Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,868
Na Dotto Bulendu
1.Mbunge anapoongea bungeni,huongea huku akiwa na kinga kwa mujibu wa Katiba,Lissu alisema atarejea nyumbani September 7 hivyo angekuwemo kwenye bunge la September,Spika anahofu Lissu akiingia Bungeni ataongea mambo ambayo yatakuwa mwiba hivyo ameamua kumuondolea mapema kinga hii ya kikatiba?
2.Serikali ilisema mtu ambaye siyo mbunge wa eneo husika haruhusiwi kuendesha siasa kwenye jimbo ambalo siyo lake,je Spika amehofia Lissu akirejea jimboni kwake atatumia nafasi ya ubunge wake kuandaa mkutano wa hadhara na kuongea na wananchi wa jimbo lake na kusema mambo ambayo labda Spika anayahofia?
3.Ni kweli Spika hajui Lissu yupo wapi na anafanya nini?kwa nini Bunge limeendelea kumlipa Lissu mshahara wakati hawajui yupo wapi?Spika anataka kusema kitendo cha Lissu kutokuwa hospital na kuwa nyumbani akipata matibabu kutoka nyumbani ni kosa na Lissu alitakiwa aendelee kukaa hospitali?
4.Je mawasiliano ya ofisi ya Bunge na familia ya Lissu mara baada ya kupigwa Risasi ambayo familia ya Lissu kupitia kwa Kaka yake Wakili Mugway ilikuwa ikiwasiliana na ofisi ya Bunge kuomba Lissu atibiwe na Bunge si taarifa rasmi ya wapi Lissu yupo na anafanya nini?
5.Barua za Lissu kupitia Familia yake kuomba Ofisi ya Bunge isaidie matibabu ya Lissu na Familia ya Lissu ikajibiwa(kwa mujibu wa kaka wa Lissu),kuwa Bunge haliwezi gharamia matibabu ya Lissu kwani hakufuata utaratibu wakati akienda Nairobi kwa matibabu hazikuwa barua rasmi za kiofisi zinazoonesha kuwa Lissu ni mgonjwa?
Haya mambo hayaaaa,yanatafakarisha sana!binafsi naamini Uongozi ni kuwawafanya watu wako wawe wamoja na wenye kupendana bila kujali tofauti walizonazo!.