Hoja au vioja vya Mtatiro?

wandamba

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
510
839
Moja ya sababu ya Julius Mtatiro mmoja wa vijana waliokuwa wakihoji kutaka maendeleo ya haraka ya Tanzania kuhama upinzani leo ni sababu inayofikirisha sana.

Ni sababu inayosadifu mwelekeo wa siasa za Tanzania katika zama hizi mpya.

Julius ameeleza sababu ya kuondoka alikokuwa ili "akapate zaidi fursa ya kufanya siasa za maendeleo."

Hakika niemwelewa, Siasa katika asili yake si mchezo mchafu kama baadhi wanavyotaka kusema...Nadharia sahihi ya siasa ni maendeleo.

Hakuna mwanasiasa awe yeyote wa kweli anayeweza kusema anafanya siasa kwa ajili ya mzaha. Siasa msingi wake ni kutafuta fursa ya kufanya au kuleta maendeleo.

Ndio maana siku Dr. Slaa alipoona CCM wamembania alitafuta fursa Chadema ya "kuleta maendeleo."

Siku Lowassa alipoona CCM hana nafasi akaenda Chadema kutafuta "fursa ya kuleta maendeleo."

Ipo mifano mingi lakini nimalizie pia kuwa hata Zitto Kabwe alipoona Chadema hakuna fursa alihamia au kuanzisha ACT ili kupata fursa ya "kuleta maendeleo."

Julius Mtatiro namfahamu bayana kuwa anaamini katika Tanzania yenye neema tele.

Tanzania yenye ukuaji mzuri wa uchumi, Tanzania yenye uongozi unaofanya uamuzi kwa maslahi ya nchi na watu wake.

Namfahamu Julius kuwa kijana anayeamini katika kupinga rushwa, ufisadi na anayeamini katika siasa za kuwaletea wananchi maendeleo.

Rais Magufuli anayafanya yote haya ya maendeleo: amekuza uchumi, ameongeza mapato ya Serikali, amepiga vita rushwa na ufisadi ipasavyo, anatekeleza miradi mbalimbali ya kuwaondoa Watanzania katika unyonge na anasimamia mageuzi ya kimaendeleo.

Sikupata fursa ya kumuuliza Julius anaamini siasa ni nini lakini kwa leo ametupa jibu kuwa yeye ni muumini wa siasa za maendeleo na siasa ambazo ndio msingi wa utawala wa Rais John Pombe Magufuli.

Kwa muktadha huu sitashangaa wanasiasa wote wanaoamini katika maendeleo wakiungana na JPM na kuwaacha wale wanaoamini katika siasa ni mchezo mchafu wabaki huko huko kwenye michezo michafu.```
 
Tumbo ni maendeleo
IMG-20180810-WA0054.jpg
 
Kuiba kura, kupora ushindi na kubambikizia wapinzani kesi fake kunakofanywa na ccm aka gambas hizi ndio siasa safi sio? Ni suala la muda tu msipomfunga break huyo mtu wenu mjue hata baki mtu salama.
 
Mnachotaka kuwaaminisha watanzania sicho, nini mnahofia kutoka upinzani..

Miaka zaiidi ya 51 ya Uhuru leo ndiyo mnawahadaa watanzania eti mnaleta maendeleo,

Upinzani hautokufa ata tusalie wawili,tatizo la msingi bado hamjalitatua hivyo msitegemee upinzani kufa.
 
Mnachotaka kuwaaminisha watanzania sicho, nini mnahofia kutoka upinzani..

Miaka zaiidi ya 51 ya Uhuru leo ndiyo mnawahadaa watanzania eti mnaleta maendeleo,

Upinzani hautokufa ata tusalie wawili,tatizo la msingi bado hamjalitatua hivyo msitegemee upinzani kufa.
Kwa kweli! Upinzani ni fikra sio vyama. Huwezi kuua fikra!
 
Kambi ya Maalim Seif imepoteza Mwenyekiti

Huyu Ni wa pili Baada ya Taha Taslima

Inabidi akamuombe samahani Prof Lipumba Au nae akaunge Mkono Juhudi Za Mbowe Kwa kujiunga Chadema
 
Kwa mtu ambaye anaishi kwa kusubiri kuteuliwa wakati ndio huu, amesoma alama za nyakati mpaka mteuaji aondoke mnamo 2015 nae ataambulia tu
 
Back
Top Bottom