Hofu ya X-MAS bila pesa: Lini Serikali itawalipa watumishi mishahara itakayowafikisha tarehe 30/31? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hofu ya X-MAS bila pesa: Lini Serikali itawalipa watumishi mishahara itakayowafikisha tarehe 30/31?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DT125, Dec 22, 2011.

 1. D

  DT125 JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2011
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 203
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Leo nilipita kijiwe kimoja nikakuta mjadala mkubwa juu ya kuwepo uwezekano wa watumishi wa serikali kutolipwa mishahara kabla ya sikukuu ya krismasi. Mara Payroll bado, mara hata wanajeshi bado. Mara Mafuriko lazima yawakwamishe mishahara. Lini watumishi wa Serikali watalipwa mishahara ya kuwafikisha tarehe 30/31. Mkulo unasemaje?.
   
 2. R

  RMA JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2011
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maisha bora kwa kila mtanzania! Kuweni wavumilivu ndugu zangu msilalamike! Hiyo serikali mliichagua wenyewe baada ya kupewa vikofia vya kijani na chumvi. Mkapiga kura kama vipofu na sasa mnalalama kama vichaa! Hakuna cha Krismasi wala ndugu yake - mwaka mpya! Kila mtu ajijue, hadi mtakapopata akili ya kuondoa ushabiki wa Yanga na Simba katika siasa! CCM hoyee!
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,542
  Likes Received: 81,975
  Trophy Points: 280
  ...Serikali imeshawakopa WARIE TU!!!! kama hawakuambulia kitu kesho ndio imekula kwao.
   
 4. CHEMPO

  CHEMPO JF-Expert Member

  #4
  Dec 23, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Serkali ya sherehe na mambo yasiyo na tija..hongera ccm kwa kutuongoza kwenye uchumi imara wenye kupaa
   
 5. B

  Baba Collins JF-Expert Member

  #5
  Dec 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 498
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Uchumi unakua kwa kasi ya mbayuwayu!
   
 6. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #6
  Dec 23, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Hii thread ni ya kichochezi na ina lenga kupandikiza chuki kwa serikali.mimi ni mwalim niko iringa nimeshapokea mshahara wangu na tayari nimeshafanya shopping kwa ajili ya X-MASS.kama wewe ni mtumishi wa serikali nenda benk achana na wazushi wa JF.
   
 7. t

  tisa desemba JF-Expert Member

  #7
  Dec 23, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 439
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  poleni, ila baadhi yetu serikalini tushalamba salary jana (dec 22)...! myself nilishangaa coz toka niajiriwe sept 2009. hii ndio kwa mara ya kwanza kupata salary mapema zaidi.
   
 8. M

  Mchomamoto Senior Member

  #8
  Dec 23, 2011
  Joined: Aug 19, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Acha uzushi mishahara kama mmepata ni wachache, watumishi wengi bado hawajapata.Baba Rizi bingwa wa mafisadi kamua twende babaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 9. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #9
  Dec 23, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Ulitegemea kukutana na story gani Kijiweni? watu ni wa kijiweni hata hiyo Payroll huwa wanaisikia tu kwa wafanyakazi, kazi kusema tu mambo ya watu.. miaka nenda rudi weapo Vijiweni....Tutolee habari za Kijuweni hapa!!
   
 10. N

  Ndamalishaz Member

  #10
  Dec 23, 2011
  Joined: Dec 11, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii serikal ni ya wachache jamen kwa hamlijui hloooo,,?kuna maajabu bado yatakuja mbna w stil ve a long way
   
 11. TASLIMU

  TASLIMU Senior Member

  #11
  Dec 23, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha kuzingua wewe mi mwenyewe n mtumishi wa serikal pesa mpaka sasa bado,nmb mobile inasoma zro,huo ndo ukweli,co ckuu ya kwanza,nipo kigoma
   
 12. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #12
  Dec 23, 2011
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Wewe ndo wale wale magamba wengine wanalia nyie mnachekelea
   
 13. t

  tisa desemba JF-Expert Member

  #13
  Dec 23, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 439
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  nitonye, plz plz nitake radhi, huwezi nifananisha na hao magamba! ndio maana nikatangulia kwa kutoa pole kwa wale ambao hawajapata ili kuonyesha masikitiko yangu.
   
 14. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #14
  Dec 23, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,857
  Likes Received: 4,533
  Trophy Points: 280
  Mkuu kijiwe sio lazima kiwe kama unavyokifikiria wewe!! Hapo kijiwe imetumikia kuelezea sehemu ambayo watu wanakaa na kujadiliana mambo. Hivyo inawezekana kabisa hicho kijiwe alichopita mtoa mada kilikua cha watu wenye kuelewa payroll ni nini!!
   
 15. R

  RUKAKA Senior Member

  #15
  Dec 23, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 100
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mishahara ni kwa awamu jamani msikonde. Kuna waliopata na wengine Bado. labda wakurugenzi wenu wanachakachua make wengine toka tarehe 20 na sasa zimeisha kabla hata ya X'mas yenyewe. Tuombe iongezwe make ni kiduchu kama posho za mjengoni wamesitisha hilo fungu wawape watumishi wa serikali ili waweze kufikia mshahara mwingine wakiwa bado na kiasi kidogo mfukoni.
   
 16. D

  DT125 JF-Expert Member

  #16
  Dec 23, 2011
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 203
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Kumbe wafanyakazi wa serikali hawana tofauti na kufanya kazi kwa Mhindi akiwalipa 5 wengine 5 mnasubiri akusanye kwanza mauzo ya wiki. Iringa wamelipwa Kigoma bado! au Kigoma sababu CCM wabunge 3 tu kati ya 8 mkoa mzima.
   
 17. h

  hans79 JF-Expert Member

  #17
  Dec 23, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  wakati wa uchaguzi(2015).
   
Loading...