Hofu yangu ndani ya fikra za kijinga karibu tutafakari kwa pamoja

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
Kila nabii na zama zake na kila jambo lina mwanzo na mwisho zaidi hakuna marefu yasiyo kuwa na ncha ndivyo wahenga wanasema hivyo tangu kuwepo kwa dunia wamepita watu mbali mbali walioacha alama kwa kufanya mambo ambayo yanakumbukwa mpaka hii leo lakini pamoja na uimara waliopata kuwa nao kuna nyakati ambazo walipitia magumu ambayo yalifanya wakaanguka na kuufikia mwisho wao na zama zao zikabaki kuwa historia za kupendeza na kusisimua katika kuzisoma au kuzikiliza waliyo yafanya.

Nikiwa mwenye woga na hofu kubwa nikiufikiria mchezo pendwa duniani namna unavyo badilika na kuibuka kwa walimu vijana na mbinu za kisasa zaidi huku kupotea kwa walimu mahiri wa miaka kadhaa nyuma wakipotezwa na makocha wa kisasa nazidi kuogopa zaidi nikimfikiria mvaa suruali za kubana(pep) katika siku zijazo

Hofu yangu ni kwamba Pep anaenda kufa kifo cha mourinho! Kutokukubali kubadilika kimbinu na kimfumo kuendana na mahitaji ya mechi husika na michuani husika.

Hivi sasa Pep ata asajili nani, bado hawezi kuwa na jipya uwanjani, sababu watu alionao wanatekeleza zaidi ya asilimia 90 ya maagizo yake, hakuna mchezaji atakuja afanye maajabu ya ziada, labda amsajili Messi ambae anaweza akafanya maajabu kwa miguu yake na uwezo binafsi ila sio wa kocha.

Ikiwa kama kocha ilani yako inatekelezwa kwa asilimia zaidi ya 90 na bado hufiki mbali, ukiwa na wachezaji wenye uwezo wa kutekeleza ilani yako karibu kikosi kizima na sub zote, ikiwa umewasajili wewe woteeee, ni wazi sasa tunauona uwezo wa mwisho kabisa wa Pep.

Soka linabadilika sana kila baada ya misimu miwili adi mitatu, Mourinho aliepaki bus akiwa na Inter milan anamfunga Van gaal na bayern yake ya mpira mwingi alionekana lulu duniani, akaenda Madrid, akawapa makombe, Chelsea akawapa kikombe.

Lakini ni Mou huyu huyu na staili yake ile ile alitaka kuwashusha daraja Chelsea, alifukuzwa madrid, kafukuzwa Utd, na sasa Spurs inachechemea chini yake, ni kwamba soka lake limepitwa na wakati na wachezaji wengi hawaamini tena falsafa yake ya mpira na menejimenti yake.

Pep alietamba na Barca, akaenda kutawala sana Ujerumani, hivi sasa nae nati zimeanza kuachia reli taratibu, ni wazi mpira wa pasi nyingi na tiki-taka sasa nao unafikia mwisho, iangalie Barca inavyokamatwa na tikitaka yake, iangalie Spain ilivyopotea hivi sasa, iangalie Man city inavyokua ya kawaida kila msimu.

Wazungu wanasema, signs could mislead, words can lie, actions can play you, but PATTERNS never lie, nor mislead or play you neither.
Tuangalieni hii pattern ya mpira wa Guardiola, Moja kati ya sababu kuu ya Van gaal kushindwa na aina yake ya mpira dakika za wachezaji walikua wakilalamimika "too much details" kwenye mbinu zake, mpaka vichwa vinapata ganzi kuelewa kila kitu katika mfumo.

Hii inatokea ata kwa Pep, wachezaji wanasema moja ya characteristic ya Pep ni maelezo mengi mno katika mbinu zake uwanjani na mazoezini.

Mbinu hizi zinafeli na zitazidi kufeli sababu wachezaji wa sasa wanazaliwa wakiwa na uwezo mchache tu wa kufikiri uwanjani na haswa hucheza kwa sababu wana vipaji vya kujua kucheza mpira na miundombinu mizuri ya kuonyesha vipaji vyao, dunia ya sasa haizalishi football geniuses kama zamani.

Hii leo barca best talent ya la masia iliopo juu ni Ansu Fati, Best touted player for ballon d'or ni Kylian Mbappe, talent nyingine utakuja kwa Jadon Sancho, hawa ndo wachezaji wenye vipaji kwa sasa duniani, wana vipaji ila u-genius hakuna, ni vipaji tu.

Tukumbuke kuna kipindi Pep alifundisha Messi, Iniesta na Xavi timu moja, hivi ni vipaji na ni genius ndani yake.

Kwaiyo Pep anahitaji genius kwenye timu yake angalau watatu ili data zake zote ziweze kuwa information na kutekelezwa uwanjani na kupata matokeo, kitu ambacho dunia ya sasa haizalishi tena, akipatikana angalau angalau atagombewa na kila mmoja duniani.
Zamani ulikua na uwezo wa kumuona Xavi akiwa Barca, Modric madrid, Pirlo Juve, Scholes Utd.

Hivi sasa kukiwa na angalau kwenye timu moja, timu zingine hazina ata uyo angalau.

Ni kama Mwalimu alivoona amezidiwa na hali ya ubepari na kuamua kuachia ngazi ili kulinda heshima yake ya kusimamia ujamaa, ndivyo Mourinho na sasa Pep nao wataenda kupotea.
 
Sasa mkuu kama hiyo ni hofu yako katika ujinga, ukitumia akili je!

Umejua kujifagilia

By the way, we reached the peak and now we go down in every aspect
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom