Hofu ya kuitosa Tanzania katika ujenzi wa LNG nchini: Shell wauliza swali - Is the cake big enough to satisfy all stakeholders?

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
May 30, 2017
2,869
3,188
IMG_9871.JPG

Ukanda wa Gesi, nchini Tanzania

Kumekuwepo hofu hapa nchini Tanzania kufuatia Kampuni ya Nishati ya Royal Dutch Shell kutiliana saini na Jimbo la British Columbia (Canada), pamoja na Serikali ya Canada ili kujenga Kiwanda kikubwa cha Kuchakata Gesi (LNG) jimboni humo. Hofu hiyo inatokana na kwamba, soko la gesi hiyo iliyochakatwa ni Nchi za Asia ambazo ndizo zinazotarajiwa kuwa wanunuzi wakuu wa gesi (LNG) ya Tanzania na kwamba huenda Makampuni ya gesi yaliyopanga kujenga LNG nchini yameshatupilia mbali mpango wake wa awali wa kujenga kiwanda hicho mkoani Lindi.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Utafiti na Uzalishaji wa Shell nchini Tanzania, Marc den Hartog, alitupilia mbali hofu hiyo na badala yake kuahidi kuwa tayari kujenga kiwanda cha LNG nchini Tanzania.

Hartog alidai kuwa, Makampuni yanayoshirikiana kuwekeza kwenye LNG nchini Tanzania (Shell, Ophir, Equinor, ExxonMobil na Pavillion), yameshamaliza kufanya utafiti na kukamilisha processes zote za awali ambazo zimeweka gharama zote hadi sasa kufikia Dola bilioni 4 hadi sasa, sawa na zaidi ya trilioni 9.

Hartog alidai kuwa, Mradi huo umekwama kutokana na kutokamilika kwa makubaliano na Serikali katika Host Government Agreement, tangu mazungumzo yaanze Mwezi Oktoba 2016.
Aidha, Shell ikiongea na The Guardian, iliwahakikishia Watanzania kuwa, licha ya kuanzishwa kwa Kiwanda kikubwa kipya nchini Canada, bado Mradi wa LNG nchini Tanzania una maana kubwa kwa sababu zifuatazo:
  • Shell imegundua teknolojia mpya na ya kisasa katika uchakataji wa gesi inayosaidia kupunguza gharama za uzalishaji.
  • Uwepo wa kiasi kikubwa cha gesi kutosheleza mauzo ya nje na mahitaji ya ndani.
  • Eneo zuri linalofaa kwa kujenga LNG.
  • Hali nzuri ya hewa kwa ujenzi wa kiwanda.
The Guardian lilipomuuliza Hartog kuwa, ni vipengele vipi vitakavyofanya mfikie makubaliano? Alijibu kuwa: Linapokuja suala la faida, swali la kwanza kujiuliza ni "is the cake big enough to satisfy all the stakeholders?"

Hapa ndipo ninapoelewa kwa nini Omuzilankende Muyago amewabania hawa jamaa, coz wanatafuta maximuma profit. Sasa kwa Makampuni matano, utayaridhishaje?

Sasa, hawa jamaa wameshasema gharama za utafiti zimeshatumia kiasi cha trilioni 9: ninajiuliza hizi records na sisi tunazo na tunazikubali?

Je, Omuzilankende Muyago anajua wazi kuwa, tumepigwa mahela mengi kwa udhaifu wa Serikali iliyopita?

Si bure wazee, something is fishy, haiwezekani Rais asite hivi hivi kujenga LNG ili apate hela nyingi tena za haraka haraka ambazo zingewezesha Serikali kujenga miundombinu mikubwa mikubwa ukiwemo SGR.

IMG_9870.JPG
 
Awamu hii hamna upigaji, hapo kwa kuzuia kuliwa Magufuli namuunga mkono. Ila ninacho shangaa akiwa waziri mbona tulipigwa sana? Kwanini hakuingilia kati? Tuseme kwa wakati ule hakuwa mzalendo?
 
Labda serikali inataka ipate best deal. Isijekuwa km yaliyotokea kwenye dhahabu na almas
 
Awamu hii hamna upigaji, hapo kwa kuzuia kuliwa Magufuli namuunga mkono. Ila ninacho shangaa akiwa waziri mbona tulipigwa sana? Kwanini hakuingilia kati? Tuseme kwa wakati ule hakuwa mzalendo?
Hakuwa na sauti ya mwisho, rudi kwenye jengo la Tanesco Ubungo
 
Awamu hii hamna upigaji, hapo kwa kuzuia kuliwa Magufuli namuunga mkono. Ila ninacho shangaa akiwa waziri mbona tulipigwa sana? Kwanini hakuingilia kati? Tuseme kwa wakati ule hakuwa mzalendo?
Ile ilikuwa serikali ya Kikwete na hii sasa ni serikali yake Magufuli.
Ukiwa kwenye nyumba ya baba yako huwezi toa maamuzi ya kuongoza familia bila baba yako kuyakubali.
 
Back
Top Bottom