Hofu yatanda: Msanii Q-Chillah hajulikani alipo siku ya tatu sasa

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,206
42,068
Wasalaam wana jamvi....

Msanii Q-Chillah toka juzi hajulikani alipo na watu wakaribu yake wameshindwa kumpata hadi sasa si kwenye simu au uso kwa uso na hawana taarifa yeyote popote alipo.

Taarifa za kupotea Kwa Q-chief zimeripotiwa jana na msanii mwenzie T.I.D kupitia E-fm radio akitaka kuujuza Umma au yeyote mwenye taarifa ya alipo Q-chief awajuze maana wana hangaika kumtafuta hadi sasa wameshindwa kumpata.

T.I.D anasema yeye mara ya mwisho waliahidiana na Q-chief wakutane sehemu fulani lakini baadae alimpigia kumwambia atapita sehemu fulani mara moja hivyo watakutana baadae , Hivyo T.I.D alibidi amsubiri pale lakini muda ulipita bila Chillah kutokea hivyo kuanza kumtafuta hewani lakini hakupatikana na hivyo akamtafuta mchumba wake lakini mchumba wa q-chillah alisema na yeye hampati hewani hivyo wakaanza kumtafuta bila mafanikio jana ilikuwa ni siku ya pili wameshindwa kumpata na hawajui alipo.

Mchumba wa Q-chilllah alisikikia kupitia radio E-Fm kuwa alibidi apige simu pale aliposema atapita kabla ya kukutana na T.I.D alijibiwa kuwa Q-chillah alichukuliwa na gari fulani hivyo wao hawajui amekwenda wapi na hawana mawasiliano nae tena...

T.I.D anasema ameshatoa taarifa polisi toka jana lakini ameona awajuzi watanzania ili kama kuna mtu anajua Q-chief alipo asaidie kutoa taarifa hata kituo cha polisi ili awezeshe kupatikana kwakwe...

Bado najiuliza
Hivi Q-chief atakuwa amedhurumu?
Hivi Q-chief atakuwa amekula vya watu?
Hivi Q-chief atakuwa amejificha kutafuta kiki?
Hivi Q-chief anapenda ugomvi au ana ugomvi na mtu?
Hivi Q-Chief atakuwa na tabia ya ulevi wa kupindukia?
Hivi Q-chief aatakuwa anafanya biashara ambayo watu wake wa karibu hawafahamu?

Hayo ni maswali tuu nimejiuliza lakini binafsi namuona Q-chief kama mtu mpole na humble sana..
Tuombe Mungu ndugu yetu apatikane akiwa salama.

Wasalaam wana jamvi.

Source: E-fm (ubaoni)
 
Wasiojulikana kama ni kweli tunalijengea taifa picha mbaya sana ya kiulinzi na usalama.

Kama watu maarufu au wanaofahamika wanapotea kwa kiasi hiki je hao wasiokua na jina ama hawafahamiki ni wengi kiasi gani?

Jeshi la polisi na inteligence community tupeni majibu ya masahibu haya wanayopitia watanzania wenzetu
 
Huyu mara ya mwisho majuzi tu hapa iliripotiwa kakamatwa na polisi huko dodoma akiwa na chid benz..

Walipigwa mkono na polisi,hawakusimama polisi wakawakimbiza ,katika hali ya mwendo kasi q chillah akagonga nguzo, polisi wakawakamata na kukuwa wapo na madawa ya kulevya kwenye gari..

Sasa kapoteaje tena.??
 
Kuna Mzee mmoja hivi Umri umeshaenda siku moja aliwahi kuniambia kwamba ukishaamua kuingia katika Biashara na Matumizi ya dawa za Kulevya basi jaribu kuwa makini na usipende kupayukapayuka au kutumika na Rafiki yako ama kwa kujua au kutokujua katika kuwafichua wenzako kamwe hutobaki salama. Lakini kama haitoshi pia ukijua una mahusiano ya Kimapenzi tena ya uwizi na Mpenzi wa Mtu kisha akakuonya mara mbili tatu bila ya hata Kukudhuru jua ya kwamba kinachokuja si kitu kizuri na huenda Kikakugharimu.

Mpaka leo nayawaza mno hayo maneno ya huyo Mzee na sijayapatia bado majawabu kuwa alikuwa akimaanisha nini hasa.
 
Qchillah hakua nae
 
Aiseeeee.................
 
Back
Top Bottom