Hofu ya CCM ni ipi hasa juu ya Zanzibar, Mameya wa UKAWA?

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
20,054
23,505
Mwenye kulielewa hili atujuze ni nini hofu kuu ya CCM juu ya kumuachia mshindi wa urais wa ZNZ ushindindi wake!
Pia tunaona hata katika uteuzi wa mameya CCM Imekuwa ikijiumauma kuiachia hali halisi ifuate mkondo wake,IPI NI HOFU KUU KWA CCM KUOGOPA KUUACHIA UMEYA!
 
Ma ccm yashasema hadharani, nanukuu 'serikali ya kimapinduzi haiondolewi madarakani kwa sanduku la kura,labda kwa kuipindua.na kuipindua hamuwezi.....'.mwisho Wa kunukuu.
 
Mwenye kulielewa hili atujuze ni nini hofu kuu ya CCM juu ya kumuachia mshindi wa urais wa ZNZ ushindindi wake!
Pia tunaona hata katika uteuzi wa mameya CCM Imekuwa ikijiumauma kuiachia hali halisi ifuate mkondo wake,IPI NI HOFU KUU KWA CCM KUOGOPA KUUACHIA UMEYA!

kuna pesa ndefu sana huwa inapigwa kwa kisingizio kuwa inapelekwa zanzibar lakini kiukweli haiibgii kwenye mfuko wa wazazibar sasa akiingia MTU mwingine atawaumbua....
kwenye halmashauri kuna mirija kitendo cha kuchukuliwa na ukawa maana yake inaenda kukatwa
 
Mwenye kulielewa hili atujuze ni nini hofu kuu ya CCM juu ya kumuachia mshindi wa urais wa ZNZ ushindindi wake!
Pia tunaona hata katika uteuzi wa mameya CCM Imekuwa ikijiumauma kuiachia hali halisi ifuate mkondo wake,IPI NI HOFU KUU KWA CCM KUOGOPA KUUACHIA UMEYA!
Jibu lake ni rahisi tu, kwa kuwa CCM wanaamini kuwa Mwenyezi Mungu amewapa wao hati miliki ya kuitawala nchi hii hadi mwisho wa dunia!
 
Ndiyo maana Profesa Lipumba aliwalinganisha hao CCM na Intarahamwe.
Kwa kuwa wao CCM wako tayari waendelee kukaa madarakani hata kama damu inaweza kumwagika.
Mifano halisi ni uchaguzi wa Zanzibar na uchaguzi wa Mameya Kinondoni, Ilala na Jijini Tanga.
Kwa upande wa Zanzibar inaeleweka wazi kuwa Jecha alishinikizwa na viongozi wa CCM ayafute matokeo baada ya kuyapata matokeo yote na kugundua kuwa Maalim Seif amembwaga Dr Shein kwenye kinyang'anyiro cha Urais.
Kwa upande wa Umeya, CCM walipobaini kuwa idadi ya madiwani walionao katika Halmashauri za Kinondoni na Ilala haziwezi kuwabeba kupata Umeya, wakaamua 'kuwa-import' madiwani mamluki kutoka Zanzibar.
Kwa upande wa Jijini Tanga, msimamizi wa uchaguzi aliamua kufanya 'uharamia' kwa kutangaza matokeo vice versa. Kwa kuwa kwa mujibu wa wakala wa CUF aliyekwenda kuhesabu kura za Umeya kurudi ukumbini akiwa na matokeo ya mgombea wa CUF akiwa amepata kura 20 na mgombea wa CCM akiwa amepata kura 17.
Kwa mshangao wa kila mjumbe aliyekuwemo ukumbini humo, msimamizi huyo 'kada mbobezi' akatangaza kuwa mgombea wa CCM amepata kura 19 dhidi ya kura 18 za mgombea wa CUF!
 
Back
Top Bottom