Hofu ya Ukimwi na Tatizo la upungufu wa Nguvu za Kiume! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hofu ya Ukimwi na Tatizo la upungufu wa Nguvu za Kiume!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by ndyoko, Dec 3, 2011.

 1. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #1
  Dec 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Kwa wanaojua suala la 'sick building syndrome' watakubaliana nami kwamba mtu unaweza ukawa mgonjwa ili hali si mgonjwa. Kwamba baadhi ya vitu unavyoishi navyo ndani ya nyumba au nje vikawa vinakufanya muda mwingi ujisikie mgonjwa wakati kiuhalisia sio mgonjwa.

  Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume ni kubwa sana kwa sasa na limekuwa likiongelewa sana kuanzia miaka ya 80. Hiki ni kipindi ndich ugonjwa wa ukimwi ulipoanza 'kuvuta kasi' ktk jamii yetu ya kitanzania na duniani kwa ujumla. Binafsi nadhani kuna sababu nyingine ambazo hazijafanyiwa utafiti ambazo nazo zinaweza kuwa zinachangia hili tatizo.

  Hebu fikiria, ktk elimu dunia kijana anaambiwa ukimwi hauna tiba na kwamba condom sio salama 100% kama kinga ya ukimwi. Ukienda kanisani/msikitini unaambiwa usitumie 'condom' kwa kuwa ni dhambi. Hapo tayari mtu anakuwa na 'moral and mental conflicts'. Mbaya zaidi, mtu pengine ktk kufanya hiyo ngono anakuwa anamsaliti mkewe-hiyo ni conflict nyingine. Hebu tujiulize, hatuoni mtu anapokuwa ktk mazingira haya, hvi hakuna uwezekano wa 'sex performance' yake kupungua? Hivi mtu ambaye ameshamsaliti mkewe anarudi nyumbani na mawazo yale ya kidini na kidunia-kwamba condom is not 100% preventive to AIDS na kwamba ametenda kinyume na mapenzi ya Mungu-kumbuka lile tangazo la mwanaume anayemuangalia kwa huzuni mkewe aliyekuwa anampigia pasi nguo zake. Hivi ktk mazingira kama yale, hata kwa mkeo unaweza kweli ukaenda raound zaidi ya moja kwa jinsi ulivyo na msongo wa mawazo kichwani?

  Nadhani kuna haja ya watafiti wakaliangalia hili. Najua kina Dr. Riwa, hii maneno kama haijafanyika ni vyema mkaiangalia. Kuna haja ya kufanya kitu kama hakijafanyika. Binafsi naona hili linaweza likawa tatizo lingine la 'sick building syndrome' linalochangia upungufu wa nguvu za kiume.

  Mjadala uko wazi kwa 'critics'!
   
Loading...