Hofu ya CCM ni kwa CHADEMA kuwa na pesa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hofu ya CCM ni kwa CHADEMA kuwa na pesa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Mar 15, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  CCM imekuwa chama chenye nguvu kwa sababu ya pesa walizo nazo au wanazo-control, kuiba (kama vile EPA) na michango ya mabilioni kupitia wafanyabiashara ambao baadhi yao hupata mwanya ya kufanya wizi na ufisadi mwingine bila hofu kubwa ya kuchukuliwa hatua.

  Sasa ukiondoa pesa basi CCM hakuna kitu. Baada ya uchaguzi, mgao wa CCM wa ruzuku kutoka serikalini umepungua kwa zaidi ya Sh milioni 200 kila mwezi na tayari tumeona hilo limeanza kuwawewesesha.

  CCM wanazo taarifa kwamba CDM wanapata fedha nyingine nyingi ukiachilia mbali ruzuku ya serikali. Hili linawatia wasiwasi mkubwa. Taarifa hizo ni kwamba kuna baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wameanza kukichangia CDM kama kinga kwamba kutokana na dalili zinazoonekana waziwazi wa kupungua umaarufu wa CCM, huenda CDM ikachukua nchi 2015.

  Hawa wafanyabiashara (Waesia na Waafrika) wajanja sana, wanachangia CDM kimya kimya, (ukiuachia huyo Sabodo) tena mabilioni mengi. Wameona upepo jinsi unavyovuma.

  Sasa hilo ndilo linaipa CCM kiwewe kikubwa na ndiyo maana wanatoa kauli kwamba CDM inapata hela kutoka nje "kufanya machafuko". Wanajua kwamba wakisema wanapata kutoka ndani, haitakuwa na element ya "crime" ndani yake kwani nao CCM si wanapata pesa kutoka ndani?

  Lakini hizi ndizo siasa -- na ninasema hivi -- CCM iko tayari kutumia kila mbinu katika uwezo wake, za halali na haramu, iko hata tayari kumwagika damu kuliko kuachia madaraka kwa chama kingine kwa njia halali za kidemokrasia. Dalili hizo ziko na baadhi yake na kama hili la kuwasingizia CDM wanapata hela kutoka nje.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0


  Na hasa CCM wakitafakari hali walionayo wenzi wao wa zamani -- yaani UNIP ya Zambia! UNIP sasa hivi iko nyikani -- haina mapesa tena kama ilivyokuwa enzi zake za mikutano ya kifahari ya Mulungushi! Ewe Mola wangu, naomba CCM nayo itokomee huko huko nyikani!!

  Lakini hata hivyo naisifu UNIP na Kaunda wake kwa kuachia madaraka bila mizengwe kabisa.
   
 3. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2011
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  jamani hizo siasa zenu mnakotupeleka siko sasa,kama chadema wanapata pesa kutoka nje mnataka serikali ikae kimyaaaa?hata nao wakibahaatika wakaingia madarakani mchezo utakuwa ni huo huo...ila penye ukweli inatakiwa serikali iingilie kati na kusema...nawasilisha
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nasikia UNIP walikuja Dom mwaka fulani (baada ya kuwa nje ya madaraka) kwenye mkutano mkuu wa CCM kutokana na mwaliko. Wajumbe wake walifikia hoteli za uchochoroni hadi CCM waliposikia wakaenda kuwaondoa na kuwaweka katika hoteli nzuri.

  Nakubaliana nawe Bwana -- kwa chama kutokuwa na pesa ni balaa. CCM inaanza kuona jeuri ya CDM -- PESA!! Ingependelea jeuri hiyo wawe nayo wenyewe tu.
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Sawa - kama wanapata kutoka nje serikali ya CCM iache kubwabwaja - itoe ushahidi, iwakamate wahusika na kuwapeleka mahakamani. CCN hawana lolooooote! kazi yao kuu siku hizi ni kusemasema hovyo.

  Mfano maneno ya 'uhaini" au ya 'matusi' ya viongozi wa Chadema majukwaani hayajawekwa bayana, CCM hawasemi ni maneno gani hayo ya uhaini au ya matusi au kuwapeleka wahusika mahakamani.
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Mar 15, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ni kweli -- CCM imekuwa inaringia pesa walizonazo. sasa wanaone CDM nayo inaanza kuwa nazo - basi all hell has broken loose. Hawana hata aibu.
   
 7. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #7
  Mar 15, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  CCM wana siasa za kipesa. Ile CCM ya zamani na TANU yake ilikuwa na siasa ya kiutu zaidi.
   
 8. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #8
  Mar 15, 2011
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  CCM wameijenga Chadema, na wanaendelea kuijenga. Kabla ya Uchaguzi wa 2010 ni watu wachache sana waliona tishio lolote la maana kwa CCM na watu humu ndani walikuwa na kauli maarufu kuwa CCM iaendelea kutawala hadi 2050. Kwa nini mambo yamebadirika sana ghafla tu?? Sababu ni mapambano na minyukano ya ndani ya CCM ambayo walioko madarkani wamethibitisha kuwa hawana chembe ya uwezo wa kupambana na minyukano hiyo.

  Sasa kuja kwa "dimension" ya pili ya pesa, kunazidi kuongeza kasi ya uwezekano wa CCM kung'oka madarakani haraka zaidi kuliko hata wao wenyewe CCM walivyofikiria. Muundo wa CCM kuwa chama dola, chama ambacho kimuundo na kiutendaji ni sehemu ya serikali ulikifanya CCM kishindwe kuwa na miradi ya maana ya kukiwezesha kupata fedha. Chama ambacho kimekaa madarakani kwa zaidi ya miongo mitatu, utashangaa kikiondoka madarakani hakina mradi wowote wa maana. Sasa hivi watu tulitarajia CCM iwe mojawapo ya taasisi zenye ukwasi wa nguvu kama ilivyo mifuko kama PPF na NSSF, kwa sababu ya uwezekano kilio kuwa nao wa kujikusanyia mali bila kushughulikiwa na watoza ushuru. Lakini muundo uliokifanya chama hicho kiwe sehemu ya dola umekifanya kiwe chama cha kudokoa na kuchota mifedha kutoka serikalini kila kinapotaka. Bonanza hiyo ya wizi na uporaji umekifanya chama kilewe ulevi wa madaraka na kushindwa kusimamia miradi yake!

  Kutokea kwa Chadema na uwezo wake wa kuvutia fedha za wanaotaka mabadiriko (au wale wanohisi kuwa mabadiriko lazima yanakuja), ni tishio kubwa kwa CCM. CCM sasa inaona kuwa kuna chama chenye uwezo wa kufika kule ambako ilikuwa ni CCM pekee wenye uwezo wa kufika huko, hasa maeneo ya vijijini.

  Lakini tishio kubwa zaidi kwa CCM ni uwezo mdogo wa ku "manage" rasilmali fedha. Udhaifu huu umejikita sana ndani ya CCM kiasi kuwa kikinyang'anywa dola ndo mwisho wake. CCM ni taasisi ya kutumia tu na mara nyingi hutumia bila ukaguzi. Ni nani wa kuikagua CCM? Pengine wao walikuwa wanaona huo ubabe kama faida, lakini ukweli hiyo ni hasara kubwa mno. Ili CCM wafanye kitu chenye "magnitude" ile ile, wanahitaji fedha mara kumi zaidi ya chama kama Chadema. Kwa hiyo utaona kuwa Chadema wakiwa na uwezo wa kutumia asilimia kumi tu ya ile wanayotumia CCM, watapata matokeo sawa na yale wanayoyapata CCM. Hili kusema ukweli ndo tishio kubwa zaidi kwa CCM kuliko matishio mengine yote!

  Suala ni je CCM wanaweza kupambana na hali hii ya udahaifu katika matumizi ya fedha? Ukweli ni kuwa haiwezekani na hii ni mojawapo ya mambo yanayoifanya CCM iwe chama kisichoweza kurekebishwa. Ni kuwa 2015, madaraka yapo wazi kwa Chadema. Wakikosa watakuwa wamepoteza, ila si kushindwa!
   
 9. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #9
  Mar 15, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Si utoe ushaidi acha kubwabwaja.
   
 10. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #10
  Mar 15, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Vyama vya Siasa na NGOs zina tofauti gani? Vyama vya siasa haviruhusiwi kufanya "Fund Raising" nje ya wanachama wake wa ndani ya nchi?
   
 11. m

  mtimbwafs Member

  #11
  Mar 15, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuwa na pesa si dhambi tatizo ni kwamba watuambie ccm nao pesa zao wanapata wapi?.

  Hofu inakuja kwa kuwa siasa siku hizi ni pesa na bila pesa hakuna siasa. Je ambaye amegeuza mchezo huu ni ccm ambao wanamiliki serikali au chadema wasio na serikali???.

  Ccm ina pesa, ina dora na ina wafadhiri na wanachama wengi kuliko cdm hofu ya nini sasa, na inatoka wapi???.
   
 12. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #12
  Mar 15, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Tatizo la Serikali ya JK ni kulalamika tu, utafikiri hawana meno yoyote! Kama wanaona kuwa fedha zinazoingizwa nchini kwa ajili ya kuipatia CDM kinyume na Sheria, kwa nini wasichukue hatua ya kuwakamata? Yaani CCM kwa sasa haina tofauti na chama cha UPINZANI!
   
 13. P

  Paul J Senior Member

  #13
  Mar 15, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi woga wa CCM zidi ya CDM unatoka wapi? Kupata pesa kutoka nje ya nchi ama mahara popote kwa Chama chochote cha siasa si kosa ili mradi pesa hizo zimelenga kujenga demokrasia ya kweli miongoni mwa wananchi na kukijenga Chama chenyewe. Na hii ndiyo kazi inayofanywa na Chadema. Kwa kweli inasikitisha kuona viongozi wa chama tawala na serikali yao kila kukicha wanalalama kwenye vyombo vya habari na kikubwa zaidi wanachokiongelea ni CDM wakati yapo matatizo rukuki yanalikabili taifa, hawaoni kama wananchi tunaumia na huduma mbovu za umeme, miundombinu, maji, elimu duni, afya na mfumuko wa bei na kuporomoka kwa shilingi, CCM na serikali yake hawaoni kama haya ni matatizo bali tatizo ni CDM. Jamani M/Kiti wa CCM aliwahi kusema vyama vya upinzani ni vyama vya msimu, inakuwaje macho yenu na masikio yenu mnayaelekeza kwa CDM? Kumbuka CCM ni chama tawala na wajibu wako mkubwa ni kutatua matatizo yanayolikabili taifa kupitia ilani ya uchaguzi na kazi ya Chadema ni kukukosoa na kukuponda ilivyo pale unapokosea na kuuelimisha umma juu ya madhaifu yako na hii yote huitaji pesa. Ikumbukwe kabisa kuwa serikali ya ccm imejengwa katika misingi ya ombaomba wakati nchi ina rasilimali za kutosha na hii haiwafurahishi wafadhiri wa kweli maana nao wangependa kuiona Tanzania ikitoa misaada kwinginepo afrika, kwa hiyo inapotokea Chama makini kama CDM chenye uwezo wa kuzitumia rasilmali zilizopo wafadhiri hao lazima wakisupport ili baadaye waondokane na mzigo wa serikali ya ccm ya ombaomba!

  Hakuna namna yoyote ya kuweza kuidhibiti CDM isipate pesa toka kwa wafadhiri wake wakati serikali na chama tawala ni ombaomba wa kutupwa na ndomaana Membe hawezi kuitaja hata nchi moja inayotoa pesa kwa CDM na CDM wakikomaa na membe na Sophia Simba outcome yake mtaiona kwenye budget ya 2011/2012! Ushauri wangu wa bure kwa CCM ni ku concentrate kuondoa kero za maji, miundombinu, umeme, afya, elimu, n.k maana wananchi tumechoka na propaganda zenu!
   
 14. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #14
  Mar 15, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,827
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  tatizo ndugu zako(CCM &co),wanabwabwaja tu bila kuthibitisha madai yao.....wameshapoteza dira!
   
 15. S

  SUTU BUTUGURI Member

  #15
  Mar 15, 2011
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapana. CCM wanaogopa mapambano dhidi ya ufisadi. Kwa nini? Kwa sababu CCM na serikali yake chini ya mawakala wa mafisadi, ndiyo ufisadi. Mtu yeyote anayepambana kutomeza ufisadi ni mhaini kwa mujibu wa CCM. Alafu, kama hamjui CCM iko sahihi ktk hili. KWANI serikali ya CCM ndiyo ufisadi. Ukiangusha au ukipindua ufisadi umepindua serikali ya Tanzania. KATIKA TANZANIA ya CCM, mtu hawezi kutomeza ufisadi halafu asitokomeze serikali ya CCM.

  Rushwa ya Tanzania haina aibu. Rushwa ina baraka zote za CCM. BILA RUSHWA CCM haiwezi kutawala. Mtu yeyote apambanae na rushwa anapambana na CCM ya leo chini ya mawakala wa mafisadi. Wananchi tukilijua hili hatupata shida na vitisho vya CCM dhidi ya wapambanaji wa ufisadi. Tunapaswa pia kujua vyombo vya habari ya mafisadi: magazeti ya RAI, MTANZANIA, THE AFRICAN, UHURU, MZALENDO, TBC ...
   
 16. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #16
  Mar 15, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,125
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  kwan mazuri kuona mpinzani wakoanakukaribia?lzm mchecheto lzm uwpo. goo go go go go chadema
   
 17. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #17
  Mar 15, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Chanzo cha pesa za CDM ishapoteza uzito labda waje tena na singo ingine
   
 18. Tumaini edson

  Tumaini edson Member

  #18
  Mar 15, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kulalamika ovyo ni dalili za kushindwa, huna jinsi unaishia kulalama. Hta katka soka ukimwona mchezaji mlalamishi mno, jua kiwango kinaelekea mwisho kama c kuisha kbs. Mfano wote twamkumbuka Jimmy flloyd Hesellbaink aliyekuwa Chelsea, Diouf na sasa Gattuso. Ccm kwisha baba, usiumize kichwa kuwaza sana. Labda jiulize, ungekuwa mgombea wa ccm na huu ni mda wa kampeni ungewambia nn wa Tanzania wakuelewe?
   
 19. zimmerman

  zimmerman JF-Expert Member

  #19
  Mar 15, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 579
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 80
  Kweli kabisa. Lakini pia kuna kitu kingine ambacho kinaitisha CCM kuhusu CHADEMA. CHADEMA kina tendency ya kuwavutia members ambao wengi wao ni vijana wenye above average intelligence na pia wenye fikra huru linapokuja suala la politics za Tanzania. Kwa upande mwingine, chama kichovu kifkra na kiuongozi kama CCM, kinachofanya blunders kila kukicha katika masuala muhimu na nyeti kwa uchumi wa nchi, hakiwezi kuvutia watu makini zama hizi. Hivyo, wengi wa mashabiki wa CCM zama hizi ni maopportunists wanaojiunga na CCM kwa lengo la kupata favor fulani fulani hivi (si unajua ukiwa na kadi ya CCM most likely things will go smooth on you -- or so they think?), au wenye udini na ukabila uliokithiri.

  Sasa suala linakuja kuwa overtime CHADEMA ina accumulate finest people of the country wakati CCM inaaccumulate majambazi (Rostam), wapuuzi (Sophia Simba), vilaza (the so called president) na maopportunists wengineo wengi. Na hiki kinaitisha sana CCM.

  Matokeo yake nini? CCM hawana jinsi bali kubakia kutapatapa kwa vitisho na visingizio. Na hapo ndo linapokuja visingizio vya huyu mama mpuuzi kweli kuwa mabalozi wanaifinance CHADEMA. It's just so pathetic to have these people being leaders of our country. God forbid it come 2015!
   
 20. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #20
  Mar 15, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Hapo sasa!
   
Loading...