Dam55
JF-Expert Member
- Oct 8, 2015
- 5,592
- 11,831
- Thread starter
- #101
Tatizo kubwa hapo ni ujuaji tu mkuu. We unadhani Tume walikuwa wajinga hawajui hiyo sheria hadi wakatoa maelekezo wadhamini wahakikiwe kwenye ofisi za majimbo? Wagombea woote wa vyama vyote kumi nne walikuwa hawajui hiyo sheria Ila ni Lissu tu na CHADEMA ndio wanaojua sana Sheria?Tatizo hapa ni mihemko ndio inatupa shida.
Yaani ccm na matawi yake yote wanavyo hangaika kupata sababu za kuwakata wapinzani wao, halafu wapate sababu lakini wawaache wapite eti kwa busara?
Kama ungesoma vizuri halama za nyakati ungegundua kwamba kila mmoja yupo katika kumtega mwenzake ili apate nafasi yakujiongezea wapiga kura.
Alichokifanya Lissu kilikuwa mtego kwa tume, lakini tume iligundua mtego huo na kuuepuka.
Na hata tweet yao iliandikwa kimtego lakini wewe mleta uzi umeshindwa kugundua mtego huo na umekunasa. Matokeo yake habari nzima uliyoandika haina faida tena kwa sababu hata ushahidi wako wa hiyo tweet ya CDM umekataana na maelezo yako.
Labda nikusaidie mtego wenyewe ulivyo. Tweet yao inasema hivi:
"Kwa ajili ya kusimamia utaratibu wa kisheria, fomu za mgombea urais wa JMT mh Tundu Lissu hazikupita kwa wasimamizi wa majimbo ya uchaguzi kwa ajili ya zoezi la uhakiki".
Maana yake ni kwamba CDM wanajua kwamba fomu kuhakikiwa na wasimamizi wa majimbo ya uchaguzi si utaratibu kisheria, ndio maana wamesimamia utaratibu wa kisheria kutopitisha fomu hizo kwa wasimamizi wa majimbo ya uchaguzi.
Maana kuu hapa ni kwamba CDM walisimama katika sheria ndio maana hawakufuata kanuni kwa sababu wanajua sheria ipo juu ya kila kitu, na kanuni haiwezi kuwa juu ya sheria.
Hivyo ungeipongeza tume kwa kuhepuka mtego wa Lissu na chama chake. Na si busara ya huruma kama unavyotaka kuwaaminisha watu.
Alafu Kama haitoshi anakuja kulalamika kakarishwa muda mrefu huoni kama ni unafiki huo?
Mkuu penye haki tutetee lakini pia lazima wakati mwingine tuwaambie CHADEMA na Lissu wapunguze ujuaji mwingi.