Hofu ya CCM ni kwa CHADEMA kuwa na pesa?

Ninachohofia kwenye hii post ni mlolongo wa kashfa na matusi ambao unaweza kufuata hapo chini.
 
2000-2008 cuf ikipokea pesa za waarabu ili kuandamana. nchi ikakumbwa na wasiwasi mkubwa. uvumi wa ugaidi ukaenea kila upande. nakumbuka hata balozi wa marekani alitoa nasaha UDSM kwenye kanisa kwa watanzania kuigopa cuf ni chama kinachopata misaada kutoka uarabuni. aliwataka watanzania wasidanganyike, aliwataka kuwa makini na CUF
lkn sasa imekuja chadema, kinapata ufadhili kutoka mataifa ya kizungu mpka majina yametajwa kwenye vyombo vya habri kufanya maandamano huku ccm ikiwatahadaharisha wananchi.sasa wenye uchungu na nchi tunakumbuka matamko ya wazungu juuya Cuf. lkn pia tunangalia taifa linaelekea wapi juu pesa za wazungu kwa chadema
jee taifa nilaekea wapi? au ndio ule msemo mavi ya Mzungu hayanuki?
wabongo kwa MIPASHO na USHAMBENGA hawajambo! ehe! tuambie huo udaku wa kuwa CDM inafadhiliwa na wazungu umetoa wapi Wacheni Mipasho ndugu zangu!
 
Acheni unafiki uliopindukia. CCM imekuwa ikipokea misaada ya fedha kutoka kotekote, mashariki na magharibi toka kwenye "Vyama Rafiki" bila ya matatizo yoyote.

Ila chama kingine chochote kinachopinga sera mbovu za CCM wakipewa msaada hata kama ni kidogo vipi ni "Uhaini".

Kwanza hizo fedha mnazosema zinatoka nchi za magharibi ni kiasi gani na zinafanya kazi ipi maana kama ni maandamano sijaona watu wabebwe kwa magari ya kukodi au "Kujitolea", wagawiwe hata chupa za maji au vilemba kama inavyofanya CCM.

Kwa uzoefu wangu watu huhamasika kwenda kwenye maandamano ya CDM bila ya hata kujiuliza watapata nini. Kwa maoni yangu CCM ndiyo mabingwa wa kutumia fedha chafu kwa minajili ya kujinufaisha kisiasa. Hatujaambiwa zile Helikopta JK alizokuwa akipasua nazo anga zilikuwa mali ya nani na alilipwaje?

Na gharama za fulana, vilemba, tai, khanga, vitenge (Ambavyo hadi sasa tunadekia) bila kuhesabu mabango nchi nzima mpaka kijijini alikozaliwa Kikwete (Ambako wanamfahamu vema) nani alizilipa na kwa makubaliano yepi? Na vipi sheria ya gharama za uchaguzi; walitungiwa wapinzani tu?

Mbona CCM ilizivuka na hatusikii lolote hadi leo?
 
Asante kwa thread. Ndiyo maana serikali ya CCM inanuka mavi kwa sababu kiongozi wake, JK amekuwa anatembeza bakuli kwa kupata pesa za Wazungu kila kukicha!

Ushauri wa bure: Angalau basi mjuwe mnatoa kau-shahidi hata kidogo kwamba CDM wamepokea sh kadha kutaka mahala kadha........ Badala yake mnatoa uharo tuuuuuuuuu!
 
2000-2008 cuf ikipokea pesa za waarabu ili kuandamana. nchi ikakumbwa na wasiwasi mkubwa. uvumi wa ugaidi ukaenea kila upande. nakumbuka hata balozi wa nchi za magaharibi alitoa nasaha UDSM kwenye kanisa kwa watanzania kuigopa cuf ni chama kinachopata misaada kutoka uarabuni. aliwataka watanzania wasidanganyike, aliwataka kuwa makini na CUF
lkn sasa imekuja chadema, kinapata ufadhili kutoka mataifa ya kizungu mpka majina yametajwa kwenye vyombo vya habri kufanya maandamano huku ccm ikiwatahadaharisha wananchi.sasa wenye uchungu na nchi tunakumbuka matamko ya wazungu juuya Cuf. lkn pia tunangalia taifa linaelekea wapi juu pesa za wazungu kwa chadema
jee taifa nilaekea wapi? au ndio ule msemo mavi ya Mzungu hayanuki?

Pumba tupui,

Mbona serikali inaishi kwa kutegemea fedha za wafadhili hao hao. Mbona Kikwete alikampeini kwa kutoa ahadi kuwa atapata au amepata wafadhafidhili kutka nje ambao wataibadilisha Tanzania kuwa Ulaya ya Afrika na mlikuwa hamkoromi.
 
Acha woga, onesha ushahidi wa hilo unachokinena, vinginevyo ni bora kukaa kimya kuliko kujitokeza mbele za mkutano ukiwa uchi
 
2000-2008 cuf ikipokea pesa za waarabu ili kuandamana. nchi ikakumbwa na wasiwasi mkubwa. uvumi wa ugaidi ukaenea kila upande. nakumbuka hata balozi wa nchi za magaharibi alitoa nasaha UDSM kwenye kanisa kwa watanzania kuigopa cuf ni chama kinachopata misaada kutoka uarabuni. aliwataka watanzania wasidanganyike, aliwataka kuwa makini na CUF
lkn sasa imekuja chadema, kinapata ufadhili kutoka mataifa ya kizungu mpka majina yametajwa kwenye vyombo vya habri kufanya maandamano huku ccm ikiwatahadaharisha wananchi.sasa wenye uchungu na nchi tunakumbuka matamko ya wazungu juuya Cuf. lkn pia tunangalia taifa linaelekea wapi juu pesa za wazungu kwa chadema
jee taifa nilaekea wapi? au ndio ule msemo mavi ya Mzungu hayanuki?
Kama kunuka wa kwanza angekuwa Kikwete maana kila leo yuko kwa wazungu.
 
Achana na habari za kwenye kahawa na kitchen party kwani hilo tamko la pesa za wazungu ilmetolewa na nani?

Umemuuliza mweka hazina wa cdm kuhusu chanzo cha pesa akakwambia? tatizo lenu ni kuruhusu watu wengine wafikirie na kutafakari badala yenu. Weka na zako pia!
 
Acheni unafiki uliopindukia. CCM imekuwa ikipokea misaada ya fedha kutoka kotekote, mashariki na magharibi toka kwenye "Vyama Rafiki" bila ya matatizo yoyote.
Ila chama kingine chochote kinachopinga sera mbovu za CCM wakipewa msaada hata kama ni kidogo vipi ni "Uhaini".
Kwanza hizo fedha mnazosema zinatoka nchi za magharibi ni kiasi gani na zinafanya kazi ipi maana kama ni maandamano sijaona watu wabebwe kwa magari ya kukodi au "Kujitolea", wagawiwe hata chupa za maji au vilemba kama inavyofanya CCM. Kwa uzoefu wangu watu huhamasika kwenda kwenye maandamano ya CDM bila ya hata kujiuliza watapata nini. Kwa maoni yangu CCM ndiyo mabingwa wa kutumia fedha chafu kwa minajili ya kujinufaisha kisiasa. Hatujaambiwa zile Helikopta JK alizokuwa akipasua nazo anga zilikuwa mali ya nani na alilipwaje? Na gharama za fulana, vilemba, tai, khanga, vitenge (Ambavyo hadi sasa tunadekia) bila kuhesabu mabango nchi nzima mpaka kijijini alikozaliwa Kikwete (Ambako wanamfahamu vema) nani alizilipa na kwa makubaliano yepi? Na vipi sheria ya gharama za uchaguzi; walitungiwa wapinzani tu? Mbona CCM ilizivuka na hatusikii lolote hadi leo?
Tell them bro.
 
Mtahangaika sana kujaribu kuiangamiza CHADEMA kwa propaganda mfu bila mafanikio...mlianza na ukabila mkaenda udini,mara uhaini sasa eti wanapewa fedha na wazungu...waaapii!Hizo zote ni dalili za mfa maji lazima mfe,pambaaaf....!
 
Tafadhali tutandikie hapa 'interim financial statement' za CDM ili nasi tuthibitishe hicho usemacho au ndo zile story za lile lichama letu lililo jibebesha mkataba wa kuitawala, kuitafuna na kuimeza tz na watz wake.<br />
Ni dhambi kuwa mvivu lakini ni dhambi kuu zaidi kutotumia ufahamu wako ipasavyo.
 
jamani hizo siasa zenu mnakotupeleka siko sasa,kama chadema wanapata pesa kutoka nje mnataka serikali ikae kimyaaaa?hata nao wakibahaatika wakaingia madarakani mchezo utakuwa ni huo huo...ila penye ukweli inatakiwa serikali iingilie kati na kusema...nawasilisha

Thibitisheni hizo kauli za CHADEMA kupata pesa toka nje sio kubwabwaja tu
 
jamani hizo siasa zenu mnakotupeleka siko sasa,kama chadema wanapata pesa kutoka nje mnataka serikali ikae kimyaaaa?hata nao wakibahaatika wakaingia madarakani mchezo utakuwa ni huo huo...ila penye ukweli inatakiwa serikali iingilie kati na kusema...nawasilisha

Nje wapi?
Kwanza ni aibu kwa serikali,ina maana haina uwezo wa kudhibiti hela zinazo ingia nchini?

Kama zinatoka nje,na zinatumika "kufanya uhauni" kwanini wasi vunje uhusiano na hiyo (hizo) nchi inayo (zinazo ) fadhili chadema?

Ni upumbavu kuongea tu bila kufanya chochote
 
CHADEMA KUPENDWA KULE KOTE NCHINI WALA SI FEDHA HATA MIZIZI

CHADEMA kupendwa saaana kule wala sio kwa uwezo wa FEDHA wala mizizi kama walivyozoea watani zetu wana-Chukua Chako Mapema isipokua tu ni kwamba WAPAMBANAJI hawa wajijengea tu kuaminika, kutumainika na kutegemeka pale CCM wanapohiari kugeuka MAFISADI kama kundi zima.

Mhe Kikwete, kazi mnayo na mtafumua nywele zote juu ya CHADEMA na hata kubaki vipara kwa visingizio vya kila aina; mara fedha kutoka nje, mara wasiandamano juu ya wizi wenu wa kura wakati ni haki ya kikatiba, nasema hadi kukatika miezi michache ijayo wengine mtakua kabisaa vichaa.

Zile fedha za CCM kutoka kwa Hosni Mubarak, Irani pamoja na kwa Alhaji Moammar Qadhaffi hivi sasa mnajisahaulisha kuzipokea kuchochea nayo udini nchini sio. Hebu endeleeni kwenye mstari huu muone mtakavyoaibika takwimu zikiporomoshwa hapa za fedha zenu za nje hata kabla walipa kodi hatujaporwa.

Inatia hasira sana tunaposikia maneno kama haya toke kwenye vinywa vyenu. Na kwa bahati mbaya sana, madikteta wafadhali wenu ndio hao wanang'olewa madarakani mkatafute wengine huko.

Siasa za sasa hivi ni UAMINIFU tuu kwa wananchi na wala sio fedha jaama!
 
Back
Top Bottom