Hofu wafanyakazi 600 kupoteza ajira Uwanja wa Ndege Zanzibar

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,023
1,609
CHAMA cha Waendeshaji Ndege Tanzania (TAOA) kimetoa siku saba kwa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kusitisha uamuzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA) wa kuiteua Kampuni ya DNATA toka nchini Dubai kuwa mtoa huduma pekee katika jengo la tatu la (Terminal III) la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.

Kwa mujibu wa notisi ya Septemba 14, mwaka huu ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar na Kampuni ya DNATA kutoka Dubai, ndiyo itakuwa mtoaji huduma pekee katika jengo la tatu la (Terminal III) pamoja na huduma ya mizigo na Marhaba Lounge kuanzia Desemba mosi, mwaka huu.

Kutokana na hatua hiyo wafanyakazi karibu 600 wapo katika hatari ya kupoteza ajira kutoka katika Kampuni ya huduma za Uwanja wa Ndege (ZAT) pamoja na Kampuni ya Trans Word zinazotoa huduma uwanja huo wa kimataifa wa AAKIA.

TAOA imechukua hatua hiyo kwa mujibu wa indhari (notisi) ya Oktoba 10, mwaka huu, waliyoitoa kupitia Kampuni ya huduma za sheria ya B/E AKO LAW kabla ya kuchukua hatua za kisheria za kufungua kesi mahakamani kupinga uamuzi uliofanywa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar kwa madai ya kufanyika kinyume na sheria.

Waraka uliotolewa na Chama cha TAOA umeeleza hayo kisiwani hapa.

Sehemu ya waraka huo umesema unaelewa kuwa zabuni ya ununuzi wa utoaji wa huduma umechapishwa kinyume na Sheria ya manunuzi na kanuni zilizopo za huduma za utunzaji wa ardhi jambo ambalo linaandika historia ya hatari katika sekta ya Anga Tanzania.

TAO imesema kwa mujibu wa sheria ya usafiri wa anga Tanzania sura ya 80 R.E ya mwaka 2020 kifungu cha 30(e)(II), Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA) ina majukumu ya kuwajengea maarifa kwa umma, ufahamu na uelewa ili kudhibiti sekta na kushughulikia migogoro.

“Chini ya kifungu cha 31(1) cha sheria hiyo TCAA ina wajibu kutoa, kuhuisha, kubadilisha au kufuta leseni za huduma za anga na utatuzi wa migogoro na malalamiko kadri yanapojitokeza,” ilisisitiza TAOA.

TAOA wamekiita kitendo cha DNATA kuteuliwa kuwa watoa huduma pekee katika Jengo la tatu (Terminal III) ni sawa na serikali kukaribisha sheria za ukiritimba na kuvunja ushindani.

Aidha, kifungu cha 45(2) cha Sheria TCAA, kinataja mamlaka ya kufanya uchunguzi kabla ya mamlaka ya kutoa, kufanya upya au kufuta leseni.

TAOA iliitaja kifungu cha 46 cha sheria kinaitaka TCAA kuzingatia na kusimamia masharti ya ushindani mzuri, yanakuwapo katika soko kwa ajili ya kuepusha mambo yoyote yanayoweza kuathiri ushindani na kuleta madhara kwa umma na maendeleo ya sekta ya anga.

“Katika ufahamu wetu wa sheria ZAA haijapewa mamlaka ya kutoa upendeleo katika uwanja wa Ndege wa AAKIA kwa vile mamlaka hayo sio ya kukabidhiwa kiutawala, TCAA imeshindwa kusimamia majukumu yake.”

Vile vile, imetajwa kanuni ya 20 ya usafiri wa Anga (Ground handiling services) ya mwaka 2012, taratibu za uteuzi zinahitajika ili kushughulikia ardhi katika viwanja vya ndege na kuzingatia kanuni za uwazi, zisizo na ubaguzi wa utoaji wa zabuni ya ushindani wa kimataifa na kuepuka upendeleo.

Wakifafanua zaidi wameleeza; “Kutoa upendeleo ni jukumu ambalo wamepewa TCAA ambalo mamlaka yake hayawezi kukosolewa na kitendo cha TCAA na kushindwa kuingilia kati suala hilo ni sawa na kutengua majukumu yake.”

Wanasiasa na wanaharakati wamekuwa wakipinga tangu kuanza kwa mchakato wa kupewa kazi ya kutoa huduma Kampuni ya DNATA na biashara za maduka kufanywa na wazawa ili kulinda ajira akiwamo mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha ACT-Wazalendo, Ismail Jussa Ladhu.

Juhudi za kumpata Mkurugenzi wa Mmalaka ya Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari kupitia simu yake ya mkononi hazikuweza kufanikiwa licha ya indhari ya siku saba ya TAOA kumalizika Oktoba 19, mwaka huu.


Chanzo: Nipashe
 
Pole yao..wapambanie waendelee na kazi...tunawaombea kheri.

#MaendeleoHayanaChama
 
....Yaani Kampuni mpya kutoka Dubai ikitaka kuanza Kazi yake Hapo ni Lazima iwastaafishe Wazawa 600 kwanza?
Kwani wanakuja na Wafanyakazi Wao wapya 600?
Hizo Kazi 600 atafanya nani?
Kwani muwekezaji mpya hawezi 'kurithi' Ajira 600 za Wazawa aliowakuta??
Maswali ni Mengi..,
Anaweza kuchukua karibu nusu yao au zaidi.... navyoona ni kuwa kuna taratibu zimekiukwa, au hao 600 hawana uhakika nani ataingia na nani atatoka...
 
AAKIA ina sehemu tatu... Jamaa zetu toka Dubai wameshinda zabuni katika sehemu ya tatu Termnal III ....

Kuna Terminal I and II ...Zat waende huko..
 
Yaani raha kama nini, huenda tukawa kama Uarabuni.

kama Ulaya yametushinda hatuyawezi wabakie nayo wenyewe, mambo ya nanihino kwao ndio maendeleo.
 
Back
Top Bottom