Hofu yatanda: Msanii Q-Chillah hajulikani alipo siku ya tatu sasa

Mkuu G kwa uliyo yaandika ni wazi kama yatakuwa yana uhusiano na Q basi ni wazi alipokuwa ana mahusiano na genge la wauza madawa na alipo acha walihisi anatoa siri zao au anataka kuwauza tena kupitia T.I.D ambaye alijitanabahisha kabisa anapinga hiyo biashara mbele ya Makonda na kumuunga mkono na kama hivyo basi wao ndio wanae na wanakula nae sahani moja pengine....
Kwenye swala la uwezekano wa kuchukua mali za watu wenye nguvu ya pesa na inawezekana ikawa ni sababu kama kuna ukweli huo......

Nashukuru kwa kunielewa Mkuu.
 
miaka ilee huyu jamaa alikuwa ustaz pale magomeni kabla ya ngoma yake ya NAMTAFUTA....Sasa leo anatafutwa yeye
 
Wasiojulikana.....wamempeleka kusikojulikana

Wasiojulikana ni kundi la watu(mafia) waliozuka /wanazuka Tanzania baada ya kukosa marupurupu, mali za magendo, walikuwa wamezoea kula bila kinawa mikono( kama waligawa Airtel, Mlimani City) na kujitajirisha na sasa wamekosa nafasi kama hizo, wanafanya maasi ili raia wa kawaida na waliowaadilifu wachukie serikali ya Dr Rais Magufuli lakini yote haya yatafichuka tu.
 
Wasiojulikana kama ni kweli tunalijengea taifa picha mbaya sana ya kiulinzi na usalama.

Kama watu maarufu au wanaofahamika wanapotea kwa kiasi hiki je hao wasiokua na jina ama hawafahamiki ni wengi kiasi gani?

Jeshi la polisi na inteligence community tupeni majibu ya masahibu haya wanayopitia watanzania wenzetu
Acha kuropoka,hivi hata mkitekana kuhusiana na unga walaumiwe polisi?
 
Acha kuropoka,hivi hata mkitekana kuhusiana na unga walaumiwe polisi?

Mbona unaongea kama Pimbi. Kuuza unga inaruhusiwa? Ina maana hata wewe ni mmojawapo ndio maana hata unajua waliomteka.
Ama unafahamu alipo maana kama ni genge la madawa limemteka wewe unafahamu.


Kwanini usitoe taarifa rasmi kwa mamlaka au kwa ndugu zake.
 
Huyu atakua amekula vitu vyake kasizi tu mahali hadi vitapopungua kichwan atarud tu
 
Back
Top Bottom