Hoja binafsi: Naomba saini zenu wanza JF dhidi ya JF Team!

Mlitika

JF-Expert Member
Mar 23, 2012
457
260
UTANGULIZI
Ni utaratibu wa kawaida na wa kiungwana kwa viongozi na wenye dhamana ya kusimamia mambo kujiwajibisha pale mambo yanapokwenda ndivyo sivyo katika vitengo vilivyo chini yao hata kama wao binafsi hawakuhusika moja kwa moja. Tunayo mifano mingi na sioni lazima kuitaja.

HOJA
Kwa takribani majuma mawili mambo yanakwenda mrama katika mtandao wetu tunaoupenda wa JAMII FORUM, hali iliyosababisha kukosekana mara kwa mara mawasiliano au kupatikana kwa taabu sana na kusababisha kero kubwa kwa watumiaji wa mtandao. Ikumbukwe kuwa watu wengi hasa tulio nje ya nchi na hata baadhi wa mikoani wanategemea sana mtandao huu kupata habari na kutoa mawazo.

MAPENDEKEZO
Kwa kuwa kukatika katika kwa mtandao wetu kumewakosesha wana bodi haki ya kupata taarifa na kutoa maoni; na kwa kuwa JF yetu ni mtandao wenye hadhi na heshima kubwa ndani na nje ya nchi; na kwa kuwa kuna team iliyopashwa kuchukua tahadhari haya yasitokee; na kwa kuwa hili limewakera hata JF Team wenyewe; napendekeza INVISIBLE NA TEAM YAKE WAJIPIGE BAN YA MWEZI MMOJA ILI KUONYESHA "ACCOUNTABILITY"

Wanaosema "ndiyo" waseme "NDIYOOOOO....................!"
 
Mpk sasa umeshaichangia Jf sh.ngapi ili iweze kujiendesha bila shida? sio kulalamika tu.....
 
sitasign kwa sababu kuna thread zinaelezea vizuri kabla ya tatizo na baada.....
 
UTANGULIZI
Ni utaratibu wa kawaida na wa kiungwana kwa viongozi na wenye dhamana ya kusimamia mambo kujiwajibisha pale mambo yanapokwenda ndivyo sivyo katika vitengo vilivyo chini yao hata kama wao binafsi hawakuhusika moja kwa moja. Tunayo mifano mingi na sioni lazima kuitaja.

HOJA
Kwa takribani majuma mawili mambo yanakwenda mrama katika mtandao wetu tunaoupenda wa JAMII FORUM, hali iliyosababisha kukosekana mara kwa mara mawasiliano au kupatikana kwa taabu sana na kusababisha kero kubwa kwa watumiaji wa mtandao. Ikumbukwe kuwa watu wengi hasa tulio nje ya nchi na hata baadhi wa mikoani wanategemea sana mtandao huu kupata habari na kutoa mawazo.

MAPENDEKEZO
Kwa kuwa kukatika katika kwa mtandao wetu kumewakosesha wana bodi haki ya kupata taarifa na kutoa maoni; na kwa kuwa JF yetu ni mtandao wenye hadhi na heshima kubwa ndani na nje ya nchi; na kwa kuwa kuna team iliyopashwa kuchukua tahadhari haya yasitokee; na kwa kuwa hili limewakera hata JF Team wenyewe; napendekeza INVICIBLE NA TEAM YAKE WAJIPIGE BAN YA MWEZI MMOJA ILI KUONYESHA “ACCOUNTABILITY”

Wanaosema “ndiyo” waseme “NDIYOOOOO....................!”

Kichwa cha habari (title) hakiendani na Majumuisho (Conclusion). Unataka sahihi au unataka tuseme ndiyoooo?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom