wadau, elimu kwa umma, mkutano mkuu wa taifa wa Katiba na kura ya maoni.
  "Mtu binafsi, taasisi, chama au dini kila kimoja kinaweza kuwa na maoni yake kuhusu Katiba ambayo kinaweza kuyatoa kwa njia ya taarifa au hata kuandaa rasimu sifuri, lakini hatimaye lazima tuwe na mfumo wa pamoja ili kuweza kuwa na makubaliano ya kitaifa kwa kuwa Katiba sio mali ya chama chochote, dini yoyote au mtu yeyote bali ni sheria mama na mkataba kati ya wananchi na serikali," alisema.
  Alieleza kuwa suala la Bunge kuweka maazimio na utaratibu ikiwemo kutunga sheria ya kuratibu mchakato wa mabadiliko ya Katiba ni la muhimu na la haraka wakati huu ambapo tayari makundi mbalimbali ya kijamii yamejitokeza na kuweka misimamo yao wazi ya kutaka Katiba mpya na mengine kutangaza kuanza kuandika miswada ama rasimu ya Katiba husika.
  Aidha, mbunge huyo alionya kutokuwapo na utaratibu wa haraka na wa pamoja kila mdau atakwenda kwa mfumo wake, kunaweza kuzalisha mpasuko katika jamii kutokana na suala la Katiba mpya.
  "Sio jambo baya makundi ya kijamii kuandaa rasimu sifuri za Katiba, lakini kama kila kundi likaandaa rasimu yake halafu utaratibu wa kuunganisha maoni ya makundi mbalimbali kupitia chombo kinachokubalika na kinachohusisha wadau wote kuchelewa, taifa linaweza kuingia kwenye malumbano; ndio maana ni muhimu kwa utaratibu huo kuwekwa kupitia mkutano wa Bunge wa Februari," alisema.
  Wakati huohuo, mbunge huyo aliwataka wananchi na wadau mbalimbali kuendelea kutoa maoni kuhusu rasimu sifuri ya katiba iliyopitishwa na Kongamano la wadau Februari 17 mwaka 2007, baada ya kuwasilishwa na Kamati ya Wataalamu iliyoongozwa na Dk. Sengondo Mvungi.
  Katika kongamano hilo pamoja na kueleza ubora wa rasimu hiyo sifuri ukilinganisha na Katiba inayotumika hivi sasa wajumbe walieleza kasoro zilizopo kwenye rasimu sifuri ambazo zinahitaji kufanyiwa marekebisho kabla ya rasimu husika kukabidhiwa katika vyombo vya maamuzi.
  "Hivyo, tunakaribisha maoni ya umma kuhusu rasimu husika inayopatikana kwenye tovuti www.chadema.or.tz, maoni yatumwe kupitia info@chadema.or.tz au yatumwe moja kwa moja kwa kamati ya madai ya Katiba mpya," alieleza mbunge huyo.
  Muda mrefu sasa, kumekuwa na vuguvugu la madai ya kuwepo kwa Katiba mpya kutoka kwa taasisi mbalimbali, viongozi wa dini na wanasiasa. Joto hilo liliongezeka baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 31 wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kilipoamua kuvalia njuga madai ya Katiba mpya.
  Kilio hicho cha CHADEMA kimekuwa kikipata watu wanaoikiunga mkono wakiwamo wanasiasa mashuhuri nchini, viongozi wa dini, asasi zisizo za kiserikali na wananchi wa kawaida.   
 2. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  i like this brother,what a nice move
   
 3. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #3
  Dec 27, 2010
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Mnyika kafuata kanuni inavyotakiwa kuwasilisha hoja yake. Kanuni namba 55(1) aliyotumia tuisome wote inasema ifuatavyo:

  55.-(1):
  Isipokuwa kama Kanuni hizi zitaruhusu vinginevyo au kama Spika atatoa idhini yake kwa kutilia maanani udharura wa jambo lenyewe, hoja yoyote haitatolewa Bungeni mpaka iwe imewasilishwa na kupokelewa na Katibu angalau siku moja ya kazi kabla ya Mkutano ambapo hoja hiyo inakusudiwa kutolewa.
   
 4. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #4
  Dec 27, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Utendaji wa Mnyika unarudisha matumaini yaliyopotea kutokana na ubinafsi na kutopenda kuwatumikia wananchi kulikodhihirishwa na watawala wengi waliopo na waliopita
   
 5. Avocado

  Avocado Member

  #5
  Dec 27, 2010
  Joined: Aug 23, 2010
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huko ndio kuwajibika kwa wananchi,sio suala la kukaa na kusubiri,tuntaka vitendo zaidi kuliko maneno, Hongera Mnyika !
   
 6. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #6
  Dec 27, 2010
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,920
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Well and good. Lakini wanajamii swali moja toka kwangu "hivi ni asilimia ngapi ya wananchi wanajua katiba na umuhimu wake?
  Mimi nadhani ni watanzania wachache sana. Swala la elimu kwa raia lipo wapi? Mimi nipo pahala kuna watu wengi tu tena wengi ni wasomi ukifanya nae mazungumzo unagundua hata hajui katiba nini nini na inamhusu vipi. Sasa tunakwenda kwenye mchakato wa katiba mpya (if so) wengi wetu hatuna elimu ya hayo mambo mchango wetu utajumuishwa vipi? Pengine labda kwenye huo utaratibu mzima humo ndani kutakuwepo hiyo uelimishaji.

  Nachukulia mfano Kenya ambapo civil society ilikuwa so vibrant katika mchakato wa katiba mpya. Wengi wao wako knowledgeable about it na ilipelekea ushirikishwaji mkubwa sana wa raia. Nina wasi wasi na ushirikishwaji wetu hapa tz kama elimu ya uraia ipo kwa kiwango cha chini hivi.
   
 7. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #7
  Dec 27, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mkuu, suala ni utashi wa serikali juu ya hili; endapo itapitishwa bungeni, itajumuisha pia elimu kwa wananchi wajue wanatakiwa kuhusika kwa namna gani!!

  La sivyo tutaishia kulia lia tu... Ingawa serilkali ya JK ni butu na ina kiburi; ilichelewesha utekelezaji wa hukumu ya mgombea binafsi kwa sababu tu ati wamekata rufaa; walipiga dana dana hadi wakakchakachua!!! Lakini kwa nguvu ya umma na uhakika impact itaonekana!!
   
 8. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #8
  Dec 27, 2010
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Ungeangalia kipindi ambacho Mnyika alihojiwa alijibu swali lako kiurahisi kabisa. Na hata humu kuna thread alirudia kujibu vilevile.

  Urahisi wa kupangua hoja yako ni kwamba wanakosa kujua watanzania ni kutaja kifungu gani cha katiba chenye matatizo. Lakini wanajua athari za katiba mbovu.

  Mfano ni nani sasa hivi asiyejua athari za Tume kutangaza matokeo inavyotaka yenyewe na hakuna wa kuihoji.

  Hii ni moja ya athari za katiba mbovu wanazijua watanzania.

  Halafu mchakato wa katiba haujaanza leo. Mwaka 1981 had 1984 watu walituma maoni mengi kupitia Redio Tanzania, na kulikuwa na kipindi maalumu kilichoitwa mabadiliko ya Katiba.

  Hivyo hoja yako haina mshiko kwa maana ya kwamba mabadiliko yale yalikuwa batili kwani yalitolewa na waioelewa.

  Kwa sasa kama CCM hawatapenda kuelewesha basi vyama tele vinaweza kuifanya hiyo kazi mradi usilete mbinu za kuwanyima viwanja vya Mwembeyanga, Furahisha nk.
   
 9. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #9
  Dec 27, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Excellent move Hon. Mnyika, hakika kura yangu ilienda kwa mtu makini na mchapakazi.
   
 10. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #10
  Dec 27, 2010
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,920
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Aisee!! duu!

  Mkuu those days 1981-1984 elimu ya uraia ilikuwa vizuri sana. Hao watu kwa sasa ni wachache. Kuna hao waliozaliwa miaka hiyo up to now, hapo ndo tatizo lilipo. Angalia elimu inayotolewa kwa sasa humu mashuleni kwetu, uone kama haya mambo ya uraia kama yapo na kama yapo yana content gani. Unajua wengi wanaongea tu katiba katiba lakini hata kuiona hii ya sasa hawajawahi, wengi hawajui ni nini. Utakuta watu wanaongelea kipengele kimoja tume ya uchaguzi na labda madaraka ya raisi. Lakini that is not all about mabadiliko ya katiba yanayo hitajika. Anyway ni mtazamo wangu.
   
 11. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #11
  Dec 27, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,374
  Likes Received: 3,138
  Trophy Points: 280
  Zitto anasemaje hapo kwani tunataka hoja zetu binafsi asiziguse huyu kirusi
   
Loading...