Hofu ya Upinzani ni CCM kuwa imara tena chini ya Mzalendo Mwenyekiti Magufuli

Kawe Alumni

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
8,685
11,988
Hizi hasira za upinzani za kuhisi wanaonewa ni hofu inayowaumiza kisaikolojia juu ya kupuuzwa na Watanzania

Kabla ya Rais Magufuli,Wanaccm walikuwa wanaona aibu kuvaa nguo za chama,na kuna Sehemu walikuwa wakitupiwa makopo wakikatiza mtaani

Wanaccm walificha sare zao ndani kutokana na masuala ya ufisadi kukithiri, kutokana na huduma za kijamii kudhorota

Lakini Upepo ulibadilika ghafla baada ya 2015
Mwenyekiti wa ccm akairudisha Ccm kwenye makali yak,Wananchi wakaanza kurudisha amani na CCM,wakaanza kuwapuuza wale wanaopinga serkali

Wananchi Wengi wamekimbia upinzani kimya kimya wamerudi CCM kutokana na kishindo cha awamu ya tano

Saaa nguo za chama zimetamalaki mtaani,kila mwananchi anajivunia kuwa CCM

Ukweli mchungu ni kwamba wapinzani wanaogopa sana CCM iliyotulia ,wanajua Ccm iliyotulia ni hawana chao

Ukiangalia hata wapinzani kushinda ubunge ilitokana na kukorogeka kwa ccm kulikopelekea kugawanya kura

Ccm iliyotulia,upinzani utaambulia viti vitatu tu vya Ubungo

Hata hii janja janja inayoendelea ya kususia Uchaguzi hisia zangu zinanituma tu hawa jamaa wamepima kina cha maji wakaona hapana hapa tutaaibika
Ndio mambo ya kubeba mpira kwapani yakaja



Tuendelee kumuunga mkono mh Rais katika juhudi zake za kuleta Maendeleo
 
Mimi naona wapinzani wakubali tu uhalisia

Waache kupingana na ukweli

Wananchi wanajionea maendeleo kuna haja gani kuendelea kupinga?
 
Polisi wanapata faida gani kukisaidia chama kushinda chaguzi huku polisi hao hao wakivihujumu vyama vya upinzani?
 
Walijua Mr.white hair ni mwenzao
Upinzani walitumia vibaya 'silver bullet' 2015, kipindi ambacho CCM ilikuwa imegonga rock bottom ya political unpopularity..wakabadili gia kumchomoa Dr na kumuweka Edward..Baada ya hapo kilichofuata ITV ni "Vihoja Majukwaani"
 
Mkapa kauthibitishia umma kuwa CCM walikwapua na kuibunya hela ya EPA, wote waliobuni na kutekeleza uporaji huu wako huko CCM tena viti vya mbele.
 
Kama Chama kiko imara kulikuwa na haja gani
1. kuzuia vyama vingine visifanye siasa baada ya uchaguzi mkuu. Wakati chama kinafanya siasa nchini nzima.

2. kuwatisha watendaji wa serikali wanaosimamia chaguzi kuwa akishinda mpinzani basi nae kapoteza kazi.

3. Kuzuia shughuli za bunge kuoneshwa mubashara mwanzo mwisho.

4. Kuwahujumu viongozi wa upinzani na kuwabambika kesi zisizoisha mahakani

5. Kuingilia mikutano ya upinzani ya kampeni na ya kisiasa kwa nguvu ya polisi badala ya kuipatia ulinzi.

6. Kurubuni wachaguliwa wa upinzani wajitoe kwenye vyama vyao kuwa wakija kwenye chama tawala watarudishiwa nyadhifa walizokuwa nazo.

7. Kuwakebehi viongozi na wachaguliwa wa upinzani katika mikutano ya hadhara ya kiserikali.

8. Kuhujumu michakato ya uchaguzi ndogo na kubwa.

9. Kutumia nguvu ya polisi kukwamisha shughuli za siasa za upinzani.


Hii maanake ni kuwa, katika hali usawa ya kisiasa bado chama tawala hakina uwezo wa kushindana na upinzani.

Tumshukuru tu Mungu wanachini wamekubali kuwa kuwa kama kondoo wa sadaka. Lakini kitakuja kizazi kingine ambacho hakiwaweza kuvumilia haya yote na kutakuwa na mwisho mbaya.
........................................
Chama kijipime kukubalika kwake katika mazingira sawa ya kisiasa na sio mazingira kandimizi na ya kibabe wa wapinzani wako halafu unasema eti chama kimeimarika.

....Ujinga mtupu...
 
Kapimwe akili wewe ngumbangu😁 😁 😁 kuogopa sanduku la kura kiasi cha watendaji kuwaengua wapinzani kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa ni ushahidi tosha kwamba hata wananchi tunawaogopesha kwamba tumewachoka
 
Mleta mada una miaka mingapi? kama uko above 30 na bado ufahamu, akili na uelewa hujapata basi ndio imetoka! Uzee wako utakuwa wa vituko na utajikuta jamii ikuita KUBWA JINGA.
 
Mtu aliyeishiwa hoja hukimbilia kwenye matusi Mkuu

Haya rudi mezani tujadili Mkuu
Mleta mada una miaka mingapi? kama uko above 30 na bado ufahamu, akili na uelewa hujapata basi ndio imetoka! Uzee wako utakuwa wa vituko na utajikuta jamii ikuita KUBWA JINGA.
 
Back
Top Bottom