mwl. mziray
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 597
- 398
Habari wanaJf.
Tukiwa kama wazazi/walezi wa wanafunzi wa kike wanaosoma shule za bweni kuna mambo ambayo hatuyafahamu lakini yanatendeka na ni hatari kwa afya za binti zetu na kitaaluma pia.
1.Wanafunzi wengi hugeuzwa wake wa walimu pindi wanapojiunga na shule za bweni. Baadhi ya walimu hao wanaishi na VVU.
2.Wakati wa kufunga shule/kufungua yapo mengi ambayo hutokea. Baadhi ya binti zetu hawaendi shuleni/nyumbani moja kwa moja. Baadhi hupitia kwa wanaume (watu wazima) wanaowapotosha na kujiingiza nao ktk mapenzi. Ni vyema mzaz kupata taarifa zote pindi mtoto asafiripo kwenda/kutoka shuleni.
3.Ruhusa za kuumwa zitolewazo mashuleni katikati ya masomo ni hatari sana kama hakuna mawasiliano na mzazi/mlezi. Baadhi ya wanafunzi hutumia mwanya wa kusingizia ugonjwa na kupewa ruhusa kisha kwenda kuweka kambi kwa mwanaume halikuwa wazaz wanajua binti yao yupo shuleni. Walimu tuwe makini hapa.
4. Mahusiano ya kimapenzi baina ya wanafunzi wenyewe. Jambo hili ni hatari sana kwani zipo baadhi ya shule hazikemei jambo hili hivyo huonekana kama desturi kwao.
Tufahamu siku hizi wapo watoto wanazaliwa na VVU na wao pia wanasoma ktk shule hizihizi na nivigumu kuwatambua. Ktk mazingira ya shule wanafunz hawana muda wa kububua kinga hivyo wapatapo mwanya lolote laweza kutokea na maambukizi kusambaa.
5.Matumizi ya dawa za kulevya ktk mazingira ya shule. Hata bint zetu huingia ktk mkumbo huu ambapo nilishuhudia wanafunzi wa kike wakitumia "valium" na "ugoro" kama kilevi wakishirikiana na wanafunzi wa kutwa. Pia wengine hutumia viroba na hivi hudhihirika siku ya disco shuleni.
Kwa muda mrefu nimekuwa nikishuhudia mambo hayo ktk shule za sekondari za bweni/hostel tangu nikiwa mwanafunz mpaka sasa ni mwl.
Mambo haya huchangiwa na utawala mbovu kuanzia mkuu wa shule ambapo pengine huweza kujihusisha na baadhi ya vijitabia hivyo.
Ni jukumu la wazazi kufanya tafiti mbalimbali kabla ya kuamua kuwapeleka wanafunzi wao ktk shule fulani.
Nawasilisha .