Hofu ya kurudiwa uchaguzi yatanda ndani ya CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hofu ya kurudiwa uchaguzi yatanda ndani ya CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Facts1, Jan 10, 2011.

 1. Facts1

  Facts1 JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2011
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 308
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Sakata la kujiuzulu kwa Naibu Meya, Michael Kivuyo, limewafanya viongozi wa CCM Wilaya ya Arusha kufanya kikao cha dharura hadi usiku.

  Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho zinasema suala la kujiuzulu kwa Naibu Meya ni mshtuko mkubwa kwa chama hicho ambapo hivi sasa wanalazimika kujipanga kwa mikakati mipya.

  Habari hizo zinaeleza kikao hicho kiliitishwa mara moja baada ya kupata taarifa za kujiuzuru kwa Kivuyo ambaye walikuwa wakiamini yuko katika msimamo mmoja na chama hicho.

  Kikao hicho kiliitishwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda, na kufanyika katika ofisi za chama hicho huku hofu ya kurudiwa kwa uchaguzi ikitawala katika kikao hicho.

  Aidha, baadhi ya viongozi wa chama hicho mjini hapa wanaona fedheha kwa chama hicho kuendelea kumuacha katibu huyo wa mkoa kushughulikia suala hilo wakati yeye ndiye chanzo cha vurugu zote hizo.

  "Unajua hivi sasa chama kama vile hakina mwenyewe kwa sababu kila mwenye nafasi ndani ya chama anafanya anavyotaka bila kuonywa ama kushughulikiwa kutokana na udhaifu ulioko makao makuu," alisema mmoja wa viongozi wa chama hicho.

  Aliendelea kusema kuwa hata kushindwa kwa uchaguzi jimbo la Arusha mjini kulitokana na uongozi wa mkoa kipindi cha uchaguzi kuanza kuhamisha watumishi hovyo hata madereva hivyo kufanya watumishi kuishi kwa hofu.

  Alifafanua hali hiyo ilipelekea kila mtumishi kufikiria jinsi ya kulinda kibarua chake badala ya kufikiria kukisaidia chama kupata ushindi hali iliyopelekea mgawanyiko mkubwa.
   
 2. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Source
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kumbe nao wanajua hawapendwi?
   
 4. V

  Vipaji Senior Member

  #4
  Jan 11, 2011
  Joined: Jun 11, 2009
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nani atampenda kichaa Kama chitanda
   
 5. n

  ngoko JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mary lazima aitishe kikao ili apate la Kumwambia Makamba
   
 6. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,207
  Trophy Points: 280
  Watabana mwisho wataachia.
   
Loading...