mgt software
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 13,767
- 7,115
Wana JF , umuofia kwenu.
Kumekuwa sintomfahamu katika sekta ya wizara ya afya baada ya wakazi wenye bifu zao na stress za maisha kuwageukia Manesi na kuwabambikia kesi nzito kiasi kwamba hawana pa kutokea kwani hawana watetezi wala wengi hawasikilizwi.
Imekuwa tabia sasa ya kuwaonea kila wakati, kuna uzembe mwingi unafanywa na wagonjwa wenyewe, mwingine unafanywa na serikali.
Mfano ngonjwa anaweza kuficha taarifa muhimu wakati wa kujifungua akapata shida. mgonjwa/mama kijacho anaweza kutengeneza kadi ya taarifa feki kutoka kwa mtu mwenye ufahamu wa mambo hayo, ambapo anaficha kuwa ana UKIMWI hivyo wakunga wakamzalisha kwa njia ya kawaida na mtoto akapata maambukizi, pia hata manesi wanapata maambukizi wakati wa kufua damu na vitu vyenye nchi kali vikimgusa. Wamama wengi wamekuwa na tabia mbaya sana, anapopima akagundulika ana UKIMWI anaweza kuanza matibabu au asianze, wengi kwa kutambua kuwa wenye ukimwi wanazaa, wanaenda kutafuta madume asije akafa bila kuacha watoto, kasumba hii imetokea sana kwa sasa, madada poa wengi wakijihisi wana ukimwi ujibebesha mimba na kuama maeneo au kuama mkoa, huko hutoa taarifa feki akijifanya mzima mpaka anajifungua. Mtoto anapozaliwa anapata maambukizi, mtoto akipata maambukizi hicho kituo cha afya kilichomzalisha wana kesi ya kujibu.
Manesi wengi walikuwa wakitukanwa ovyo na wagonjwa kiasi kamba anapandishwa hasira kwa kukosa uvumilivu na kuanza kujibizana. hii inatokea kwa serikali kukosa kupeleka vifaa kwa wakati, wananchi wanaambiwa dawa zipo, vifaa vya kujifungua vipo, wamama hawa wakienda wakavikosa, matusi kwa mane, wakikosa dawa matusi pia kwa manesi wakiambiwa wao ni wezi wakubwa wengine kutishiwa kuchapwa makofi hadharani...
Serikali chukueni hatua za kiuchunguzi kufuatilia mienendo ya manesi na wateja wao la sivyo atakuja kutokea maafa.makubwa kwani sasa hivi manesi hawaheshimiki ni watu wakunyanyaswa ovyo, daktari anamyanyasa nesi, mkuu wa mkoa ananyanyasa nesi, DED ananyanyasa Nesi. Chama chao cha kuwatetea masirai yao kimekuwa butu, hawana wa kuwasemea kwenye kazi zao, ni watu wa hofu muda wote.
Manesi ni watu wanafanya kazi mgumu na za hatari, magonjwa mbaya uwapata wakiwa kazini, lakini cha kushangaza ndio walio na masirahi kiduchu, angalau wakati wa awamu yanne walikumbukwa kidogo kwa kuongezea mishahara, sasa hivi baada ya serikali kutoa dawa bure wanafanya kazi ngumu wamezidiwa na wagonjwa wakati idadi yao ikiwa ndogo.