Hoja Binafsi: Serikali za Mitaa wana Ulazima katika kuokoa Wananchi!

SYLLOGIST!

JF-Expert Member
Dec 28, 2007
463
250
Heshima zenu nyote Wananchi.

Kwanza kabisa niwape pole wote waliokumbwa na vurugu zote zaku pambana na korona kumi na tisa. Poleni wanafamilia wote.

Pili, niwapongeze wale wote walio mstari wa mbele katika vita hii.

Tatu....Mheshima Raisi hawezi kufanya vyote kama wengi wetu tunavyotaka kuamini, kwa hilo basi....

Na katika pita pita zangu kwenye vyombo vya habari, sijaona wala kusikia Serikali za Mitaa zinavyojihusisha na mapambano ya Korona kumi na tisa, pamoja na kuwa serikali kuu ndio wahusika wakuu,

Serikali za mitaa ziwe na mikakati ya kuokoa Wananchi wa maeneo yao kwa kufuata "protokali" za kimataifa pamoja na mwongozo wa Mh. Rais

Sio lazima kuwe na "lockdown" nchi nzima, walakini maeneo yenye maambukizo mengi wawe na mikakati. Serikali za Mitaa must act!
 

Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
6,681
2,000
MKUU HUKU MITAANI CORONA IKICHANGANYA VIZURI SERIKALI ITAKUWA NA KAZI YA KUOKOTA MAITI BARABARANI
 

hyperkid

JF-Expert Member
Jun 7, 2019
1,492
2,000
TUEPUKE HOFU!!!.Ni hatari kuliko corona yenyewe kikubwa tahadhari ichukuliwe ,naiyamini serikali kwa ujumla binafsi nimemwelewa Sana raisi Magufuli

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
 

SYLLOGIST!

JF-Expert Member
Dec 28, 2007
463
250
MKUU HUKU MITAANI CORONA IKICHANGANYA VIZURI SERIKALI ITAKUWA NA KAZI YA KUOKOTA MAITI BARABARANI
Ndipo napoongelea huko, kwenye serikali za mitaa, mtaani, hatuwezi kusubiri mpaka hata mawazo mbadala yatoke Serikali Kuu...TAMISEMI must act...
 

SYLLOGIST!

JF-Expert Member
Dec 28, 2007
463
250
TUEPUKE HOFU!!!.Ni hatari kuliko corona yenyewe kikubwa tahadhari ichukuliwe ,naiyamini serikali kwa ujumla binafsi nimemwelewa Sana raisi Magufuli

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
Baba na Mama awe CCM ACT CHADEMA NCCR na wengine...Jamii ndio walio mtaani, wachukue hatua dhibiti hata pale wakitoa "lockdown" kwa wale vijana wao wanaorandaranda mitaani bila ya tija kwa kushirikiana na Serikali za mitaa badala ya kusubiria nguvu za Serikali kuu ambazo zina mkono mrefu wa dola.

Ukweli ni hofu tu ndio inayojengeka sasa. Jamii za watu mitaani lazima waongeze juhudi za kuondoa hilo...TAMISEMI must act.

HK, kwa mda Mh. Raisi amekuwa akisema kuwa siyo yote anaweza kufanya ndio maana ana wasaidizi kama hao serikali za mitaa...TAMISEMI must act wanamwelewa, tatizo ni kutenda bila woga manake wanafanya kwa hofu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom