Hofu ya maambukizi ya VVU inanimaliza kiafya, nilishiriki ngono na muathirika wa UKIMWI

Zegota

JF-Expert Member
Jun 5, 2020
274
584
Ni siku ya 31 leo tangu nianze kutumia dawa za Kuzuia maambukizi ya Ukimwi kwa watu walio mazingira hatarishi kupata ugonjwa huo (PEP), Dozi hii nimeimaliza jana.Hofu niliyo nayo imenifanya nishndwe kufanya kitu chochote cha maana zaidi ya kuzorota mwili.

Binafsi nina utaratibu wa kupima afya kwa kila mwanamke mpya ninaekutana nae, lakini siku ya kufa nyani miti yote huteleza.
Huyu mdada sikuwahi kukutana nae katika maisha yangu, kwa mara ya kwanza nimekutana nae MALAIKA BEACH HOTEL MWANZA ilikuwa ni usiku wa Jumapili, Mimi nikiwa ni mgeni pale kwa siku kadhaa na huyu dada alikuwa na marafiki zake kwenye meza iliyokuwa pembeni yangu. Kwa umbo na uzuri wamebarikiwa haswa.

Alikuwa amevaa vazi ambalo ukichanganya umbo na rangi yake kwa namna yoyote ile mwanaume yeyote aliyekamilika lazma atatamani kuwa karibu, na vyombo vilikuwa vimeshanikolea kama saa 6 hivi usiku nikamuita kumuomba kampani ahamie kwenye meza yangu hakusita, huo ukawa mwanzo ambao mwisho wake tukawa wote kwenye room yangu niliyofkia pale hotelini. Siku hii sikuwa na vipimo, nilijaribu kutafuta pale hotelini nikakosa ilibidi nichukue condom, Tukafanya sikuwa na vurugu katkati ya mchezo mwenyewe nikaomba kuchomoa ile condom akakubali hata hivyo sikuchukua mda nikamaliza baada ya kumaliza nikawa najilaumu sana na sikurudia tena mpaka alivyoondoka tukapanga, tukutane kesho yake ili tuweze kupima tufanye mambo yetu kwa uhuru, Akakubali.

kesho yake Jumatatu Akaja, na mimi nikawa tayari nimeshanunua Vipimo. Mwenzangu akabadilika akagoma kupima baada ya kumbembeleza kwa mda mrefu akakubali kwa sharti nianze mimi na majibu yeye nisimpe nibaki nayo mimi. Baada ya kupima majibu yake yakawa na changamoto. Nilijihisi kufa na isitoshe kipindi tunapimana ile kujitoboa nilishika kile kidole chake bila tahadhari, Sehemu ya damu yake ikagusana na kidole chngu nilichojitoboa kutoa damu. Hapa nilichanganyikiwa zaidi.

Asubuhi ya Jumanne nimeamka mapema kazi ilikuwa ni kusaka hospital ambayo naweza Kupata dawa za PEP ili nianze dozi, nilizunguka na boda kama kichaa. Jana nimemaliza hii dozi na kila wiki tangu nianze kutumia hii dozi nacheki afya yangu. Mpaka mda huu bado sijapata maambukizi ila nina hofu sana.

Kila nikifikiria huu ugonjwa napata shida sana.
 
Kama umemeza pep mkuu kua na amani uwezi kupata, kama ulipima kabla ujaanza kutumia ukawa upo negative, then umemaliza pima alaf subiri miezi mitatu upime tena apo ndo utakua umekamilisha, kua na amani kabisa chief.
Niliwahi kabla ya 72hrs kuisha, na kila week napima mpaka mda huu navoandika hapa sina maambukizi ila ninahofu sana, nasubiri nijitazamie miezi 4 to 5
 
Pole na relax usiwe na wasiwasi.

Tumeshapitia huko tunajua tunafahamu mziki wake wa kuwa na mawazo.
Acha kabisa mkuu, mpaka miezi 5 ipite ndio naweza kurudi kwenye maisha yangu ya kawaida kama hali ya kiafya itabaki kama ilivo sasa
 
Kapime ili uwe na amani.Mkuu,most probably uko safi,wanaume huo sio rahisi sana ku-contract HIV-Aids,unless kama una vidonda vidonda kwenye uume wako.Kapime ili kama unao uanze ARVs.

You can still leave a happy long life with ARVs.Nina shemeji zangu wawili waligundulika wana HIV muda mrefu sana uliopita,wana watoto wakubwa tu,na wenyewe wanene tu,wala huwezi kujua,na wanaume wanawapapatikia Kama kawaida.
Nikapime Mara ngapi tena chief? Kila week tangu nianze kutumia hizi dawa napima, Mara ya mwishi ni Leo
 
Back
Top Bottom