PakaJimmy
JF-Expert Member
- Apr 29, 2009
- 16,203
- 8,724
Wanabodi,
Nasikiliza Redio One stereo, kipindi kinachoitwa Yaliyomo Yamo.
Kuna hoja inaendeshwa ikitaka ifanyike petition kwenye makampuni ya simu kupitia TCRA ili bei ya SMS ipandishwe sana ili kuwakomesha watu waliozua mitindo inayokera ya kutunga meseji za kila tukio linalotokea nchini ikiwa ni pamoja na kuzua vifo vya watu. Walitoa mfano kuwa kuna meseji zilizosambazwa jana kuwa MwanaBongo Flavor aliyezikwa jana amekutana na Kanumba na Mafisango...!
Aidha walisema kuna sms nyingi za matusi na mambo yasiyo ya kistaarabu zinazotungwa na kusambazwa kila kukicha, bila kujali umri wa mtumiwa, kisa ni bei poa ya utumaji.
Wamesema makampuni ya Mawasiliano yafute meseji za offer na kupansdisha sana bei ya sms, wakidai itawakomesha waharibifu hao wanaozua au kuamsha simanzi kwa waliofiwa.
Mdau,
Unaionaje hoja hiyo?...je ndiyo mwarobaini wa hizi meseji?