Hoja binafsi: Mwaka mzima wa masomo wa shule uahirishwe na mwakani uanze upya

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,197
25,516
Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa yote anayoyatenda kwa Taifa hili hasa kwenye kipindi hiki kigumu cha ugonjwa hatari wa corona. Hakika, Mungu wetu atatunusuru na janga hili na kutusongesha mbele kama Taifa.

Pili, nikiri kuona na hivyo kupongeza juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali yetu sikivu na wadau wengineo za kupambana na changamoto za kiafya na kijamii zinazoletwa na janga la corona. Serikali yetu na wadau mbalimbali wanafanya jambo jema na hatuna budi kama watanzania wazalendo kupongeza juhudi hizo kimaneno na kivitendo.

Ugonjwa huu wa Corona tayari umeshaleta athari mbalimbali kwenye masuala mbalimbali kama kwenye elimu, afya, ajira na kadhalika. Taifa lipo kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa huu wa corona. Tayari shule na vyuo vyote nchini vimefungwa tangu mwezi wa Machi. Kufunguliwa kwake kutategemea hali itakavyokuwa.

Nawiwa kutoa mawazo/hoja yangu binafsi ya kuahirisha mwaka wa masomo kwa shule za awali, msingi na sekondari na mwakani uanze upya. Kinachopaswa kuamuliwa na kufanyika ni kutoandikisha darasa la kwanza tu. Madarasa mengine yatabaki kama yalivyo.

Kuhusu vyuo na vyuo vikuu, semista zao za pili zianze upya kwa muda ambapo hali ya kiafya na kijamii nchini itatengemaa. Nasema hivi kwakuwa wanachuo walishasoma semista ya kwanza tofauti na wanafunzi wa shule. Kuanza upya kwa semista za pili kutaathiri kuanza kwa mwaka mpya wa masomo. Lazima tukubali hill kwakuwa tayari limeshatokea.

Kuendelea kwa masomo kuanzia yaliposimamishwa,kwangu binafsi, kuna athari kubwa kwa wanafunzi wa shule. Masomo hupangwa kwa muda maalum wa kusoma na kupumzika. Tayari muda wa kusoma umeshaliwa. Tena, wanafunzi wa shule hawakuwa wamesoma vya kutosha kabla ya masomo yako kusimamishwa. Siioni miezi ya kulipa miezi iliyokwishapita.

Yapo madarasa ya mitihani huko mashuleni: darasa la NNE, darasa la saba, kidato cha pili, kidato cha NNE na kidato cha sita. Wote wasaidiwe kwa kuahirishiwa mwaka wao wa masomo ili mwakani waanze upya. Wanachoweza kushauriwa kwasasa wako na wazazi/walezi wao ni kujisomea ili wawe kwenye mstari wa masomo yao.

Kwakuwa masomo ya watoto na wadogo zetu yameshaathiriwa na janga hili la corona, kama Taifa, tukubali matokeo. Tukubali kuwa jambo hili limetukuta na kutuathiri. Ndiyo maana kama mzazi na mdau wa elimu natoa hoja ya kuahirishwa kwa mwaka mzima wa masomo kwenye shule za awali, msingi na sekondari. Vyuo na vyuo vikuu waanze upya semista zao za pili. Serikali yetu tulivu itoe muongozo tu kuhusu suala la ada zilizolipwa mwaka huu na zile za mwakani.

Nawasilisha.
 
Mkuu, tafadhali nisome tena. Nimelizungumzia hilo
Ok.

But still, huoni mwaka utakaofuata patakuwa na idadi kubwa ya watoto watakaotakiwa kuanza darasa la kwanza, hao watakaobaki watapelekwa wapi?

Kwasababu kama hawatachukuliwa wote kwasababu ya upungufu wa vyumba vya madarasa, hilo tatizo litaendelea kuwa endelevu, hasa ukizingatia vyumba vilivyopo sasa bado havitoshi, nadhani tutaenda tengeneza tatizo jingine mbele ya safari ushauri wako ukifuatwa.

Binafsi naona muda bado unaruhusu shule zifunguliwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi unafahamu kuwa tangu shule zifungwe ni wiki3 na siku kadhaa tu za masomo ndizo zimepotea!!
Uzuri ni kuwa ratiba za masomo zina vipindi vingi sana vya kupumzika ambazo siku hizo zinaweza kufidiwa.
Napendekeza hadi siku za juma mosi zitumike ili kufidia ambapo mwezi januari unawezwa fanywa wa mitihani kwa madarasa yote ya mitihani.
 
Hivi unafahamu kuwa tangu shule zifungwe ni wiki3 na siku kadhaa tu za masomo ndizo zimepotea!!
Uzuri ni kuwa ratiba za masomo zina vipindi vingi sana vya kupumzika ambazo siku hizo zinaweza kufidiwa.
Napendekeza hadi siku za juma mosi zitumike ili kufidia ambapo mwezi januari unawezwa fanywa wa mitihani kwa madarasa yote ya mitihani.
Mkuu, tangu mwezi wa pili hadi leo ni wiki tatu? Sikuwa najua hili
 
... kutoandikisha darasa la kwanza kwa mwaka mmoja kutakuwa na backlog ya over a million. Sijui itakuwaje hapo. Wanandoa nao washauriwe angalau kwa mwaka huu na ujao wapange uzazi vilivyo ili vizazi vipungue ndani ya kipindi hicho. Otherwise, mzigo utakuwa mkubwa.
 
Back
Top Bottom