Hofu ya Katiba Mpya

Achanakia

Member
Jan 28, 2021
70
81
Nimsikiliza Rais Mama yetu mpendwa Samia Suluhu Hassan,katika hotuba yake ameongea mambo mengi ya msingi na yenye kutia matumaini.

Moja ya maeneo aliyonifurahisha katika hotuba yake ni tone anayotumia katika uwasilishaji wa hoja zake. Kitendo cha kuahidi kufanya maboresho kwenye sera zetu za biashara na uwekezaji kwa lengo la kukuza uchumi na kuongeza ajira. Kuanzisha utalii wa kutumia meli na maboti kwenye eneo la bahari. Kuinua sekta ya kilimo ili kuleta tija.

Serikali kuwa tayari kupokea ushauri wenye kujenga kutoka kwa mtu au kubdi lolote la watu vikiwemo vyama siasa na kuruhusu ukosoaji wenye nia ya kujenga.

Kurekebisha mfumo wa ukusanyaji kodi ili uwe rafiki kwa walipa kodi badala ya kutumia nguvu na mabavu.

Kubwa sana ni hili la kutaka kukutana na viongozi wa vyama vya siasa kwa lengo la kujadiliana namna bora ya kuboresha demokrasia yetu kwani palipo na demokrasia na maendeleo ya kweli yanapatikana. Hilo limenifurahisha sana kwani huo utakuwa mwanzo mzuri wa kuliweka taifa letu pamoja ambalo kwa kiasi kikubwa limeingia kwenye mgawanyiko mkubwa kutokana na aina ya siasa zilizokuwepo.

Hata hivyo nilitarajia kumsikia Rais akiahidi suala la katiba mpya ikiwa ni pamoja na kuondoa sheria zote kandamizi ambazo kwenye utawala uliopita zilitungwa mahususi kwa ajili ya kupunguza uhuru wa kiraia.

Kuhusu suala la katiba mpaka sasa sielewi hofu ya viongozi wetu kuruhusu upatikanaji wa katiba mpya inatokana na nini?
Nasema hivi maana nikikumbuka watangulizi wa mama yetu Samia ukiachilia mbali Rais Magufuli ambaye alitamka wazi kabisa kwamba katiba mpya sio kipaumbele chake.

Rais Kikwete alianzisha mchakato huo vizuri kabisa mpaka na bunge la katiba likanza kufanya vikao. Lakini cha kushangaza alipoona wahafidhina wa ccm hawakubaliani na mapendekezo mengi ya ile rasimu ya Warioba ambayo kimsingi yalikuwa ndio maoni na mapendekezo ya Watanzania nayeye akageuka na kuungana na wahafidhina wa chama chake ambao hofu yao kubwa ilijengwa kwenye madaraka wala si vinginevyo.

Swali langu ni je hawa viongozi wetu wanaihofia katiba mpya kwasababu gani?

Je hawaoni kwamba katiba mpya ni hitaji muhimu kwa mustakabali mzima wa amani na umoja wetu kama nchi?
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom