Hofu/Woga ni adui mkubwa kuliko ugonjwa wowote duniani

Monster20

Senior Member
Nov 30, 2020
160
159
Kwanza nitoe pole kwetu sote wakati huu wa majonzi ya kumuaga mpendwa wetu.
MUNGU amrehemu.

Kwa uzezo wangu mdogo wa kutafakari mambo nimegundua Viongozi walitukosea sisi wanainchi sana. Siku chache kabla ya msiba huu, mitandaoni kulikuwa na taharuki ya kiwando cha juu sana juu ya afya ya Rais wetu.

Taharuki hiyo ilipozidi sana tukafarijiwa na viongozi wetu wa juu kuwa rais ni mzima na anachapa KAZI ...... ametutaka na sisi tuchape kazi(kumbe si kweli).

Marehemu amekuwa muumini mzuri sana wa kuamini MUNGU yupo na tukimwomba kwa jambo lolote kama nchi, kwa umoja, anatusaidia. Tumeona akilisisitiza hili kwenye swala COVID - 19, ambapo alitupa ujasiri wa kufanya maombi, na nithubutu kusema alifanikiwa, tukavuka kwenye swala la covid.

WOGA/HOFU
J
e haikuwa jambo jema kuwaambia wanainchi Rais wetu anaumwa, sote kwa pamoja tumkaribidhi kwa MUNGU kwa maombi. Kulikuwa na hofu gani kuwaambia wanainchi ukweli juu ya afya ya rais?

Je kuambiwa tumuombee kama yeye alivyokuwa akiamini katika maombi kungevuanja amani ya nchi? Je ulikuwa woga/hofu kwamba tukiwambia wanaicnhi halafu akapona, watafukuzwa nyadhifa zao?. Ni nini basi kilifanya kuugua kwa rais kuwe siri kuu?.

MUNGU ampumzishe kwa amani. Nafikiri kuna somo tumejifunza.
 
Huyo marehemu ndio ilikuwa zake kuendesha nchi kwa usiri mkubwa, uwongo na hofu,

hata vyombo vya hapa nyumbani hakuna hata kimoja kilichothubutu kuulizia alipo marehemu sababu vingefungiwa

Hata hiyo Corona aliyowadanganya imeisha ndio iliyomuondoa

Uwongo na propaganda ndio adui mkubwa kuliko ugonjwa wowote Duniani
 
Huyo marehemu ndio ilikuwa zake kuendesha nchi kwa usiri mkubwa, uwongo na hofu,

hata vyombo vya hapa nyumbani hakuna hata kimoja kilichothubutu kuulizia alipo marehemu sababu vingefungiwa

Hata hiyo Corona aliyowadanganya imeisha ndio iliyomuondoa

Uwongo na propaganda ndio adui mkubwa kuliko ugonjwa wowote Duniani
MAREHEMU AMEMALIZA ALIYOYATANGULIZA HIVYO NI JUKUMU LETU KAMA BINADAMU KUMUENZI KWA MEMA YAKE YOTE ALIYOYAFANYA.
 
Back
Top Bottom