Hofu ya serikali ya CCM Kilimanjaro yazuia graduation Majengo Sec School | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hofu ya serikali ya CCM Kilimanjaro yazuia graduation Majengo Sec School

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by dm2000inter, Oct 27, 2010.

 1. d

  dm2000inter Member

  #1
  Oct 27, 2010
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 29
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Ama kweli CHADEMA imeishika pabaya CCM. Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Moshi mjini,Bernadette Kinabo leo amepiga marufuku sherehe za mahafali ya sekondari ya Majengo inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Moshi kwa sababu itaipa ujiko Chadema. Taarifa za maofisa usalama zinadai mkuu wa shule hiyo aliitwa leo saa 3:00 asubuhi na Kinabo na kuambiwa afute Graduation hiyo iliyokuwa ifanyike Jumamosi ya Tarehe 30.10.2010 hadi uchaguzi utakapomalizika. Inaelezwa kuwa mkuu wa shule hiyo alielezwa wazi kuwa maagizo hayo ni maelekezo toka ngazi za juu. Taarifa ni kwamba Academic Master wa shule hiyo, Pantaleo Minja anagombea Udiwani kata ya Majengo kwa tiketi ya Chadema na ndiye anayepewa nafasi kubwa ya kushinda. Shule hiyo ina wanafunzi zaidi ya 2,800 na wanafunzi 1,600 wamejiandikisha kupiga kura katika daftari la kudumu la wapiga kura. Uamuzi huu wa serikali umechochea hasira ya wazazi na wanafunzi kwa kuwa baadhi ya wazazi walishakodisha kumbi kwa ajili ya kuwapongeza watoto wao, kutoa order za cake na kadha wa kadha. Swali la kujiuliza ni je Uamuzi huu wa msimamizi umekisaidia CCM au ndio umekimaliza zaidi kisiasa?Jibu unalo kwa kichwa....:sad:
   
 2. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Wazazi, wanafunzi, vote ccm out!
   
 3. R

  Rugemeleza Verified User

  #3
  Oct 27, 2010
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Msimamizi wa Uchaguzi hana mamlaka hayo kila shule ina haki ya kufanya sherehe zake na kwa kuwa siku hiyo ni sahihi. Ingekuwa kama sherehe imegeuzwa kuwa mkutano wa kampeni hapo sawa. Hivyo huyo Mkuu wa Shule anaweza kupuuza hayo mawazo ya huyo Mkurugenzi.
   
 4. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  uchaguzi hauna maana ya kusimamisha kila kitu, waacheni watoto wafanya graduation yao
   
 5. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  bado haizuii kuipeleka chadema ikulu duuuh huyo ni bogas kama mrs mkwere
   
 6. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyu Bi Bernadette Kinabo huyu mmmh:tape:
   
 7. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Jamani angalieni! mwishoni mtakuja kuahirisha mazishi. Hofu yote ni ya nini? kumbe mambo ya CCM yamefikia hali hiyo. Kwa kweli tufanye maandalizi ya kuiaga CCM.

  Watu walishatabiri huko nyuma kuwa CCM itakufa mikononi mwa Kikwete.
   
 8. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Karibu mkuu! NAONA UMEAMUA KUINGIA USIKU HUU HUU!
   
 9. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Dah! Hii kali mkuu. Kuahirisha mpaka mazishi? In short it means hakuna kufanya event yoyote yenye mkusanyiko wa watu mpaka baada ya uchaguzi?
   
 10. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Changanya na zako, watani wamebaki wasanii tu :smile-big:
   
 11. GFM

  GFM JF-Expert Member

  #11
  Oct 28, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kama hii taarifa ni ya kweli basi tujiande na vurugu za matokeo maana kwa mtaji huu sintashangaa wakivuruga matokeo
   
Loading...