Hoja binafsi, ni vipi naweza kukabiliana na ku escape athari hizi?

Pendaelli

JF-Expert Member
Feb 13, 2014
10,488
29,678
Habari za wakati huu wadau, mimi ni kijana wa miaka 27 kwenda juu. nizaliwa na kulelewa katika mazingira yasio ya kawaida baada ya mama kufariki nikiwa na miezi 3 na mwaka 1 baadae baba nae akafariki. nikajikuta chini ya malezi ya bibi ambae mwaka wangu wa 2 alikuwa hawezi kuona tena, akaw ananiteegemea mimi ninae on namtegemea kama mkubwa.

Hali ya maisha haikua nzuri kabisa kwani mwane aliebakia baada ya kufa mwingine hakua akimjali zaidu ya majirani tuu.halu hio ilinipekea kua mtu kuomba na kutegemea kuonewa huruma.
hali hio ilifanya nisijichanganye na wenzangu, kuogopa ogopa watu, kuona aibu na kuwa mkimya saana. mpaka na maliza shule ya msingi kula yetu ilikua ikinitegemea mimi japo changamoto ilikua ni nyingi la Mungu alinishindia.

Shida sasa nimekua ila zile athari zimekua nami mpaka sasa woga, aibu,ukimya, huruma, unyonge ambavyo vimepelekea maisha yangu kuwa duni mno. nimkuwa ni mtu wa kuonewa kutumiwa na kudhulumiwa na kunyanyasika hadi nimeshindwa kutimiza lengo lolote maishani mwangu.

Wakuu ni vipi naweza kuvuka hapa ilihali niliishia la saba na elimu ya ufundi seremala ambao kwa huo nimekuwa kibonde kwa watu. nivipi nitawez ku escape hapa ?
 
Pole
unaanza taratibu
shule jielimishe kidogokidogo

anza taratibu kukataa unyonge...utafika tu
uko hatua nzuri unajitambua tatizo lako tayari
 
Penda na kuthamini unachokifanya.
Maisha ni kile ukiishicho, jiamini, kuwa na imani na pambana naamini utaushinda unyonge.
 
Pole sana Mkuu, cha muhimu jaribu kuanza kujichanganya na watu wema ikiwezakana wenzio katika dini yako itakusaidia, pia kataa nafasi ya kujiogopaa, pia simamia misimamo yako kwa kujiamini nadhani itasaidia kutompa nafasi aliyepanga kukudhulumu naye kupata hofu
 
Huo unyonge na uoga kwa kweli sio rahisi kuvisahau kwenye maisha yako. Ila kuvitatua inategemea na hali halisi. Huwezi kumuachia mtu akudhulumu haki yako burebure tu. Kaa chini tafakari nini unahitaji kuzidisha na nini upunguze kwenye maisha yako. Nakutakia mafanikio mema
 
Hilo tatizo nilikua nalo!
Huwa natamani nije niiandike vizuri iwafikie wenye tatizo hilo tuko wengi, wengi linawamaliza kabisa!
Nimekulia mazingira yanayofanana na yako. Kwa bahati nzuri pamoja na unyonge nilisoma mpaka chuo kikuu, ila nilikuja kujua tatizo langu baada ya kuanza maisha, watu kunitumia na kunizulumu, Jasho nitoke mimi faida wale wengine, Nilifanya kazi kwa bidiii lakini naishia kuzulumiwa. Nilipojua tatizo langu kazi ikawa rahisi! Tatizo langu lilikua ni hili :
Kwa namna nilivyotendewa mabaya katika maisha yangu sikuweza hata kusimamia stahiki yangu nikihofia kumuumiza mtu, yaani yale machungu niliyopitia niliogopa kumsababishia mtu mwingine! Katika mazingira yoyote yale kati yangu na mtu mwingine niliona ni bora niumie mimi kuliko mimi nimuumize mtu mwingine, kufanya hivyo niliona ni kama kumtendea yale niliyotendewa nikaumia sana huko nyuma!
Hata kama tunashindana niliona huruma kumshinda mtu naacha tu ashinde asije akajisikia vibaya. Sasa watu wengi sio wema kiasi hicho wao walitumia huyo udhaifu kunipanda kichwani!
Nilipojua tu mara moja nikabadilika kichwani, ukishindana na mimi iwe kwenye kazi au biashara lazima nikomae nikushinde, sio dhambi. Haki yangu utanipa tu hata kwa nguvu, Nimekua aggressive (machachari) kazini napiga kazi zangu fasta fasta na kwa uhakika, najiamini na naheshimu kazi za watu, ule upole wa kumuangalia mtu akiniharibia sina tena, nasimamia maslahi yangu kwa nguvu zote.
Nimekua sharp kucheki michongo na kuiweka kapuni hakuna kumuonea mtu huruma ilimradi nafanya vitu halali basi,
Ni kukubali tu kwamba yale mateso na unyonge vimepita sasa ni kuchapa kazi na kujitengenezea maisha, linda maslahi yako kwa nguvu zote, hakuna mtu kula chako... Uchapa kazi na uaminifu ni vitu tunavyo sana hivi, vitumie sawa sawa ndio silaha zako hizo.
Usiwe na mashaka na chochote ufanyacho, jiamini, fanya kazi za watu kwa ubora na uaminifu na kuongeza ujuzi na juhudi kila siku basi
Usisahau kuweka akiba kabla hata ya kufanya matumizi mengine, najua hatunaga msaada tikikwama
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom