Nina hofu ya Hepatitis B naomba ushauri

Pole sana bro. Ila haina haja ya kupanic sana haswa ukizingatia kwa sasa unajihisi upo normal ingawa madaktari wanasema unaumwa,Kila siku moja unayoamka ukiwa salama ni muhimu sana kwako na kwa jamii yako Jaribu kuishi maisha uliyonayo sasa,USIKUBALI KESHO YAKO IKUHARIBIE LEO YAKO!
Nakushukru mkuu
 
KINGSLEE, Chanjo kwa watoto wadogo imeanza kutolewa miaka ya 2000s. Na hata ukiangalia kwenye kadi za clinic za watoto hbv ni miongoni mwa chanjo zinazotolewa.

Kwa waliozaliwa kabla ya hapo chanjo zinatolewa Ocean road hospital. Kwa sasa ni jukumu la mtu kuamua kupata chanjo au kutopata kwani zipo zinatolewa kwa wote.
 
One of my family members was diagnosed with hepatitis B three decades ago, akaambiwa hakuna tiba. Baadae akapata complication ya ini. Alifuata masharti ya dr ya don’ts. My late mother alihangaika na dawa za kienyeji mbalimbali. Ajabu mgonjwa alipona na anadunda vizuri, lakini hajui specifically ni dawa ipi ilimponya kwa sababu alitumia concoction ya kutosha
Ashukriwe Mungu kwa kuwezesha uponaji huo.
 
Pole sana mkuu,wataalamu si wanasema kwamba Ini linatabia ya kujitengeneza upya lenyewe.
Ni kweli, lakini pia wanasema inategemeana na kiwango cha madhara yaliyokwishatokea. Kama ni kidogo na mashambulizi ya virus yakikoma, ini linao uwezo wa kuclear pale lilipokuwa limeathirika.
 
Hakuna kinachoshindikana kwa Mungu Hofumoyoni, Mtumaini Yeye! Kwa Imani yako uwe na Moyo Mkuu! Alikujua hata kabla hujazaliwa na anaujua mwisho wako! Mkabidhi maisha yako ishi kadri ya matakwa yake! Mungu ni mwema Atakuponya maradhi yako!
 
moesy, Nakushukru mkuu.
1. Viral load nimefanya ikasoma negative wakati hbv antibody ni postive.
2. LFT nimefanya ikaonesha linafanya kazi vivuri. japokuwa kulikuwa na baadhi ya maeneo 2 ambayo moja ilikuwa juu kidogo ya kiwango na nyingine ilikuwa chini kidogo.
3. Figo normal
4. CT Scan ya ini ndo sijafanya.
5. Endoscop nilifanya nikashauriwa kufanyiwa band ligation, miezi sita baada ya banding nikarudia wakasema iko normal.

Hofumoyoni,
Pole kwa yote unayopitia.
Ningependa kusisitiza juu ya kutulia na kutafakari juu ya ukuu wa Mungu. Natumaini anayosababu ni kwa nini alliwezesha wewe kuwepo. Na uwepo wako hautegemei nguvu zako, hivyo mtumainie muumba zaidi na uendelee na ratiba zako za maisha ukizingatia ulichoelekezwa ufanye au usifanye kulingana na hali yako. Hautaondoka duniani pasipo kutimiza kusudi la Mungu, hivyo ondoa hofu.

Kuna kitu ambacho ningependa kupata maelezo kidogo kwani kwa jinsi nilivyoona naona kuna mkakanganyo. Hii inatokana na majibu namba moja hapo juu:

1: Kwamba walipima antibody- hii tunaitumia kwenye kufatilia kama mtu alishapata chanjo na kama chanjo ilifanikiwa na si kwa kuangalia mgonjwa halisi, hivyo jaribu kuangalia ni hiki kipimo kilifanyika au la? Na kama ni hiki majibu hutolewa kwa kiasi na si kusrma ni positive au negative.

2: Viral load negative- viral load nilitegemea kupata idadi yake ili kuona kama idadi imevuka kiasi kinachotakiwa na si neno negative peke yake. Kwani hivi ni moja ya vigezo katika mtu kuanzishiwa dawa.

3: Kama ilivyosemwa na mdau hapo juu (Moesy), fanya CT scan ili kupata uhalisia katika maumbile ya ini. Ni vyema kuwa na daktari bingwa wa njia ya chakula mwenye uzoefu na tiba hizi ambaye atakuwa anafatilia hali yako.

Maana, wakati mwingine sisi binadamu tunakuwa na mwitikio hasi tunapoona hali inayotatanisha kwa wenzetu na hatimay kuwavunja moyo kwa kutokuwa na uhakika/kujua au kwa makusudi.

Ahsante.
 
Toa hofu ndugu Mimi nilikua natumia dawa za hepatitis b yaani truvada (arv) nilitumia miez 18 baadae hi hospital ya hapa mkoani kwetu wakanambia hawatoi dawa Tena niende nikachukue muhimbili,Basi nikaenda kwa doctor ili aniandikie transfer ya muhimbili ,yule doctor akanambia ndugu yangu utapoteza pesa bure huo ugonjwa utaisha wenyewe tu mwilini na palikua na wazungu madaktar wakashauri hivo hivo,Basi nikarud nyumbani.

Hivi Leo ni mwezi wa 6 ni mzima wa afya na situmii dawa zozote , Kuna wakat nasahau kabisa Kama niliwahi pata hili tatizo,chamsingi acha stress kuhusu Hilo suala sababu stress zinazoofisha Kinga ya mwili , we usiwaze Sana coz mwisho wa siku mauti yapo palepale unapona hepts b unagongwa na gari unakufa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom