Hoja binafsi: Viongozi wakuu CHADEMA washitakiwe...

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,223
11,287
Namshukuru Mungu amenipa nafasi kuleta hoja yangu binafsi mbele ya jukwaa huru la jamiifprums, naupongeza uongozi mzima wajamiiforum kwakufanya watu kama sisi kusikika mpaka magogoni tena ndani ya taahasisi za siri za mkuu. Nawashukuru sana.

Baada ya kutoa shukran niseme hii sii mara ya kwanza kuleta hoja kama hii na ikapata wanasheria na mwisho mbunge fulani wa chama akakamatwa na kutiwa ndani baada yakuikashifu serikali ya Rais Dr Magufuli.

Hoja yangu kubwa mbele ya jukwaa hili nikutaka viongozi wote waandamizi ndani ya chadema kukamatwa nakutiwa ndani kuanzia sasa ikiwa hoja yakutokuandamana wataipinga ama laa. Ktk kutoa sababu kwanini wakamatwe ningependa yeyote atachangia anipinge kwa hoja zakisheria na sio matusi. Kutukana mtu nikukosa hoja ama akili kufika ukomo wakufikiri.

Hoja yangu kutaka viongozi wote waandamizi kukamatwa inasababu zifuwatazo.

Kabla ya mkutano wa ndani wa chadema kulikuwa na kauli halali ya jeshi kupinga mikutano yote ya kisiasa ambayo haipo ktk ratiba za chama na mikutano iliyo ruhusiwa ni mikutano ya ndani ya vyama ambapo ccm ilianza na mpaka wamemaliza hapakuweko hoja toka viongozi wa ndani wa chama tawala kuwaambia wafanye mikutano ya kisiasa ila chadema kikao chao cha ndani walitoka na maazimio yakichochezi na kisudio lakufanya maandamano nchi nzima kupinga udikteta.

Pili sheria za nchi yetu zipo very clear mtu yeyote asie ridhika na utendaji wa serikali au maamuzi yake au matokeo ya uchaguzi anapaswa kufungua shauri mahakamani je maazimio ya chadema yanaushaidi wowote kabla ya kuazimia maandamano je wanalo shauri lolote lenye mashiko kuhusiana na kile wanataka kukifanya? Au ndio mtu yeyote asie ridhika anaingia barabarani kuandamana?

Tatu hoja ya maandamano nikupinga udikteta. Sasa tungependa kwa maandishi watueleze serikali ya kidkteta ipoje na Rais wetu ambaye hana hata mwaka amekuwaje dikteta wakati alichaguliwa kihalali na watanzania na mpaka sasa watanzania wamepata faraja na utendaji wake kiasi kila mahali hapa kazi tu.. Tunatakakujuwa hili.

Nne serikali yetu inabunge ambapo ndipo malalamiko ya wananchi yanapelekwa mbele ya serikali nakupata majibu stahiki na hatuna serikali ya direct government ambapo kila mtu anauwakilishi na ndio maana mbunge anakinga bungeni sasa inaluwaje chadema wasuse bunge alafu waje mtaani kuleta maandamamo je hii sii ajenda ya siri kuchafuwA amani yetu..

Tano katiba inakataza vyama vya siasa na raia wa tanzania kutumia vibaya uhuru wakutoa maoni. Katiba inakataza uchochezi na maneno yakuudhi lakini imekuwa tabia ya viongozi wa chadema kukashifu, kuzusha taharuki kwa watanzania pasipokujali wala tafakari katiba inasema nini je wanaweza kutueleza udikteta ndani ya serikali hii upo wapi? Je wananchi kupata dawa, mama zetu muhimbili kulala kwenye vitanda na sio kwenye baraza ndio udikteta?, kufukuza viongozi wabadhirifu ndio idicteta, kuanzisha mahakama ya mafisadi kwa kipindi kifupi ndio udkteta?, kuwafungia vibali wafanyabiashara wanyonyaji ndio ufikteta? Kufanya ziara za ghafla kwenye wizara ndio udikteta? Au kusema huu ni muda wskujenga taifa na sio siasa ndio udkteta. Tunaitaji kujuwa.

Last nani anawatumia na nikwa minajili gani?
Tukijuwa hayo na mengine ndipo warudi kitaa kujenga taifa
 
img_3312.jpg

UKUTA inawapa kiwewe chama cha mang'ombe.
 
Katiba inasemaje kuhusu Uhuru wa kutoa maoni,sheria ya vyama vya siasa inasemaje kuhusu mikutano,ukijibu haya bila kuingiza maneno ya kijinga kama hayo hapo juu,basi ntaamini wazazi wako hawakufanya kazi ya bure usiku ule
Tatizo nyie mliozoezwa kuandamana bila kutumia akili, hamsomi hata hiyo Katiba yenyewe.
Mnafikiri Katiba ni kufanya uhuni wowote katika jina la demokrasia.

Mbowe tsyari keshafanya kosa.
Fuatilia maudhui ya sheria ya vyama;

Sheria ya Vyama vya Siasa no 5 ya mwaka 1992 Kifungu 9(2)(c) na (f), inasema aidha vyama haviruhusiwi kutumia nguvu kufikia malengo ya kisiasa na kutotumia lugha za matusi, kashfa na uchochezi.
 
Hivi CCM mkawaacha UKAWA wakafanya mikutano na maandamao mnapungukiwa nini? Hamtakusanya hizo VAT?, hayo maendeleo miaka 50 mko madarakani maandamano ya siku moja au mbili yatazuia maendeleo yapi? Hoja kubwa hamtaki kusikia yale ambayo hamtaki kusikia zaidi ya kusifiwa kama Marehemu hata kama alikuwa Jambazi. Badilikeni Tanzania tajiri ya wananchi masikini ni yetu sote.
 
Tatizo nyie mliozoezwa kuandamana bila kutumia akili, hamsomi hata hiyo Katiba yenyewe.
Mnafikiri Katiba ni kufanya uhuni wowote katika jina la demokrasia.

Mbowe tsyari keshafanya kosa.
Fuatilia maudhui ya sheria ya vyama;

Sheria ya Vyama vya Siasa no 5 ya mwaka 1992 Kifungu 9(2)(c) na (f), inasema aidha vyama haviruhusiwi kutumia nguvu kufikia malengo ya kisiasa na kutotumia lugha za matusi, kashfa na uchochezi.
Sasa wapi Mbowe au UKAWA, wametumia nguvu,lugha za matusi,kashfa na uchochezi hapo?? Au unafafanua katiba kwa faida ya tumbo lako,acha upumbavu,Ng:eek:mbe kasoro mkia
 
Mwulize Msajili wa Vyama, utapata jibu lako, nyumbu mfuata maandamano!
 
Namshukuru Mungu amenipa nafasi kuleta hoja yangu binafsi mbele ya jukwaa huru la jamiifprums, naupongeza uongozi mzima wajamiiforum kwakufanya watu kama sisi kusikika mpaka magogoni tena ndani ya taahasisi za siri za mkuu. Nawashukuru sana.

Baada ya kutoa shukran niseme hii sii mara ya kwanza kuleta hoja kama hii na ikapata wanasheria na mwisho mbunge fulani wa chama akakamatwa na kutiwa ndani baada yakuikashifu serikali ya Rais Dr Magufuli.

Hoja yangu kubwa mbele ya jukwaa hili nikutaka viongozi wote waandamizi ndani ya chadema kukamatwa nakutiwa ndani kuanzia sasa ikiwa hoja yakutokuandamana wataipinga ama laa. Ktk kutoa sababu kwanini wakamatwe ningependa yeyote atachangia anipinge kwa hoja zakisheria na sio matusi. Kutukana mtu nikukosa hoja ama akili kufika ukomo wakufikiri.

Hoja yangu kutaka viongozi wote waandamizi kukamatwa inasababu zifuwatazo.

Kabla ya mkutano wa ndani wa chadema kulikuwa na kauli halali ya jeshi kupinga mikutano yote ya kisiasa ambayo haipo ktk ratiba za chama na mikutano iliyo ruhusiwa ni mikutano ya ndani ya vyama ambapo ccm ilianza na mpaka wamemaliza hapakuweko hoja toka viongozi wa ndani wa chama tawala kuwaambia wafanye mikutano ya kisiasa ila chadema kikao chao cha ndani walitoka na maazimio yakichochezi na kisudio lakufanya maandamano nchi nzima kupinga udikteta.

Pili sheria za nchi yetu zipo very clear mtu yeyote asie ridhika na utendaji wa serikali au maamuzi yake au matokeo ya uchaguzi anapaswa kufungua shauri mahakamani je maazimio ya chadema yanaushaidi wowote kabla ya kuazimia maandamano je wanalo shauri lolote lenye mashiko kuhusiana na kile wanataka kukifanya? Au ndio mtu yeyote asie ridhika anaingia barabarani kuandamana?

Tatu hoja ya maandamano nikupinga udikteta. Sasa tungependa kwa maandishi watueleze serikali ya kidkteta ipoje na Rais wetu ambaye hana hata mwaka amekuwaje dikteta wakati alichaguliwa kihalali na watanzania na mpaka sasa watanzania wamepata faraja na utendaji wake kiasi kila mahali hapa kazi tu.. Tunatakakujuwa hili.

Nne serikali yetu inabunge ambapo ndipo malalamiko ya wananchi yanapelekwa mbele ya serikali nakupata majibu stahiki na hatuna serikali ya direct government ambapo kila mtu anauwakilishi na ndio maana mbunge anakinga bungeni sasa inaluwaje chadema wasuse bunge alafu waje mtaani kuleta maandamamo je hii sii ajenda ya siri kuchafuwA amani yetu..

Tano katiba inakataza vyama vya siasa na raia wa tanzania kutumia vibaya uhuru wakutoa maoni. Katiba inakataza uchochezi na maneno yakuudhi lakini imekuwa tabia ya viongozi wa chadema kukashifu, kuzusha taharuki kwa watanzania pasipokujali wala tafakari katiba inasema nini je wanaweza kutueleza udikteta ndani ya serikali hii upo wapi? Je wananchi kupata dawa, mama zetu muhimbili kulala kwenye vitanda na sio kwenye baraza ndio udikteta?, kufukuza viongozi wabadhirifu ndio idicteta, kuanzisha mahakama ya mafisadi kwa kipindi kifupi ndio udkteta?, kuwafungia vibali wafanyabiashara wanyonyaji ndio ufikteta? Kufanya ziara za ghafla kwenye wizara ndio udikteta? Au kusema huu ni muda wskujenga taifa na sio siasa ndio udkteta. Tunaitaji kujuwa.

Last nani anawatumia na nikwa minajili gani?
Tukijuwa hayo na mengine ndipo warudi kitaa kujenga taifa
WE NI FARA,,,,USIFIKILIE HY MAGUFULI WENU NI MUNGU
 
Mawazo duni kutoka katika fikra duni. Sheria inasemaje kuhusu uhuru wa mawazo, haki ya kuandamana, haki ya mikutano kwa vyama vya siasa, wajibu wa raia kulinda katiba?

Anayezuia haki ya watu kutoa mawazo yao na anayezuia mikutano ya vyama vingine vya siasa lakini anaruhusu chama chake kufanya mikutano, jina sahihi la kiongozi huyo ni lipi?

Kutopambana na udikteta ni kukosa uzalendo maana ni wajibu wa kila mzalendo kuhakikisha katiba inalindwa.

Hivi hujiulizi kwa nini hilo unalotaka hakuna anayefikiria kulifanya? Hiyo itakuwa ni sawa na mtu aliyeiba ng'ombe halafu anafukuzwa na mwenye ng'ombe kisha anatokea mtu anamshauri yule mwizi aende mahakamani kumshitaki mwenye ng'ombe kwa kumfukuza akiwa na ng'ombe wa wizi.
 
Tatizo nyie mliozoezwa kuandamana bila kutumia akili, hamsomi hata hiyo Katiba yenyewe.
Mnafikiri Katiba ni kufanya uhuni wowote katika jina la demokrasia.

Mbowe tsyari keshafanya kosa.
Fuatilia maudhui ya sheria ya vyama;

Sheria ya Vyama vya Siasa no 5 ya mwaka 1992 Kifungu 9(2)(c) na (f), inasema aidha vyama haviruhusiwi kutumia nguvu kufikia malengo ya kisiasa na kutotumia lugha za matusi, kashfa na uchochezi.
Unasoma lakini huelewi. Kutetea katiba kwa nguvu zote siyo kashfa, siyo uchochezi na siyo matusi. Unajua ni kwa nini hao wenzako hawachukui huo ushauri wa kipuuzi ulioutoa?
 
WAFUASI WA CHADEMA MSITISHIKE HII NCHI SIO YA CCM PEKE YAO

Ndugu Mfuasi wa CHADEMA huu ni wakati wa kusikia sauti ya viongozi wetu tu. Kile kinachosemwa na viongozi wetu wa chama ndicho sahihi, Viongozi wetu hawajavunja Katiba wala sheria yoyote ndio maana CCM wanahaha na kushindwa kupumua sawasawa. Kwasasa wameamua kutoa matusi,kukejeli na kuwadharua Watanzania wanaotaka demokrasia hai.

Mtanzania/Mfuasi na mwana CHADEMA mpenda demokrasia na haki usisumbuliwe na maigizo ya CCM, hayo tumeyazowea tangia uhuru hadi sasa. Kaa ukijua muda huu ndio vyama pinzani uchwara vilivyo olewa na CCM vitajitokeza kuitetea CCM ili waingize mkono kinywani, msiwashangae hiyo ndio ajira yao. Usishange kumwona kiongozi wa chama kingine cha upinzani akipinga CHADEMA na kuitetea CCM hiyo ndio kazi waliyopewa kufanya ndani ya Nchi, hao ni wanafiki na wasaliti.

Tuwasikilize viongozi wetu na kuwatii,ili tujenge chama na demokrasia Tanzania. Kuna asasi na makundi mbalimbali vitajitokeza kupinga na kulaani msimamo wa CHADEMA katika operesheni UKUTA, msishangae wala kutetereka hao ni wale wale wa CCM sare ndio wanavaa tofauti na hizo ndizo kazi walizopangiwa na CCM.

Tuzidi kuwaamini viongozi wetu na kuwapuuza watu wenye maneno ya uwoga ya kutia watu hofu,haki haiombwi kwa maneno tu bali kwa vitendo kama UKUTA. Kuna vyombo vya habari vipo kwa ajili ya CCM sio kwa ajili ya Tanzania mvipuuze na mkae tayari tarehe 01/09/2016 ni mikutano na maandamano ya nchi nzima.

Kuna mtindo wa Polisi kujidai kwamba wanapata taarifa za kitaalam za kiintelijensia kuhusu usalama,hasa kwenye mikutano ya wapinzani na kushindwa kupata taarifa hizo kwenye matukio ya kihalifu yanayotokea nchini kila kukicha. Tunaiomba polisi pale watakapo pata taarifa za kiintelijensia waje kwa wingi watulinde ili tufanye mikutano vizuri sio kuvuruga taratibu za CHADEMA na kuwapiga Watanzania. Nchi za wenzetu siku hizi matukio yanatokea kwasababu wanakoswa taarifa za kiintelijensia mapema, lakini kwa kuwa Tanzania tumejaliwa kupata taarifa hizo hasa kuhusu mikutano ya upinzani tunawaomba ulinzi wa kutosha.

HAPA KAZI TU imekuwa chungu zaidi ya shubiri,badala ya kufanya kazi maneno ya kuwatukana wapinzani,watanzania na kuwadharau wanyonge ndio imekuwa kazi yao. Wanyonge wali ahidiwa mengi walichoambulia ni T-sheti na kofia huku maisha yakizidi kuwa magumu zaidi na zaidi. CCM ni waigizaji wanaopenda kuwa abudu watu wachache ndani ya chama. Wapuuzeni maana hata bei elekezi tu ya sukari hadi leo imewashinda kusimamia sasa wamebakia kutoa ahadi kila kukicha.Hakuna kazi wanayofanya inayosababisha wazue mikutano ya kisiasa na hawana sababu za misingi hata kidogo.

Jiandaeni kwa nguvu zote, simameni imara na msiogope chochote kile, hao mabwenyenye,maafidhina na walamba nyayo za wenzao achaneni nao. Taarifa za kupinga CHADEMA zitazidi kutolewa lakini pia mzidi kuwapuuza na mwendelee kusimamia kauli za viongozi wetu.

By Afixa

UKUTA
 
Back
Top Bottom