Uchaguzi 2020 Hoja binafsi: Dkt. Magufuli anastahili kupewa miaka mingine 5

Ccm mpya ni certified gang criminal utekaji, ufisadi, ubambikaji, uzulumati, udhalimu, udikteta, usadukayo, ni pango la wezi na wanyangaji wanatumia uchaguzi Kama sehemu ya kutakasishia Kodi zetu.
 
Mnamo mwaka 2015 JPM alijipigia chapuo sana kuwa ni Rais wa wanyonge. Sikuelewa sana, nikasema ngoja nijipe muda nione.

Baada ya mwaka mmoja tu nikaona dalili za wanyonge kuumizwa sana, huku akidai ananyoosha nchi. Sikuelewa!

Hapa chini nakudadavulia mambo ambayo yanaonesha JPM alivyowafukarisha hoi bin taaban hata wale waliokuwa nacho kidogo.

1. Aliongeza makato ya bodi ya mikopo (HESLB) kutoka 8% hadi 15% kila mwezi
Mshahara hajaongeza hata tone, anadai anajenga reli, na kununua ndege. Hivi jamani, Rais hujaongeza mshahara wa mtumishi, unaongeza vipi makato? Naombeni mnisaidie kushangaa! Mshahara hutaki kuongeza, bado unawaongezea makato kweli?

Chini ya JPM, aliyekuwa anapokea laki 3, kwa makato haya amefanywa kupokea laki 1 na pointi.

(maskini amekuwa fukara, hoi bin taaban).

2. Alipandisha kilo ya sukari kutoka 1,800/- ya jk hadi sh. 2,500/- au zaidi
Wananchi wakiwa wanyonge vile vile kaingia kazuia kuingizwa sukari, bila hesabu wala maarifa. Matokeo yake sukari ikapungua, bei ikashuti. Kaanza kukimbizana na watu ma-godown huko. Ovyo kabisa!

Mwisho wa siku anatangaza eti bei elekezi eti sh. 2,500/- Nisaidieni kushangaa!

Hivi umekuta bei 1,800/- kwa kg, yeye jpm miaka miwili tu ikawa mara mbili sh. 3,000/-

Yani iko hivi hela ambayo maskini alikuwa ananunua kg 2, leo ananunua kg 1 tu imeisha.

(waliokuwa maskini amewafanya mafukara, hoi bin taaban)

3. Alizuia minada ya mazao kama mbaazi, korosho, ufuta n.k.
Akawapekekea jeshi watu wa kusini kuchukua korosho zao. Matokeo yake, bei ya mbaazi ikashuka kutoka sh 1500/- kwa kg hadi sh. 200/- kwa kg zikakosa wanunuzi, hasara kwa maskini.

Korosho zilivyobebwa hakuna ajuaye. Jeshi kwenye mambo ya kiraia, huwezi kuhoji. Wengine wakaishia kuambiwa korosho zao zilikuwa eti mbovu. Mpaka leo hawana kitu. Hawana hela na uendelezaji wa mashamba msimu mpya umekuwa mgumu.

(maskini mkulima amefanywa fukara, hoi bin taaban)

4. Bomoa bomoa ya nyumba DSM (Kimara), na huko Moro bila fidia kwa sheria ya mwaka 1938/50.
Huyu JPM aliacha sheria za miaka ya 80, za road reserve kuwa mita 60. Akachukua sheria ya kikoloni road reserve mita 120.

Kabomoa mpaka ambako barabara haitapita. Waliokuwa na nyumba, wakabaki nje na maskini hatari. Kwa maisha yale yale

(maskini akafanywa, fukara hoi bin taaban)

5. Hatoi ajira
Toka ameingia madarakani ni madaktari elfu 3 na ushee na walimu baadhi wa sayansi ndio waliajiriwa.

Yani mzazi kasomesha mtoto, kwa kujikamua, enzi za jk walimu walikuwa hawaombi ajira, ilikuwa ukimaliza ualimu degree, au cheti/diploma, unasubiri kupangiwa kituo. Ukatae mwenyewe kazi. Ila leo soma, maliza ng'ombe za wazazi, na kazi JPM hatoi.

(maskini amekuwa fukara zaidi, hoi bin taaban)

6. Hakuwajengea walioharibikiwa nyumba na tetemeko la Kagera pamoja na kukusanya michango kila pembe ya dunia.
Maskini wa Kagera, akaambiwa hajaletewa tetemeko.

(maskini akawa fukara, hoi bin taaban)

7. Kikokotoo cha pensheni ya wastaafu.
Akaleta kikotoo eti ukistaafu zile hela ulizohifadhi, upewe kiduchu. Yani ufanye kazi miaka 60, uzeeke. Wkt unataka hela yako, jpm anasema chukua kiduchu. Huko nyuma wastaafu walikuwa wanapewa mara moja 75% ya hela , yeye akasema wapewe 25% tu.

(hapa maskini mstaafu anapunguziwa hata jasho lake la kwenda kupumzikia). Fukara, hoi bin taaban.

8. Kahawa huko kagera alikuta wanauza kilo 2500/-, kazuia wa Uganda wasije kuinunua. Ikashuka bei hadi sh 1000/-

Maskini akawa fukara zaidi, hoi bin taaban chini ya JPM.

Kwa ufupi:
Wakulima hoi bin taaban
Wafanyakazi hoi bin taaban
Wastaafu hoi bin taaban
Waliomaliza vyuo hoi bin taaban
Wafanyabiashara hoi bin taaban
Wavuvi hoi bin taaban

Eti huyu anataka mi5 tena!! Afanye nini?

Huyu ni rais wa wanyonge gani?

Ongezea wengine walio hoi bin taaban
 
Kuua watu ndo mbinu ya mwisho ya viongozi waliokosa vibali machoni pa wananchi. Meko na CCM mmekosa kibali cha watanzania.CCM wana hofu kuu,imagine wanaua watu,wamezima whatsapp call,nasikia leo saa sita mchana bank zinapigwa pini,wamezima whatsapp call,wanazuia SMS,etc.Hii ni hofu ya kukataliwa na wananchi
Mtukufu Mkoloni kaburu mweusi hataki kutoka ikulu kwa hofu ya kunyang’anywa kinga kama kule Malawi kisha kushinda mahakamani kama Elbashiri wa Sudan au Jacob zuma wa Africa kusini
 
Sijui ni mahaba au kitu gani, Ila naona aibu Mimi mtu Kama mzee mwanakijiji kuamua kujitoa ufahamu na akili zake nyingi ili kusapoti ushenzi na uuaji. Never trust a hungry man!!!
 
Sijui ni mahaba au kitu gani, Ila naona aibu Mimi mtu Kama mzee mwanakijiji kuamua kujitoa ufahamu na akili zake nyingi ili kusapoti ushenzi na uuaji. Never trust a hungry man!!!
Ni mnufaika au ni mnyonge ( a futureless person) asiye na mbele.Maana yeyeto amabae ni civilized na educated katu hawezi sapoti Utawala dhalimu unaopambana na watu badala ya maendeleo
 
Tii sheria bila shuruti ijali familia yako

Usijaribu kupima kina cha maji
Hao mnaowategemea Wana utii wa kwenye uniforms tu sababu mmewazulumu haki zao ikiwemo nyongeza za mishahara ndo Wana hasira nanyi hatari hata wao wanataka mabadiliko mtashangaa watakavyokukugeukeni
 
Tii sheria bila shuruti ijali familia yako Usijaribu kupima kina cha maji
Hao mnaowategemea Wana utii wa kwenye uniforms tu sababu mmewazulumu haki zao ikiwemo nyongeza za mishahara ndo Wana hasira nanyi hatari hata wao wanataka mabadiliko mtashangaa watakavyokukugeukeni
 
Mateso manyanyaso wafanyabiashara wakubwa wadogo kubambikiwa kodi kubwa TRA kupewa kesi za uhujumu uchumi, BOT kuwapora wafanyabiashara wakubwa wawekezaji na watu wa kawaida pesa zao zinazotumwa tokea nje na wakipiga kelele wanaoishi kubambikiwa kesi za utakatishaji fedha, unataka viendelee kwa miaka mingine mitano tena? au unataka nini maana haya ni mojawapo ya manyanyaso yaliyopelekea kuitaka CCM itoke ikulu Nchi ipate uhuru haki ipate kutamalaki
Hayo manyanyaso ya wafanyabiashara yakoje? Ulitaka wasilipe kodi?

Kwa hiyo kama mtu ana kosa la uhujumu uchumi aachwe? Mbona sio kila mtanzania anapewa kosa la uhujumu uchumi? Una mtetea Sethi?
Kama watu wanatakatisha pesa unataka waachwe wakati kuna sheria ya kuwabana? Tumia akili,acha kupinga pinga.
 
Ccm mpya ni certified gang criminal utekaji, ufisadi, ubambikaji, uzulumati, udhalimu, udikteta, usadukayo, ni pango la wezi na wanyangaji wanatumia uchaguzi Kama sehemu ya kutakasishia Kodi zetu.
BOT kwa Amri za Doto na mtukufu kaburu Mkoloni mweusi wamepora pesa nyingi za watu mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara wakubwa wadogo wazee vijana wawekezaji nk na pindi walipopiga kelele wakawatishia kuwabambikia kesi za utakatishaji fedha, hizo pesa zote wanazo wao binafsi ni unyama unyanyasaji uporaji ulioje, hii ni kero kubwa mno na ndiyo imetengeneza chuki kubwa tokea kwa wananchi wawekezaji na kupelekea wafanyabiashara wakubwa na wawekezaji kwenda kuhamishia pesa zao Uganda Zambia kenya na sehemu zingine Duniani.
 
Tetesi musiba,dotto, bashite walionekana viunga wanachukua pasipoti mpwa ili watoroke nchi kwa hofu waliotenda.
 
Weka tiki (vema) kwenye jina la mwisho la mgombea, hakikisha hiyo vema ama tiki yako haitoki nje ya kibox (kisanduku). Pia usitoboe macho kwa mgombea number moja kwa hasira maana kufanya hivyo utakuwa umeharibu kura yako.
 
Tii sheria bila shuruti ijali familia yako Usijaribu kupima kina cha maji

Weka tiki (vema) kwenye jina la mwisho la mgombea, hakikisha hiyo vema ama tiki yako haitoki nje ya kibox (kisanduku). Pia usitoboe macho kwa mgombea number moja kwa hasira maana kufanya hivyo utakuwa umeharibu kura yako.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom