Kleptomaniacs
Member
- Apr 23, 2008
- 86
- 2
Hii ni sehemu ya nukuu katika gazeti la Raia mwema toleo la wiki hii naomba tuitafakari
"Mwanasiasa mmoja mkongwe na ambaye amekwisha kushika nyadhifa mbalimbali za uwaziri, aliliambia Raia Mwema wiki hii kwamba, hali ya sasa isipodhibitiwa nchi itaingia katika hali ya machafuko ambayo hatujajiandaa kukabiliana nayo.
Sasa ukipita na gari zuri unaitwa fisadi na pole pole mafisadi watapigwa mawe, magari yao yatachomwa moto nyumba zitavamiwa na kuchomwa moto. Watakaofanya hayo watakuwa ni wananchi ambao hawana vigezo vya kujua nani ni fisadi na nani anatumia mali halali. Serikali, asasi zisizo za kiraia, viongozi wa dini, wazee na vyombo vya habari ni lazima tushirikiane kuhakikisha hayo hayatokei, alisema mwanasiasa huyo mstaafu".
Je hii ndio hofu kuu ya mafisadi? na sio maelfu ya watanzania wanaokufa kwa magonjwa yanayoweza kuzuilika,kutembea kwa miguu katika barabara mbivu vijijini,zahanati bila dawa,shule zisizokuwa na walimu nk kwasababu ya ufisadi wa wachache! Huyu mwanasiasa mkongwe anayetaka tusihoji na wananchi wasujue ukweli kwasababu wataanza kuwashughulikia mafisadi ajue kwamba moto ushawaka busara kubwa mafisadi wajitokeze watubu hadharani warudishe mali waliyokwiba wataishi kwa amani,lakini kinachofuatia wakiendeleza kiburi wananchi watakapoamua staili ya mapinduzi ya Kifaransa yaliyomwondoa Mfalme Louis tusilaumiane!