Hofu ya CCM ya Magufuli 2020 ni Hatari kwa nchi

Isemwe ukweli tu, makundi hasimu na wenye mitazamo tofauti ndani ya CCM yamekuwepo toka enzi za Mwalimu.
Tofauti iliyopo saa ni kushindwa kwa Mwenyekiti kuyabalance makundi hayo kwa kuyapa vyeo, nyadhifa na hata kuyakusanya kwa dinner pamoja.

Kutumia mabavu si suluhisho maana hiyo italeta mtafaruku mbaya aidi.
Hivi kuna ubyaa gani Mwenyekiti akiwaita wale anaotofautiana nao ndani ya CCM, wakakaa pamoja, pasuliana ukweli behind closed doors na kutoka na tamko la Umoja?

Yanayoendelea yataliangamiza Taifa na Umoja wake kama tunavyolifahamu.

Watu wakifunuliwa myumbo aliokuwa nao mkwere halafu yule mkwere alikuwa anakula bata utafikiri kuko shwari vile kumbe CCM ilikuwa mbaya balaa tena joka mkubwa EL alikuwa ndani ya nyumba upande mwingine CDM yenye nguvu ikichagizwa na EL pamoja na RA bado pressure ya raia lakini mkwere aliishi kwa hesabu na timing na akawafanyizia maadui zake wakati sahihi na mahala sahihi..
 
,Ndio maana watanzania wazalendo wanapigania demokrasia ndani ya vyama vyao na kwa serikali yao .Wale wanaopinga jambo hili nakukazania kujenga mfumo wa autocratic system utasababisha mifarakano kwa kuwa mfumo huo umeisha pitwa na wakati .Watanzania wanaitaji wote washiriki kujenga nchi yao bila kubaguana na chuki za ukabila,ukanda nk
 
Huyu Zitto naye anataka kutuaminisha nini, Aelewe kuwa yeye ni mpinzani na anatumia milage kujiendesha kisiasa. Hapa anataka kuwatumia hawa wazee ambao hana imani nao na sio mtetezi wao. Mbona alipokuwa chadema na alisikika na watu akisema Kinana anawapa tabu sana na yeye na Dr.Slaa wakamtengenezea uongo wa ujangili, alipofukuzwa hakusema ukweli. Leo anakata kutuimanisha nini?

as like any politician use the milage lakini tunajua huna upendo wowote na hao wazee.
 
Lakini busara itumike, huyu bwana magufuri wote tayari tunajua yuko tayari kuua watu ilimradi analotaka yeye liwe, sasa hii hofu yake inavyoongezeka ndio raia wengi zaidi uhai wao unakuwa matatani.

Nashauri, kama inawezekana ahakikishiwe kuwa rais mpaka 2025 akili yake itulie, nashauri tu.
Haki ya MUNGU!.Aisee.
 
Isemwe ukweli tu, makundi hasimu na wenye mitazamo tofauti ndani ya CCM yamekuwepo toka enzi za Mwalimu.
Tofauti iliyopo saa ni kushindwa kwa Mwenyekiti kuyabalance makundi hayo kwa kuyapa vyeo, nyadhifa na hata kuyakusanya kwa dinner pamoja.

Kutumia mabavu si suluhisho maana hiyo italeta mtafaruku mbaya aidi.
Hivi kuna ubyaa gani Mwenyekiti akiwaita wale anaotofautiana nao ndani ya CCM, wakakaa pamoja, pasuliana ukweli behind closed doors na kutoka na tamko la Umoja?

Yanayoendelea yataliangamiza Taifa na Umoja wake kama tunavyolifahamu.

Nakubaliana na wewe lakini wakati huohuo sikubaliani na wewe pia...Kosa ni hao wengine kuandaa mipango yenye mwelekeo wa uhaini...nimeisikiliza kwa umakini ile clip inayotambaa mitandaoni ambapo baadhi ya maneno kwenye clip hiyo ni kuwa 'bwana mkubwa' amechanganyikiwa na kwamba eti anaogopa kurudi Dar....ile clip, kwa maoni yangu, ni ya kweli na wala siyo fake...sasa basi maneno hayo kumhusu 'bwana mkubwa' ni ya hatari mno...Nimmaneno yenye mwelekeo wa usaliti kamma siyo uhaini...ni hatari...Ni nani aliyeshika mpini ??? Hii CCM ilikuwa imeoza mno...juhudi zilizopo ni 'ku-cleanse' hili lichama ...hapa ndipo lilipo tatizo.. Ngoja tusubiri tuone how things are unfolding...lakini mimi binafsi nauona mwisho mbaya wa baadhi ya watu tuliowazoea...kujinusuru itabidi wakaombe radhi kimya kimya....
 
Dereva wa Bedford kona inamshinda anaona dawa ni kuwatupa baadhi ya abiria ili kazi iwe nyepesi
 
Asante Zitto, tuungane pamoja na yeyote mwenye nia njema bila kujali itikadi zetu kwa ustawi ma umoja wa taifa letu.Tanzania ni kubwa zaidi ya Binadamu yeyote.Madaraka ni koti la kuazima.
 
-HOFU ya CCM ya Magufuli ni Hatari kwa Nchi yetu

Kwa wiki moja sasa kumekuwa na mjadala mkali nchini kuhusu Tamko lililotolewa na Makatibu Wakuu wastaafu wa CCM Kanali Abdulrahman Kinana na Luteni Yusuf Makamba kuhusu mtu anayeitwa Cyprian Musiba. Wana CCM hao wameandika malalamiko yao kwa Baraza la Wazee wa Chama chao ili hatua zichukuliwe. Katika hali ya kawaida hili lilipaswa kuwa jambo la CCM na kushughulikiwa na chama hicho wenyewe. Hata hivyo jambo hilo limechukua mkondo wa kitaifa na haswa usalama wa watu na usalama wa Taifa.

Tamko la Kanali Kinana na Luteni Makamba limeujulisha Umma mipango dhalimu ya kubumba kesi za uhaini kwa Wanasiasa waandamizi nchini kutoka Chama Tawala na Vyama vya Upinzani. Pia baadhi ya wana harakati ambao Bwana Musiba amekuwa akiwataja kuwa ni watu hatari kwa nchi ni miongoni mwa wahanga wa mipango hiyo. Kina Kinana wametibua mpango huo ndio maana wafuasi au wanaojiita wanaomwunga mkono Rais Magufuli wametaharuki na wanajaribu sana mipango yao iendelee. Shabaha ya kesi ya uhaini ni kuhakikisha ama mwaka 2020 hapatakuwa na uchaguzi au uchaguzi ufanyike wakati wanasiasa wote waandamizi nchini wakiwa magerezani au wasiwepo kabisa.

Baadhi ya wanasiasa wameanza kujiokoa kwa kujiegemeza upande wa wenye mamlaka. Hata wale ambao kwa muda sasa wamekuwa ni tumaini la Wananchi kwa kuwa wakosoaji wakuu wa Serikali wamerudi nyuma na kutoa kauli za kujikosha . Kwa mfano mtu ambaye amekuwa akikosoa vikali Serikali kule mwanzo nia ilikuwa ni kumnyima uhalali Rais Magufuli ? Mbona wakati wa Uongozi wa Rais Jakaya Kikwete alikuwa anashambuliwa sana na Wazee kama vile Mzee Butiku, Warioba nk lakini hatukusikia haya? Kitu gani ‘special’ wakati huu? Nadhani huu Ni wakati kwa wapenda demokrasia wote kutoogopa na kuwa pamoja.

Sisi wengine tunajua kitambo kuwa CCM imeshafika mwisho wake. Bahati mbaya sana CCM ya Magufuli inataka kuondoka na nchi yetu. Tusikubali. Tumesoma kuwa kabla ya Wazee hao wastaafu wa CCM kuandika, waliomba ushauri na Mzee Pius Msekwa akawaambia ‘jibuni Mapigo’. Ina maana Msekwa naye anataka kuua Chama chao? CCM ianguke yenyewe na ituachie nchi yetu.

Hofu ya Watawala kuhusu 2020 isihatarishe nchi yetu. Mipango ya Kesi ya Uhaini iachwe mara moja. Ukosoaji ndani au nje ya vyama vya Siasa kamwe haiwezi kuwa uhaini. Acha demokrasia ishamiri

Zitto Kabwe
18/7/2019
Sawa sawa
 
Naangalia Azam UTV, JIWE yuko live Kongwa. Anamsafisha Ndugai eti sio fisadi ni msafi mzalendo. Nae anamuomba Mungu ampe hekima ili asiwe na 'kiburi'. Mpaka kufikia uchaguzi tutaona vichekesho vingi.
 
Asante Zitto, tuungane pamoja na yeyote mwenye nia njema bila kujali itikadi zetu kwa ustawi ma umoja wa taifa letu.Tanzania ni kubwa zaidi ya Binadamu yeyote.Madaraka ni koti la kuazima.
Kwa Zitto NI nwachama wa CCM? Mnajisumbua bureee JPM ni Hadi 2025/30
 
Naangalia Azam UTV, JIWE yuko live Kongwa. Anamsafisha Ndugai eti sio fisadi ni msafi mzalendo. Nae anamuomba Mungu ampe hekima ili asiwe na 'kiburi'. Mpaka kufikia uchaguzi tutaona vichekesho vingi.
Hahahahahaaa,pesa alizotumia India zikaguliwe!
 
Back
Top Bottom