Hoja binafsi kuhusu umri wa wabunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja binafsi kuhusu umri wa wabunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwongozo, Jun 19, 2012.

 1. m

  mwongozo Member

  #1
  Jun 19, 2012
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa mujibu wa katiba ya yetu ya mwaka 77, ili mtanzania agombee ubunge, anapaswa kuwa na umri usiopungua miaka 22. ruhusa huu umefanya bunge letu liwe na wabunge wengi vijana. ni jambo zuri! tatizo langu liko kwenye mwenendo na tabia ya vijana kwa ujumla. wabunge wengi vijana akina zitto, kafulila, mnyika, sugu. mkosamali, mdee, magige, bulaya.... nk..... hawajaoa au kuolewa. pana umuhimu kwao kuoa au kuolewa  NDOA HUJENGA AKILI NA NA HULETA HESHIMA

  nasisitiza wakaoe au wakaolewe kwa sababu uwezo wa kufanya hivyo wanao. ndoa humfanya mtu ajiheshimu na pia aheshmike. jamii humuona alieoa kama mtu aliekamilika.  UJANA UNAWASUMBUA WABUNGE VIJANA

  umri wa mtu aghalabu kuathiri upeo wake wa kufikiri na kujieleza. kitendo cha mnyika kumtukana mh Rais bungeni na kumuita dhaifu ni kinyume cha kanuni za bunge na ni kinyume na desturi zetu watanzania. la kushangaza alichokua anazungumzia hakimhusu Rais moja kwa moja! kusema hadharani bungeni kuwa "rais kikwete ni dhaifu" ni kauli ya kumdhalilisha mh rais. mnyika licha ya kuwa na shahada ya chuo kikuu, damu ya ujana inamsumbua. aliombwa na naibu spika kufuta kauli yake lakini akakaidi kufanya hivyo! mchango ambao angeutoa kuwawakilisha wana ubungo kuhusu bajeti hakuweza kuutoa baada ya kutolewa nje ya ukumbi wa bunge na naibu spika ndugai  NINI KIFANYIKE?  kwa nia njema nashauri katika maoni ya katiba mpya, tupendekeze umri wa mbunge uanze miaka 30. umri huu mtu anakuwa keshapitia mikiki mingi ya maisha. anajua la kusema kama mtu mzima aliekamilika. naomba kuwasilisha!!!!!!
   
 2. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,569
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Watu wamekupuuza na uzi wako! Ni pointless! Hivi komba wake wawili anaongea point? Unaweza mlinganisha na zitto au jj?
   
 3. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2012
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  wewe umri wako labda?maana huu uzi siyo wa kawaida!
   
 4. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #4
  Jun 19, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Kaka kwa akili hii naamini unachambuliwa sirini maana hii si akili kabisa mwaka 2012
   
 5. T

  TUMY JF-Expert Member

  #5
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka suala la kuoa ni personal sana huwezi jua kwa nini mtu hajaona ama hajaolewa, as long as wao wanatimiza wajibu wao katika lile ambalo wananchi wao wamewatua kwenda kulifanya mimi sidhani kama ni tatizo kiasi cha kuzuia utendaji wao wa kazi, japo pia una point nafikiri wahusika wamekusikia ama wamekusoma.:hand:
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Nonsense!
  Kama mtu kwa kuoa au kuolewa automatically anakuwa na Busara, basi kusingekuwa na sababu ya kuweka vigezo vinginevyo.
  Silly season?
   
 7. Piere. Fm

  Piere. Fm JF-Expert Member

  #7
  Jun 19, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,194
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Poor argument.
   
 8. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #8
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,125
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Sijaona kama malezo yako yana mashiko hata kidogo. Natamani mods wangekuwa wengi hapa jamvini ili waweze kupima mantiki ya kila thread. Nyuzi kama hizi zinashusha hadhi ya jamvi!!!!
   
 9. nkyalomkonza

  nkyalomkonza JF-Expert Member

  #9
  Jun 19, 2012
  Joined: Jun 18, 2012
  Messages: 1,165
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  jamani mara nyingi tumeshauriwa kutofikiri kwa kutumia makalio lakini hatusikii huu ushauri. Swala la umri linahusika vipi? Mnyika kaongea suala la ukweli. Watanzania wote wenye akili timamu wamempongeza.

  Sasa wazee kama wasira mbona wanaongoza kwa pumba?? Umri umewasaidia nini????
   
 10. m

  mwongozo Member

  #10
  Jun 19, 2012
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hoja yangu kuu ni umri. someni makala yangu vizuri. acheni ushabiki usiyo na tija...
   
 11. Malunkwi

  Malunkwi JF-Expert Member

  #11
  Jun 19, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 314
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  naona unataka kuongeza idadi ya posts zako ili upande cheo JF
  kuna wazee wangapi wasio na busara?? Tunajua ukweli unauma lakini hoja yako haina mashiko!
   
 12. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #12
  Jun 19, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 25,563
  Likes Received: 16,530
  Trophy Points: 280
  Tuangalie kwa undani hoja siyo umri hoja amesema kweli?Tufike mahali tuone kwamba vijana ni wakati wao na wanahaki ya kuongoza.Ule ujinga tuliokuwa tunalishwa zamani umepitwa na wakati.Unamwambia mtoto wako ati mtoto anaokotwa baharini wakati hata hapo alipo bahari hakuna.Kama ni ujinga waache watuambie jamani huu ni ujinga.Tufike mahali watanganyika tukubali kuambiwa ukweli japo unauma.Mnyika amesema kweliamesubiri pipi aliyoahidiwa hajaletewa kwa nini asimwambie baba yake uko dhaifu?Amechoka amesema ukweli.Mpongezeni tu hata kama inaumiza.
   
 13. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #13
  Jun 19, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Mwigulu Nchemba ameoa? Mbona mzinzi huyu mwenzetu?
   
 14. m

  mahoza JF-Expert Member

  #14
  Jun 19, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 1,242
  Likes Received: 411
  Trophy Points: 180
  Hakuna point hapo. Saa ingine bora ambaye hajaoa. Lusinde alivyotukana si ameoa? Sasa iweje awe na matusi hivyo. Wabunge vijana hawaongri matusi ila wazee wa chichiem.
   
 15. f

  fered mbataa JF-Expert Member

  #15
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 19, 2012
  Messages: 240
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi mwigulu,lusinde na mapressure hawajaoa? Mawazo na matusi yao hujasicia lipi tusi cwa president? its true ni dhaifu.
   
 16. Mbaga Michael

  Mbaga Michael Verified User

  #16
  Jun 19, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 2,914
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 160
  kweli anatuletea uji kaambiwa hapa kuna mzazi?
   
 17. b

  bdo JF-Expert Member

  #17
  Jun 19, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,712
  Likes Received: 1,611
  Trophy Points: 280
  hebu nisaidieni, hivi rais wa Botswana kaoa? na marais hawa-Liberia, Malawi, wameolewa? na hata Marehemu Kanani Banana rais wa kwanza wa Zimbabwe alikuwa na Mke? kama kwa hawa viongozi wa kiafrika naamini mmoja wao atakuwa au ni - mseja (hajaoa/ulewa) na wananchi wao wanawaamini? sasa iweje hawa wabunge wetu? thread yako siiungi mkono kabisa...
   
 18. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #18
  Jun 20, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Sredi yako pumba tupu! nawaomba vijana msikubali watu wengine waishi dunia yenu. Mpiganie maisha ya watoto wenu na wajukuu zenu. Achana na hawa mafisadi.
   
 19. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #19
  Jun 20, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  du, yaani hata ule usemi wa ukubwa wa pua si wingi wa makamasi umekupiga chenga?pole sana kwa kuwa na miaka 55 lakini akili za mwanafunzi wa chekechea
   
 20. UKI

  UKI JF-Expert Member

  #20
  Jun 20, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 699
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  nahisi umekosea njia mkuu jipange upya please siungi mkono hoja. sorry
   
Loading...