Hogera sana Mzee Mwanakijiji kwa sera yako ya Gomea tozo ya kodi kwa laini za simu

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,170
2,000
https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/488914-siku-3-za-kuanza-kugomea-kodi-ya-sim-cards-july-29-30-na-31-a-11.html#post6946777Tozo ya kodi kwa laini za simu - Bunge letu litakuwa limepata somo la kutosha:

"Kufutwa kodi ya simu, Bunge aibu tupu"


Hatua ya Rais Jakaya Kikwete kutia saini hati ya dharura ili Muswada wa Fedha wa mwaka 2013 ufanyiwe marekebisho na kuondoa tozo ya kodi kwa laini za simu imeliacha Bunge katika fadhaa na fedheha kubwa.
Bunge la Bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2013 lilishuhudia wabunge wa chama tawala wakitumia wingi wao bungeni kupitisha kodi hiyo ambayo iliamsha hasira na vilio kutoka kwa wananchi kutoka kila kona ya nchi.
Tunasema hatua hiyo ya Rais imeleta fadhaa na fedheha kwa Bunge kutokana na kuwapo matukio mengi ya aina hiyo katika kipindi kifupi, ambapo Bunge limekuwa likipitisha miswada mingi muhimu kwa ushabiki wa kisiasa badala ya kuangalia masilahi mapana ya taifa. Rais kwa kuwasitiri wabunge wa chama chake amekuwa akitia saini miswada hiyo na kuwa sheria, lakini baadaye amekuwa akisikiliza hoja za wapinzani na kulazimika kurudisha sheria hizo bungeni ili zifanyiwe marekebisho.
Siyo nia yetu hata kidogo kuorodhesha hapa sheria zote ambazo Rais amezirudisha bungeni kufanyiwa marekebisho katika miaka ya hivi karibuni. Hata hivyo, wasomaji wetu watakumbuka kuwa, moja ya sheria nyeti zilizorudishwa bungeni ni Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo ndiyo hasa iliyoanzisha mchakato wa kupata Katiba Mpya yapata miezi 18 iliyopita. Kama tulivyosema hapo juu, muswada wa sheria hiyo na miswada mingine mingi muhimu ilipitishwa na Bunge kwa ushabiki wa kisiasa na kiitikadi, kwa maana ya hoja za wabunge wa upinzani kuzimwa au kujadiliwa kwa kejeli, vijembe na matusi na hatimaye kupuuzwa.
Ni katika muktadha huo, Sheria ya Fedha ya mwaka 2013 iliyoanzisha tozo ya kodi kwa laini za simu inapaswa kuangaliwa. Bunge kwa staili hiyohiyo ya ushabiki wa kisiasa na kiitikadi lilipitisha muswada wa sheria hiyo, huku wabunge wa upinzani wakipinga na kuainisha athari zake kwa wananchi na uchumi wa taifa. Ni kweli Rais alisaini muswada huo na kuwa sheria, lakini kutokana na athari zake kwa uchumi na wananchi kwa jumla, sasa ameirudisha bungeni kwa hati ya dharura akitaka ifanyiwe marekebisho na kuifuta kodi hiyo mara moja.
Ni aibu kwa Bunge, Serikali na Kamati ya Bajeti iliyobuni tozo hiyo kutoona mapema madhara ambayo yangesababishwa na kodi hiyo ya Sh1,000 (kwa kila laini ya simu kila mwezi) kwa wananchi maskini ambao wanahangaika kupata mlo mmoja kwa siku. Spika wa Bunge, Anne Makinda na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa kutojua hali halisi ilivyo, hasa vijijini walikaririwa bungeni wakitetea kwa nguvu hoja ya kuwekwa kwa tozo hiyo, wakidai kila mwananchi anao uwezo wa kuilipa kila mwezi.
Kutokana na utata uliosababishwa na tozo hiyo, kodi hiyo ilikuwa haijaanza kulipwa mpaka sasa, licha ya Bunge kupitisha muswada huo Julai, mwaka huu. Rais Kikwete baadaye aliingilia kati kwa kuagiza mamlaka zote husika kukutana mara moja kumaliza mvutano wa kodi hiyo kwa kutafuta vyanzo mbadala vya kodi ili kuziba pengo la Sh178 bilioni ambazo zingetokana na kodi kwenye laini za simu. Ni matarajio yetu kwamba Bunge letu litakuwa limepata somo la kutosha, hivyo litakuwa makini siku zijazo kwa kuhakikisha linapitisha miswada pasipo hila wala ushabiki wa kisiasa.
Serikali yahamisha kodi ya simu:


"Hata hivyo, kodi hiyo imerejeshwa kwa staili nyingine baada ya kuongezwa katika tozo la kodi ya manunuzi iliyokuwepo kutoka asilimia 14.5 ya awali hadi asilimia 17."


Dodoma.Serikali imeondoa kodi ya kadi za simu iliyopitishwa na wabunge katika Mkutano wa 13 wa Bunge ambayo ililalamikiwa na wadau na watumiaji wa simu nchini.
Hata hivyo, kodi hiyo imerejeshwa kwa staili nyingine baada ya kuongezwa katika tozo la kodi ya manunuzi iliyokuwepo kutoka asilimia 14.5 ya awali hadi asilimia 17.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salumu, bungeni jana wakati akisoma Muswada wa Sheria ya Manunuzi wa mwaka 2013, ambao uliingizwa bungeni kwa hati ya dharura.
Muswada huo ulipelekwa bungeni kwa hati ya dharura baada ya Rais Jakaya Kikwete kuridhia upitishwe na Bunge kabla ya kuwa sheria kutokana na malalamiko yaliyokuwa yametanda kila kona.
Katika muswada huo ambao ulichukua muda mfupi na kuchangiwa na wabunge wachache, Serikali imesema kuwa kilio cha Watanzania kilisikika na Serikali haikuona haja ya kuendelea na kodi hiyo, badala yake ikaamua kutafuta njia nyingine.
¡°Mheshimiwa Spika, Serikali imeamua kutafuta njia nyingine ya kukusanya mapato hayo ambayo yalilengwa kupatikana kwa zaidi ya Sh170 bilioni ambayo yangepelekwa katika huduma za umeme na maji, hata hivyo tumepata njia mbadala,¡± alisema Mkuya.
Alitaja njia hiyo ni kukusanya katika mitandao ya kimawasiliano yote ambayo awali hawakuwa wameilenga na kwamba kupitia njia hizo, wanaweza kupata kiasi cha Sh140 bilioni huku kiasi cha Sh30 zikitarajia kutolewa na kampuni za mawasiliano.
Katika maelezo yake, alisema kuwa kampuni za simu nchini yalikubali kutoa kiasi cha Sh30 bilioni ili kuisaidia Serikali katika kufidia pengo ambalo lingepatikana kwani tayari bajeti ilishapangwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Bunge, Andrew Chenge alisema kuwa Kamati ilikutana juzi mjini Dodoma kwa dharura na kukubaliana jinsi ya kurekebisha kodi na kutafuta njia nyingine ambayo ni kutoza kuongeza kodi katika manunuzi.
Kwa upande wake msemaji wa Kambi ya Upinzani kaika Wizara hiyo Christina Lissu, alilaumu mpango huo kwa madai kuwa hakuna kitu kilichoondolewa na badala yake kilichofanyika ni kiinimacho kwa Watanzania.


MCL
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom