Hofu ya ugaidi: Ibada ya mkesha wa pasaka kuanza saa 11 jioni!; | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hofu ya ugaidi: Ibada ya mkesha wa pasaka kuanza saa 11 jioni!;

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by YAGHAMBA, Mar 25, 2013.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. YAGHAMBA

  YAGHAMBA JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2013
  Joined: Aug 8, 2012
  Messages: 538
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ndugu wanajamvi, salamu.

  Kutetereka kwa hali ya amani ya nchi yetu Tanzania kunakotokana na tetesi za uwepo wa vikundi vya kigaidi vya siasa kali za kiislamu vinavyodaiwa kupanga kufanya mashambulizi kwenye makanisa mbalimbali wakati wa sikukuu ya pasaka, makanisa mbalimbali yamewatangazia waumini wao watakaohudhuria misa ya mkesha wa pasaka kuwa misa hizo zitaanza kati ya saa 11 jioni na saa 1 badala ya saa 3 usiku kama ilivyozoeleka miaka yote.

  Kanisa katoliki jimbo kuu la Mwanza kupitia mahubiri ya jana jumapili limewaelekeza waumini wake walioko kwenye vigango kuanza misa saa 11 na wale wanaosali parokiani kuanza misa saa 12 ili kufikia saa 3 usiku shughuli ya ibada iwe imekamilka. Pia waumini wametakiwa kuchukua tahadhari kwa kitu au mtu yeyote wanayemtilia mashaka.

  Vilevile waumini wa kikristo wametakiwa kufunga kwa siku saba na kuliombea taifa na kwamba silaha pekee ya mkristo awapo kwenye nyakati ngumu za mateso ya kiimani ni kufunga na maombi.MY TAKE; Serikali ya CCM inajisikiaje kwa haya yanayoendelea nchini?, nauliza hivyo kwa kutambua kuwa mbegu hizi za udini na ukabila zimepandwa na wanasiasa wake huku serikali hiyohiyo ikitoa vibali kwa wahubiri wa dini moja kuzunguka nchi nzima kueneza chuki dhidi ya ukristo na baba wa taifa Mwl.

  Nyerere huku wakikishambulia chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA. Nasema wahubiri hao walipewa kibali kwasababu polisi walikuwa wakilinda mihadhara iliyokuwa ikifanyika viwanja na kumbi za wazi. Miongoni mwa kauli zilizokuwa zikitolewa katika mihadhara hiyo ni hii; " KUFA KUPONA TUTAHAKIKISHA UKATOLIKI UNANG'OKA MIZIZI YAKE TANZANIA".

  Ebu fikiria kauli kama hiyo inatolewa mbele ya polisi na usalama wa taifa ndani ukumbi wa Diamond Jubilee halafu watu hao wanaendelea kuzunguka mikoa mingine kueneza hayohayo, serikali haichukui hatua, maana yake ni kuwa tutaamini viongozi wakuu wa chama na serikali inayotawala wapo nyuma mpango wa wahubiri hao na wana baraka zote za mkuu wa nchi na vyombo vya ulinzi na usalama vina taarifa ya kutokuwachukulia hatua zozote wahusika.

  Leo tumefika hapa kwa mbegu hizi zilizopandwa chini ya usimamizi wa watawala, na huenda hali ikawa mbaya zaidi kwani watawala hawaonekani kuchukua hatua stahili ingawa ni kweli kuwa hawawezi kuchukua hatua stahili kwa jambo waliloliunda kwa maslahi ambayo mpaka sasa nashindwa kuyatambua.

  WITO; CCM na serikali chini ya Jakaya Kikwete, hili jambo mmeliasisi wenyewe kwa malengo mnayoyajua, mlitatue na mlimalize ili nchi yetu ibaki salama. Mungu ibariki Tanzania.
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2013
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,109
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 160
  Jimamosi kuu huku kwetu hatusali usiku, tunasali jioni na misa iishe kabla jua halijazama kwa hofu
   
 3. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2013
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,109
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 160
  Andika kwa paragraph basi
   
 4. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2013
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,646
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  What kind of god is this?
   
 5. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2013
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Huko Zanzibar hali ni aje kwa wanaofahamu?
   
 6. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2013
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,896
  Likes Received: 741
  Trophy Points: 280
  Wasiwe na hofu mtuhumiwa wa ugaidi nchini ambaye ni kiongozi wa CHADEMA bwana LWAKATARE bado yupo kizuizini.
   
 7. kashesho

  kashesho JF-Expert Member

  #7
  Mar 25, 2013
  Joined: Oct 19, 2012
  Messages: 4,742
  Likes Received: 958
  Trophy Points: 280
  kwetu misa ipo kama kawaida vijilia ya pasaka ni saa tatu usiku
   
 8. A

  Alfu Lela Ulela JF-Expert Member

  #8
  Mar 25, 2013
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwanini vitendo vya kigaidi vije wakati wa Pasaka na sio wakati wa Idd au mwezi mtukufu?
   
 9. bushman

  bushman JF-Expert Member

  #9
  Mar 25, 2013
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Tutaanza ibada mapema saa moja jioni hatuvai bullet proof silaha yetu ni maombi na sala na wiki hii tumeingia katika maombi juu ya amani ya taifa hili,mungu wetu wa amani atatenda muujiza soon.
   
 10. A

  Atongwele JF-Expert Member

  #10
  Mar 25, 2013
  Joined: Feb 22, 2013
  Messages: 2,471
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kuna watu hiyo hofu wanaitengeneza kwa maslahi yao binafsi. walianza na kusema kuwa serikali inawapendelea waislam, baadaye wakazusha kuwa kuna waislam wametoka somalia kuwadhuru wakristo siku ya pasaka. hawa watu wajinga mno
   
 11. A

  Atongwele JF-Expert Member

  #11
  Mar 25, 2013
  Joined: Feb 22, 2013
  Messages: 2,471
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  halafu nasikia kuna wale magaidi wa CHADEMA wanataka kufanya mambo ili kuneutralize issue ya lwakatare. pamekaaje hapo?
   
 12. A

  Atongwele JF-Expert Member

  #12
  Mar 25, 2013
  Joined: Feb 22, 2013
  Messages: 2,471
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  watu wachoyo naona wameanza kutuingilia watanzania ili tusishirikiane. walianza kuja na hoja ya wakristo wawe na mabucha yao na wajichinjie kitoweo, walivyoshambuliwa wamekuja na hoja ya ugaidi ili waislam na wakristo wasishirikiane kusherehekea pasaka. pumbavu. mbona miaka yote tulikuwa watulivu?
   
 13. Lizaboni

  Lizaboni JF-Expert Member

  #13
  Mar 25, 2013
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 33,793
  Likes Received: 13,787
  Trophy Points: 280
  umeongea kama nani mkuu, msemaji wa kanisa katoliki? watu kama wewe ni hatari sana unachokipinga humu ndicho unakiendeleza. Hivi hapa unachokiendeleza siyo udini kweli?
   
 14. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #14
  Mar 25, 2013
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,434
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Ipo siku tutasitisha "KUCHAMBA KWA MARA TANO KWA SIKU" Hii ni kwasababu kitendo cha kutusakama sisi Wakristo bila sababu itafika muda tutasahau huruma yetu na tutaiweka kando ROHO YA KUVUMILIA nasi TUTAAMUA LIWALO NA LIWE. Haiwezekani ibada yetu kuvunjwa na kupangwa muda usio just kwasababu ya KUWABEBA MAGAIDI HAWA.

   
 15. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #15
  Mar 25, 2013
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 359
  Trophy Points: 180
  mimi huwa sina shida na mch msigwa ila huwa ninashida na uelewa wake kama mtakumbuka aliwahi kushilikishwa kuamua kesi ndani ya chadema iliyohusu mahusiano ya kimapenzi baina ya wenje na rose kamili lakini alivyoiamua huwezi amini.
   
 16. A

  Atongwele JF-Expert Member

  #16
  Mar 25, 2013
  Joined: Feb 22, 2013
  Messages: 2,471
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  au ndiyo wameanza kuwaandaa waumini ili wamuondoe kikwete madarakani?
   
 17. A

  Atongwele JF-Expert Member

  #17
  Mar 25, 2013
  Joined: Feb 22, 2013
  Messages: 2,471
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mkuu, magaidi ni LWAKATARE na LUDOVICK. Wote ni wakristo
   
 18. YAGHAMBA

  YAGHAMBA JF-Expert Member

  #18
  Mar 25, 2013
  Joined: Aug 8, 2012
  Messages: 538
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nasiktika unaleta mzaha kwenye mambo muhimu, ebu niambie-Je Lwakatare ndiye alikuwa anafanya mihadhara ya kukashifu na kuutukana ukristo hususan wakatoliki na kumzulia uongo marehemu baba wa taifa Mwl. Nyerere?, je ni Lwakatre aliyezunguka nchi nzima, mkoa kwa mkoa, wilaya kwa wilaya, msikiti kwa msikiti kueneza chuki kwa waislamu kuwachukia wakristo?. Naamini wale wahadhiri walikuwa na baraka zote za mkuu wa nchi kwa malengo ambayo ipo siku tunapaswa kuyafahamu kutoka kwake, hata hivyo na wewe unayejiita Tume ya katiba naamini ni mmoja wanaotumiwa na haohao waliowatumia hao wahubiri waeneza chuki. kwenye mabo ya msingi acha kutumiwa , kaa kimya kama hauna la kuchangia, vinginevyo washauri hao wanaowatumia warekebishe hii hali waliyoiunda na kuilea.
   
 19. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #19
  Mar 25, 2013
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Wewe ni mpuuzi kweli na hauna maana kabisa.
  Ni kweli hata sisi tutaanza Misa saa 2 usiku. Tunaomba tu Mungu atuepushe
   
 20. YAGHAMBA

  YAGHAMBA JF-Expert Member

  #20
  Mar 25, 2013
  Joined: Aug 8, 2012
  Messages: 538
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Tuombe na kufunga kuliombea taifa letu, hata ambao si wakristo wafanye hivyo.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...