HOJA BINAFSI: Maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru yaahirishwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

HOJA BINAFSI: Maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru yaahirishwe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mchemsho, Nov 1, 2011.

 1. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #1
  Nov 1, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Nadhani itasaidia. Kwa sasa hali ya uchumi hasa mdogo (micro-level) ambao ndio hasa unawagusa wananchi wa chini moja kwa moja imekuwa mbaya sana, huku mfumuko wa bei nao ukipaa kwa kasi ya ajabu, hii imesababisha kupanda kwa bei za bidhaa muhimu kama vile mafuta, sukari na vyakula vingi, kwa upande wa pili pato la mwananchi limebaki kuwa lile lile la zamani au linazidi kupungua hivyo kuwapa wananchi wakati mgumu, wengi hawana tena hata uhakika wa ile milo mitatu kwa siku. Kwa upande mwingine serikali imetenga na inaendelea kuteketeza mamilioni ya shillingi eti kwa ajili ya maandalizi ya sherehe za miaka 5
  ya uhuru, bila kuchukua hatua za dharura kuunusuru uchumi unaolekea icu. Binafsi naona kama serikali inajitegea bomu yenyewe linaloweza kulipuka mda wowote, sina uhakika mfumuko wa bei utakuwa umefikia asilimia ngapi. Hofu yangu ni kwamba sijui nini kitatokea hiyo 9 disemba kama wananchi wataamua siku hiyo kudai upya uhuru wao wa kweli kutoka kwa genge la watawala mafisadi. Tusubiri tuone, Naomba kuwa silisha.
   
 2. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #2
  Nov 1, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 721
  Trophy Points: 280
  walivyo wapuuzi hawwezi kukusikiliza kaka........we ona hayo masherehe kila wizara yametafuna kiasi gani??!!!nchii hii inashangaza kweli
   
Loading...