Hoja binafsi: Mwaka mzima wa masomo wa shule uahirishwe na mwakani uanze upya

Wazo ni nzuri kimtizamo ila unaufahamu kuwa kuna wanafunzi watoka huko ndani vijijini hata nishati ya umeme hakuna? Kufanya applications tu za vyuo ilikuwa hadi mtu asafiri wengine hadi makao makuu ya wilaya? Hii mbinu ingewezekana kama nchi nzima kuanzia vitongoji na vijiji vingekuwa na huo mtandao wa umeme na internet ikiwepo. Nje ya hapo ni tatizo kubwa sana kwa wengine.
Mbona mashindano makubwa kama World Cup na mengineyo yanatazamwa maeneo karibia yote na watu wenye hamasa ya kufanya hivyo??
This is just a matter of mind set...
Tukiamua kujaribu hatuwezi kushindwa!!!
 
Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa yote anayoyatenda kwa Taifa hilo hasa kwenye kipindi hiki kigumu cha ugonjwa hatari wa corona. Hakika, Mungu wetu atatunusuru na janga hili na kutusongesha mbele kama Taifa.

Pili, nikiri kuona na hivyo kupongeza juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali yetu sikivu na wadau wengineo za kupambana na changamoto za kiafya na kijamii zinazoletwa na janga la corona. Serikali yetu na wadau mbalimbali wanafanya jambo jema na hatuna budi kama watanzania wazalendo kupongeza juhudi hizo kimaneno na kivitendo.

Ugonjwa huu wa Corona tayari umeshaleta athari mbalimbali kwenye masuala mbalimbali kama kwenye elimu, afya, ajira na kadhalika. Taifa lipo kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa huu wa corona. Tayari shule na vyuo vyote nchini vimefungwa tangu mwezi wa Machi. Kufunguliwa kwake kutategemea hali itakavyokuwa.

Nawiwa kutoka mawazo/hoja yangu binafsi ya kuahirisha mwaka wa masomo kwa shule za awali, msingi na sekondari na mwakani uanze upya. Kinachopaswa kuamuliwa na kufanyika ni kutoandikisha darasa la kwanza tu. Madarasa mengine yatabaki kama yalivyo.

Kuhusu vyuo na vyuo vikuu, semista zao za pili zianze upya kwa muda ambapo hali ya kiafya na kijamii nchini itatengemaa. Nasema hivi kwakuwa wanachuo walishasoma semista ya kwanza tofauti na wanafunzi wa shule. Kuanza upya kwa semista za pili kutaathiri kuanza kwa mwaka mpya wa masomo. Lazima tukubali hill kwakuwa tayari limeshatokea.

Kuendelea kwa masomo kuanzia yaliposimamishwa,kwangu binafsi, kuna athari kubwa kwa wanafunzi wa shule. Masomo hupangwa kwa muda maalum wa kusoma na kupumzika. Tayari muda wa kusoma umeshaliwa. Tena, wanafunzi wa shule hawakuwa wamesoma vya kutosha kabla ya masomo yako kusimamishwa. Siioni miezi ya kulipa miezi iliyokwishapita.

Yapo madarasa ya mitihani huko mashuleni: darasa la NNE, darasa la saba, kidato cha pili, kidato cha NNE na kidato cha sita. Wote wasaidiwe kwa kuahirishiwa mwaka wao wa masomo ili mwakani waanze upya. Wanachoweza kushauriwa kwasasa wako na wazazi/walezi wao ni kujisomea ili wawe kwenye mstari wa masomo yao.

Kwakuwa masomo ya watoto na wadogo zetu yameshaathiriwa na janga hili la corona, kama Taifa, tukubali matokeo. Tukubali kuwa jambo hili limetukuta na kutuathiri. Ndiyo maana kama mzazi na mdau wa elimu natoa hoja ya kuahirishwa kwa mwaka mzima wa masomo kwenye shule za awali, msingi na sekondari. Vyuo na vyuo vikuu waanze upya semista zao za pili. Serikali yetu tulivu itoe muongozo tu kuhusu suala la ada zilizolipwa mwaka huu na zile za mwakani.

Nawasilisha.

Mkuu hoja yako ina mashiko ila baada ya kuvuka mto. Hapa tulipo hatujavuka mto na ndani kumejaa mamba wenye njaa. Kama vile haitoshi jemedari wetu yuko busy kuwatukana hao mamba.

Sasa mkuu kupanga mipango ya nini cha kufanya kabla ya kuvuka mto huo inaweza kuwa ni kujilisha upepo au ugoro kabisa.

Pana Corona inayoendelea kusambaa huru kabisa bila ya hatua zozote za maana kuchukuliwa ili ku idhibiti. Hakuna asiyejua, tumeanzia kwenye maombi na sasa tuko kwenye nyungu.

Hii haiwezi kuondoa Corona na kwa mwelekeo huu - ukweli mchungu. Corona itatumaliza.

Napendekeza tupate mkakati wa kuudhibiti ugonjwa huu kwanza kama jambo la dharura sana. Mengine yafuate baadaye. Si shule tu yako mengi mzuri na ya muhimu tu, ikiwamo miradi yote mikubwa na midogo.
 
Vipi kuhusu bundle mkuu watawawezesha naomba elimu hapo!

Sent using Jamii Forums mobile app

Hicho kikosi kazi ndio kitakuja na mapendekezo mujarab juu ya masuala yote hayo.

Ila suala la bando nadhani wanafunzi watatumia fedha wanazopewa na bodi ya mikopo au wazazi na walezi.

Sijui ni lini wamewahi kulalamika kuwezeshwa (na serikali) bando la WhatsApp, instagram, facebook, JF, YouTube n.k na hata bando la kusomea watake litoke serikalini.
 
Na bando wanapewa wanafunzi?? Kwa hizi mb za voda madogo si watakacha vipindi?? Akose kabisa bando la kucheki Diamond kapost nini Leo anunue bando la kusoma online??

Sent using Jamii Forums mobile app

Nadhani ni suala la vipaumbele tu, kama wanachuo watakua wanatunza bando kwa ajili ya kuangalia Diamond amepost nini mtandaoni badala ya kusomea online...
Nafananisha na mwanachuo ambaye ataamua kutokulipa ada chuoni badala yake hela hiyo akaitumia kwenda kwenye show ya mziki ya Diamond na akafanyia starehe huko. (It's all about priorities).

Kusomea online (mwanafunzi akiwa nyumbani) kutapunguza baadhi ya gharama za kumkalisha chuoni (chakula, makazi n.k) hela hizi zinaweza kutumika kwa ajili ya kununua bando kwa ajili ya kusoma.
Tusisahau hawa wanafunzi (sio wote) wana mikopo ambayo itawasaidia.

Lakini tunaweza kuongea na watu wa mitandao ya simu, wao Kama wadau muhimu katika hili wanaweza kusaidia kupunguza gharama za internet japo kwa kipindi hiki cha mpito ili kulifanikisha hili.
 
Mkuu kulingana na hali ya Corona kwasasa ingekua vizuri kama wanafunzi wangerudi shule tu sababu hali ya Corona nchini sio mbaya kama viongozi wetu wakivotueleza CC Petro E Mselewa
 
Nashauri wanawake wasibebe mimba mwaka mzima, ili kufidia hilo GEPU..:Dnatania

NGUMU, tuangalie beberu, atafanyaje kisha tu copy & paste...

Everyday is Saturday....................... :cool:
 
Nimeona UDSM wameunda kikosi kazi kwa ajili ya kufanikisha ''online learning''....
Kama hali ya Corona itazidi kuwa mbaya, vyuo na vyuo vikuu wanaweza kutumia njia za kimtandao kufundisha.
Kuhusu Sekondari, msingi na awali, nakuunga mkono mtoa mada
60% YA WANAFUNZI WAKO VIJIJINI MKUU HUKO HATA NETWORK YA KAWAIDA NI SHIDA HOW POSSIBLE WAO WATUMIE E LEARNING?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inawezekana pia kutunga mitihani yenye kurudi nyuma mwaka mmoja wa darasa husika ili kuweka uwiano ulio sawa.
Hata hivyo mtaala kama utaruhusu ni vyema ukajikita kwenye kutunga mitihani yenye maswali mengi rahisi yatakayotengenezewa uhaba wa muda.
Mfano,: 1.maswali 60@2dk=masaa 2.(std iv-vii)
2.maswali 30@4dk=masaa 2 (form 4 & 6)
(ule mfumo wa zamani wa udahili wa wanafunzi wa vyuo Vikuu)
3.Kwa upande wa vyuo vikuu na vyuo vya ufundi,waendelee pale walipoishia na majaribio /coursework nyingi ili kukimbizana na muda.
 
Back
Top Bottom